google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SABABU ZA KWANINI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
SEMINA YA VIJANA, ALHAMISI, 25/07/2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: SABABU ZA KWANINI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA

  • Inaweza kukuletea urahibu (addiction).Kila mwenye urahibu haikuanza tu, lakini kwa kufanya kitu kile kile mara kwa mara. Mwili unapozoeshwa mambo kuyaacha inakuwa kazi ngumu sana pamoja na kujua madhara yake. 

“Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.” Zaburi 141:4

Namna ya kushinda urahibu wa kufanya sex kabla ya ndoa ni kutokuanza kabisa ili usiizoelee.

  • Ili kuepuka kutoka nje ya ndoa hata ukiwa kwenye ndoa.
Mtu anayeanza sex kabla ya ndoa ni rahisi kutoka nje ya ndoa. Uwezo wa mtu kutotoka nje ya ndoa hupimwa kabla ya ndoa akiwa kwenye uchumba kwa kutokufanya sex kabla ya ndoa. 

Mtu anayeweza kuzuia hisia za kufanya sex kabla ya ndoa amefuzu hata akiwa ndani ya ndoa anaweza kudhibiti tamaa ya kutoka nje ya ndoa.

Jaribu la kutoka nje ya ndoa ni endelevu kwa wanaume wote. Hata ukioa kama haujaudhibiti na kuuweza mwili wako basi utatoka tu nje ya ndoa ukiwa kwenye ndoa. Udhihirisho wa kuwa utalishinda jaribio la kutoka nje ya ndoa ni ukiweza kuushinda mwili kwenye uchumba.

“Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.” 1 Wakorintho 7:3-5

Kuna mazingira ambayo inakuwa ngumu kupata sex hata ndani ya ndoa mfano mwenzi wako akiwa mgonjwa, yupo mbali na wewe nk, kama huwezi kujizuia inakuwa rahisi wewe kwenda kutafuta sex nje ya ndoa.

  • Inaweza kuondoa shauku ya kuoa.
Moja ya sababu inayofanya vijana kuoa ni ili kutimiza hitaji la msingi bila kuvunja sheria ya Mungu. Kijana anayepata sex kabla ya ndoa anakuwa hana shauku na ndoa maana anapata hitaji lake la msingi kabla ya ndoa.

Kibiblia ndoa ni sababu ya msingi watu kukimbia uzinzi na kutokumtenda Mungu dhambi.  

“Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.” 1 Wakorintho 7:2

“Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.” 1 Wakorintho 7:8-9

Inatakiwa uipate ndoa mkiwa wadogo, mnakuwa pamoja kwenye ndoa. Ili kuepuka kuzoea ndoa epuka kufanya sex kabla ya ndoa.

“Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.” Mithali 5:18

Post a Comment

0 Comments