google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KARAMA YA MUNGU HAINA MAJUTO - SEHEMU YA PILI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 01.09.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KARAMA YA MUNGU HAINA MAJUTO - SEHEMU YA PILI

Kila mtu kuna karama ambayo Mungu kaweka ndani yake aje kutimiza duniani. Sio kila ulicho nacho kinatokana na elimu yako, ulicho nacho umepewa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu. Ukijihusisha na chochote ambacho sio chako kitakuwa ni cha muda tu, ni Mungu tu ndio anajua utamalizaje kwa sababu anajua mwisho wako tangu mwanzo. 

"Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote." Isaya 46:9-10

Karama ambayo Mungu ameweka ndani yako ina uwezo wa kufanya mambo makubwa sana. Karama ni uwezesho wa ki Mungu anaopewa mtu ili aje atimize kusudi aliloitiwa duniani.

Mbinguni wanakujua tofauti na unavyojiona wewe. Wewe sio muoga, maskini wala dhahifu, wewe ni jitu umetoka mbinguni unakazi ya kufanya duniani. Jambo likienda mahali ambapo wewe huwezi kufika usifikiri halipo, neno la Mungu juu yako li hai na analiangalia neno lake apate kulitimiza. Neno ndio asili na neno ndio kila kitu.

"Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize." Yer 1:12

Kuna kiu ndani ya moyo wa mtu inajazwa na neno la Mungu. Mafanikio ni kutimiza kile kilichokuleta duniani. Kiu uliyokuwa nayo itii hiyo, hilo ndilo ambalo Mungu alipanda ndani yako. Na kwenye kila kiu, Mungu anakupatia mtu ambaye ukiambatana nae hadi mwisho unaongezeka kama alivyo yeye, na akipungua utapungua kulingana nae.

Joshua alikuwa na kiu ya kuwa karibu na Musa, kwa sababu wito wake ulikuwa ni kuongoza bila yeye kujua. Hata kabla hujaitwa unakuwa na kiu, Musa alikuwa na kiu ya kuwasaidia wayahudi wenzake.

“Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga. Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako? Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana.” Kutoka 2:11-14.

Mungu akikuita jambo fulani kuna kiu unasikia, kuna wengine kiu yao ni kutengeneza pesa, wengine wameitwa kwenye eneo la siasa, mungu amependa kiu ndan ya kukuonesha utakuwa nan baadae fuata kiu yako.

Kwenye kila karama nzuri ambayo Mungu ameweka ndani yako kuna madhabahu za kishetani ambazo zitasimama kuzuia ambazo lazima uzivunje ili ufikie hatima yako. Mungu anamwambia Gideoni abomoe madhabahu ya Baali iliyosimamishwa Ofra. 

"BWANA akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa. Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri. Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng’ombe wa baba yako, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng’ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata." Waamuzi 6:23-26

Kuna vita hata kama ukikimbia unapelekwa kwenye uwanja wa mapambano kwa sababu unamiliki kwa kupigana. wewe ni yule ambaye biblia imekusema si kama watu wanavyokuona, karama yako inaweza kuzalisha biashara, kampuni nk. Pia kwenye kila karama ndani ya mtu Mungu ameweka mtu wa kukutengenezea njia kuelekea kwenye hatima yako.

Ili kuiendea karama ambayo imefungwa na madhabahu ya shetani, ni lazima uivunje kwa mamlaka tuliyopewa katika jina la YESU. 

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments