google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UMUHIMU WA MAOMBI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
MKESHA WA VIJANA 30.08.2024
ASKOFU BARAKA TEGGE
SOMO.UMUHIMU WA MAOMBI

Mtu aliyefanikiwa yako mambo anayafanya kwa namna fulani, watu wengi tunaona matokeo na kuna baadhi ya watu wanajua ni kipi wamefanya, wachache zaidi wanajua ni kipi amefanya na matokeo yake ni nini, kuna matokeo ya mtu aliyeomba na asiyeomba.

Matokeo ya mtu ni namna anavyowaza. Mawazo mazuri au mabaya ni zao la rohoni, Roho Mtakatifu anakuletea mawazo ili kufanya jambo fulani.

Watu wengi wanapuuzia mambo ya kiroho kwa sababu ya kuamini mambo ya mwilini kama vile elimu.

Yakobo alikuwa Tajiri kwa sababu Mungu aliingilia kati kwa kumpa mawazo na Mungu akambariki.

“Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.” Daniel 9:12

Inabidi tufanye jambo kwa mfululizo au kwa desturi , mara nyingi zaidi hata kama hauoni matokeo ila inatubidi tufanye kama desturi na baadae inaleta matokeo mazuri.

Mungu analeta mawazo lakini pale tu unapoomba bila kukoma, unapoomba kuna akili Mungu anakupa, hauwezi kushindwa ikiwa kama unaomba.

Reading books can give you intelligence but by prayers give wisdom. Mtu anaweza akawa intelligence lakini hana wisdom.

Kwenye kila eneo Mungu ametaka kukuweka ni lazima akupe akili na ili uipate ni lazima kuomba,

Kama kuna jambo Mungu amekupa ni lazima akupe akili ila ni kwa kuomba.

“Mungu akikuitia jambo anakujaza akili moyoni. Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.” Danieli 10.11

Tukianza kuomba kuna maneno ambayo Mungu anaongea na mtu. Maombi yana uhusiano na akili za ki Mungu.

"BONYEZA HAPA KUANGALIA MKESHA MZIMA WA VIJANA"

Post a Comment

0 Comments