google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VITA VYA HATIMA - SEHEMU YA TATU

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 26.05.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMOVITA VYA HATIMA - SEHEMU YA TATU

Namna utakavyokuwa baadae ndio kitu kinaitwa hatima utaishiaje/ utamalizaje baadae. Mungu anakuona kwa namna utakayoishia sio kwa unavyoonekana leo, mambo yote unayoyapitia ni njia ya kufikia au kuwa yule uliopangiwa kuwa, kila mwenye hatima kubwa kuna matukio anayapitia ni makubwa kiasi cha kuhisi Mungu amemuacha lakini unatengenezwa kuwa yule unaetakiwa kuwa.

Mungu anaweza kuwatumia wachawi kukufanyia mambo ambayo ni kwa ajili ya kukutengeneza kuifikia hatima yako, sio kila jambo linalokupata ni limetoka kwa shetani, mambo mengine Mungu anawatumia ili kukutengeneza kwa ajili ya hatima yako aliokupangia kuwa. Mungu anaweza kuwaonyesha wachawi namna utakavyo ishia na kutumia vinywa vyao kukubali kwa niaba ya Mungu. Mungu anawatumia hao kwa ajili ya utukufu wake wameandaliwa na Mungu kukunoa kuifikia hatima yako.

“Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa Israeli walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua”. Yoshua 13:22

Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. “Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba, ukaniandalie hapa ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba. Balaki akafanya Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima. Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. BWANA akatia neno katika kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno haya. Akarudi kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote wa Moabu pamoja naye. Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli. Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye BWANA hakumshutumu? Akarudi kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote wa Moabu pamoja naye. Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli. Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye BWANA hakumshutumu? Kutoka kilele cha majabali namwona; Na kutoka milimani namtazama; Angalia, ni watu wakaao  peke yao, Wala hawatahesabiwa pamoja na mataifa. Ni nani awezaye kufanya idadi ya mavumbi ya Yakobo, Au kuhesabu robo ya Israeli?

Na nife kifo chake mwenye haki, Na mwisho wangu uwe mfano wa mwisho wake. Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, Kutoka kilele cha majabali namwona; Na kutoka milimani namtazama; Angalia, ni watu wakaao peke yao, Wala hawatahesabiwa pamoja na mataifa. Ni nani awezaye kufanya idadi ya mavumbi ya Yakobo, Au kuhesabu robo ya Israeli? Na nife kifo chake mwenye haki, Na mwisho wangu uwe mfano wa mwisho wake. Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.  Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile BWANA atialo kinywani mwangu?.” Hesabu 23:1-12

“Balaamu akamwambia Balaki, Je! Sikuwaambia wajumbe wako ulionipelekea, nikisema, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi. Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa watakayowatenda watu wako siku za mwisho. Aguzi la Nne la Balaamu Akatunga mithali yake akasema, Balaamu mwana wa Beori asema,; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na Yule mtu aliyefumbwa macho asema, Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho, Namwona, lakini si sasafimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.” Hesabu 24:12-17

Namna Yesu alivyoishia kulijulikana miaka 700 kabla yeye kuzaliwa na magumu yote na mateso yalionekana kabla hajazaliwa, alijulikana atakuwa nani au ataishia nani kabla hajazaliwa, mambo yote yanayompata mtu hujulikana kabla hajazaliwa. Watu wa Mungu wanaweza kujua utakuwa nani au utaishia kuwaje kwa kuongozwa na roho. 

“Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.” Isaya 7:14

“Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.” Isaya 52:14-15

“Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Isaya 53:3-5

Anayekukera ameandaliwa na Mungu kwa ajili ya kuitengeneza kesho yako, haijalishi unapitia mangapi lakini kile alichokipanga Mungu kiwe kwa ajili yako kitatimia tu, hakuna mtu anaweza kubadilisha kile Mungu ameandaa kwa ajiri yako kitatimia tu. Mambo yote unayoyapitia sio kwamba umekosea ila Mungu anayaruhusu yakupate kwa ajili ya kukujengea tabia ya kesho yako. Ulicho andikiwa wewe hakuna mwanadamu alie hai anaweza kuzuia kikifikia kile ulicho andikiwa, ukiinuliwa na Mungu hakuna mwanadamu atakaeweza kukushusha ila Mungu huwashusha wale wote wanaojikuza na Mungu huwapinga wenye kiburi.

Mwenye kesho kubwa hata ukumuona anataji la miba analo tu kwa muda, mwenye kesho kubwa hata kama hana nguo ni kwa muda tu, mwenye kesho kubwa hata kama ana dhiki sana ni kwa muda tu, ila kesho yake ipo pale pale ni swala la muda tu ataiishi hatima yake alioandaliwa na MUNGU.

Mungu atawaangamiza wote watakaonyoosha mkono kuizuia hatima yako aliokuandalia, maana Mungu anatimiza makusudi yake kupitia wewe anafanya kile anataka kitimie au kitendeke kupitia wewe upo duniani kwa niaba ya Mungu kwa hiyo yoyote atakaeinuka kukuzuia Mungu atamkatilia mbali.

“Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakaonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi.” Ezra 6:12

Post a Comment

0 Comments