google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SABABU ZA KWANINI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
SEMINA YA VIJANA, ALHAMISI, 18/07/2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: SABABU ZA KWANINI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA

Mambo huonekana magumu sana kwa mtu ambaye hana maarifa, na kwa sababu hiyo watu wengi sana huwa na maisha yasiyo na matokeo mazuri kwa sababu walipuuzia kutoa jasho kwa ajili ya kutafuta maarifa.

Moja ya sifa kuu ya dunia hii ni kwamba inalaana, lakini maarifa yanaweza kupunguza ukali wa laana kama ukikubali jasho likutoke kuyatafuta maarifa. Nimuhimu kufahamu kuwa ujinga hauwezi kabisa kukuruhusu ufanikiwe na pia maarifa ya eneo moja lenye mafanikio hayawezi kuhamishika pasipo kuamua kutoa muda wako kuyaendea maarifa na kujifunza.

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria” Hosea 4:6

Mtu anayejifunza ni uhakika kwamba wakati wa mafunzo huwa yuko sawa na yule asiye jifunza. Lakini baada ya muda fulani wa mafunzo, atatofautishwa na yule asiye kuwa na maarifa kwa sababu ya kupuuzia mafunzo, kwani wakati huo yeye ana kitu anakijua kutokana na mafunzo aliyoyapata. 

Unaweza kupuuzia maarifa lakini huwezi kupuuzia matokeo ya kupuuzia hayo maarifa. Kwa sababu ilikufanya maamuzi sahihi ni lazima kuwa na kitu unacho kijua kwanza ndipo ufanye uchaguzi sahihi. Maisha yanaongozwa na kanuni, ni muhimu sana kuwa na maarifa ambayo unayajua na kuyaamini na ndipo kujiwekea kanuni zitakazoongoza maisha yako.

Kuishi maisha ya kiholela, yaani bila kanuni ni kuyaharibu maisha yako kabisa, kwa hiyo ni muhimu kujiwekea mipaka ili uweze kuwa na maisha ya usafi na yenye mafanikio.

SABABU ZA KWANINI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA.

  • Sex kabla ya ndoa huwafanya watu wasiaminiane tena hata kupelekea kuvunjika kwa mahusiano;

Kuaminiana ni nguzo na msingi imara unaojenga mahusiano ya muda mrefu. Itawagharimu sana kuishi kwa upendo na kuaminiana kama kuna sex ilihusika kipindi cha uchumba, Kwani ndoa nyingi zinazodumu hutokana na wanandoa kuaminiana wao kwa wao tangu mwanzo wa mahusiano yao. Uaminifu unagharama ingawa upendo ni bure, hivyo ni muhimu kutunza uaminifu kwani gharama yake ni kubwa sana.

“Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema. Nami nitakuposa kwa uaminifu; nawe utamjua BWANA.” Hosea 2:19-20

  • Sex kabla ya ndoa ni kuivunjia heshima taasisi ya ndoa;

Kuna mambo huyafanyi kwa sababu hauna vigezo vya kufanya mambo hayo, hivyo kufanya hivyo ni kuivunjia heshima taasisi husika. Mungu ameweka sex kuwa halali na ifanyike ndani ya ndoa pekee, hivyo ni chukizo kufanya sex nje ya ndoa.

Namna mbili za kuiheshimu ndoa;

  1. Kutokufanya Uzinzi na uasherati kabisa.
  2. Ndoa ni baina ya watu wawili wenye jinsia tofauti.

“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia” Waebrania 13:4

  • Sex kabla ya ndoa huharibu dhamiri yako na kuwa na hatia endelevu inayohatarisha ndoa yako;

Wapo watu ambao wamedhamiria kutokufanya sex mpaka waoe au waolewe, kwa hiyo ikitokea mtu wa aina hii akafanya sex, dhamiri yake itamhukumu na kuwa na hatia hata baada ya kutubu na kuingia kwenye ndoa kiuhalali. Hivyo kupelekea mtu kutokuifurahia ndoa yake kabisa kwa sababu ya dhamiri iliyo na hatia mbele za Mungu  na watu.

 “Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.Matendo 24:16

  • Sex kabla ya ndoa huwa sababu ya jina la Mungu kutukanwa;

Hii ni kwa sababu mambo ambayo watu wa mataifa hufanya, wakiona mtu aliyeokoka anafanya pia huleta sura mbaya ya wokovu na watu huacha kumtukuza Mungu. Kwa sababu mtu aliyeokoka lazima ajitofautishe kwa matendo na mienendo yake ili Mungu atukuzwe.

“Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu? Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati? Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.” Warumi 2:22-24

Kumheshimu Mungu ni Pamoja na kufuata yale yote ambayo ameyaagiza, kushindwa kujizuia kufanya sex kabla ya ndoa ni uasi kinyume na Mungu na pia huwafanya watu kukudharau.

“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.” 1Timotheo 4:12

Kumheshimu Mungu huanza na nidhamu yako binafsi, uwezo wako wa kukataa, na kujizuia kufanya yale yaliyo kinyume cha Mungu, ni pamoja na kueneda katika usafi wa mwili na roho.

“kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.” 1Thesalonike 4:4

Post a Comment

0 Comments