google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANGU ASILI (BWANA AMEKUCHAGUA 2)

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 14.07.2024
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: TANGU ASILI

Kwenye biblia kuna mianzo mingi, kwa mfano: ukisema hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi au hapo mwanzo kulikuwa na neno naye neno alikuwa kwa Mungu, huo ni mwanzo wa kitu fulani, watu wengi huwa wanawaza kwamba wewe ulianza siku ulipozaliwa na mama yako na utaishia siku utakapofariki, lakini jambo usilolijua ni kwamba mwanadamu ni kiumbe wa milele. Mwanadamu pekee ndio anaweza kufanya kazi sehemu mbili, yaani ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili. Kila mtu unayemuona mwisho wake ulishaamriwa tayari na yule anayejaribu kushindana na wewe anapoteza muda. Liko jambo ambalo kila mtu kapewa ili alifanye duniani.

Bidii uliyo nayo si yako umewekewa na Mungu ili uwe yule uliyepangiwa kuwa. Utele uko ndani ya muda, kwa nini watu wanakosea? wanataka wapate utele nje ya muda wao. Hapa ulipo wewe una vitu ndani yako hivyo unatakiwa ujipe muda ili uwe kwenye mazingira ya kupata.  Ukiwa unachota maji mtoni halafu mamba anataka akukamate, anakukamata anakutupa kwenye maji, akikutupa wewe unaishiwa nguvu yeye anakuwa na wepesi kwa sababu yupo kwenye eneo lake.

Kuna aina ya nyoka wanaitwa mamba akikugonga ndani ya dakika tatu unafariki na ana uwezo wa kukimbia kwa km ishirini kwa saa. Sasa siku moja akaja tai akamnyakuwa akaenda nae juu sana, ghafla akamuachia, na nyoka hawezi kupaa. Tai akamdaka halafu akamuachia tena, hii ina maana gani siku utakapofikishwa kwenye eneo si lako tayari umeshauwawa. Sisi watu wa Mungu eneo letu ni neno la mungu.

Ili shetani ashughulike na wewe anakupeleka kwenye eneo lake, uwanja wa mipango ya haraka. Kila mtu ameshapangiwa atakuwa nani baadae na hakuna mwanadamu atakayezuia wala atakayekuuwa, kuna watu unasubir sana halafu unakufa moyo,

"Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda." 2 timotheo 2:6

Kwenye kupandwa, nyakati ngumu ni sehemu ya maisha kabisa. WAKATI MGUMU HAUDUMU ILA WATU WAGUMU WANADUMU, kila unayemuona na yuko juu kuna wakati mgumu alipitia ili umjenge. Ukitaka mafanikio ya haraka huwezi kupata, nda ndio maana kuna wezi kwa sababu hawataki kusubuiri wakati wao ufike.

“Wapandao kwa machozi, watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, aichukuapo miganda yake.” Zaburi 126:5-6

Kwenye shamba moja unaweza kupanda mazao mabli mbali, kuna choroko, kuna maharage, lakini yamepandwa, kile kilichowekwa na Mungu kiko ndani yako kinatakiwa kifike mahala sahihi na ndio hapaa unatakiwa umwagiliwe uote.

"Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma." Yakobo 5:11

Haukuanza siku ulipozaliwa ulikuwepo hata kabla hujazaliwa. Yesu anawaambia watu alikuwepo hata nyakati za Ibrahimu, hii ilikuwa kwa sababu mtu haanzi kuwepo akizaliwa kwenye mwili.

"Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. 57Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni." Yohana 8:51-59

Ukimuona mtu na miaka yake usihesabu miaka ya ganda la nje (mwili) maana kabla hajazaliwa alikuwepo. Yesu kabla hajazaliwa alikuwepo na wewe kabla haujazaliwa ulikuwepo. Sura yako inatoka kwa baba na mama lakini wewe ulitoka mbinguni. Mungu amekuchagua kwa ajili ya jambo fulani ambalo hata wewe hujajua bado bali tu ndani yako roho inapepea kufanya jambo fulani hilo ndilo Mungu alilokuitia. Zipo hila nyingi ila lile alilolikukusudia Bwana juu ya Maisha yako litasimama.

"Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua." Yohana 1:10

Mungu akiwa na wewe huchelewi waache wakuseme, waache wakusimange wewe endelea mbele. Mungu akikuhifadhia jambo haliozi. 

Wachawi huwa wanaiona kesho yako hawana shida na sura yako hawana muda na wigi lako, wanapambana na kesho yako. Wewe unatakiwa kusema yale yaliyopangwa kwa ajili yangu yako pale pale, wale wanaotakiwa kukusaidia wakikataa kukusaidia waache mungu atakusaidia kwa njia nyingine. Wewe safari yako ilishaamriwa na mungu hakuna wa kukuzuia. Mabonde, mashimo na makorongo, yote hayo hayazuii safari yako ya kuendelea mbele. AMEN

Post a Comment

0 Comments