google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATUKIO YA KICHAWI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 09.06.2024
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MATUKIO YA KICHAWI

Unaweza ukaziona balaa ukafikiri ni asili ya mwanadamu kumbe ni balaa ya kichawi.

“Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; kama Eliya naye alivyofanya.” Luka 9:54

Sio kila moto ni moto kuna moto mwingine ni wa kutengeneza.

“Ndipo mfalme akatuma akida wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka. Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake. Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.” 2 wafalme 1:9-11

“Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.” Ufunuo 13:11-15

Shetani anaweza kuagiza moto kutoka mbinguni ila si mbingu ya Jehovah, kuna matukio ya kichawi na kuna uhai wa kichawi na ndio maana mchawi anakunywa damu ili uchawi uhuishwe, anakunywa damu kwa sababu shetani hana kinachotokana na yeye kila anachokifanya anaiga kutoka kwenye uhalisia.

Kila mmoja ana kipaji maalumu na lile eneo lenye kipaji ndio shetani anahangaika nalo, kila anayekuja kutoka juu anakuwa amwepewa vifaa vya kutimiza wito wake, wewe hauishi kwa bahati mbaya, wewe ni mpango wa Mungu kamili.

“Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.” Ayu 1:8-12

Kuna watu wamechukua moyo wako wanatumia mahali, wewe sio kwamba huna akili ni kwamba wamechukua, unaona miguuu inawaka moto je miguu yenyewe unayo, usishangae ukaona unaenda mahali unakatakiwa kumbe huna kibali wamechukua na kutumia katika shughuli zao. 

Kuna uchawi wa aina  tofauti tofauti:

  • White magic - Uchawi wa kubadilika badilika ni kama mazingaombwe, mazindiko ni uchawi, uchawi ni kama serikali ina vitengo tofauti tofauti, kila shida uliyo nayo ina chanzo cha rohoni, shetani ana uwezo wa kuona yajayo ndio maana anashindana na wewe, Mungu akiwa na haja na wewe hata kama wakikuloga kuanzia asubuhi mpaka jioni atakuokoa.

  • Black magic - Uchawi wa waziwazi, matumizi ya nguvu za kichawi kwa madhumuni mabaya, ya uharibifu na ya ubinafsi.

Kinachofanya shetani apate nafasi ya kukuloga ni dhambi, dhambi ndio chanzo cha yote, ukitaka Mungu akufungue cha kwanza ondoa dhambi, hakuna tatizo ambalo linatokea lenyewe matatizo yote yanatokea rohoni ukiharibu chanzo unapona tatizo.

Post a Comment

0 Comments