google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LAANA YA KICHAWI


UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 06.10.2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: LAANA YA KICHAWI 

Laana ni maneno ya kinyume anayotamkiwa na mtu mwenye mamlaka. Ulimwengu inaongozwa na neno na ulimwemgu upo kwasababu ya neno.

 Matukio kwenye maisha  ayaongozwi na elimu bali inaongozwa na neno ambaye ni roho. Maneno hayo ya laana mtu anatamkiwa ili ashidwe kwenda sehemu fulani. wachawi nao wanafanya kazi zao ili aweze kumloga mtu ili asiweze kupata kile anacho kitaka.

Wachawi wapo kila sehemu na wao wanataka kuharibu lile kusudi la Mungu ambalo mtu analo kama vile biashara, kazi, elimu, kusafiri na nyingine nyingi. inakupasa upigane vita ili kuweza kuharibu kila laana za kichawi.

“Usimwache mwanamke mchawi kuishi.” kutoka22:18

Mtu yoyote anaweza kulogwa atakama ana elimu ndio maana watu wengi sasa wakubali mambo mabaya kama vile ndoa ya jinsia moja na mengine mengi ya uovu kwasababu wamelogwa. Elimu zetu aziwezi kutusaidia pasipo kuongozwa na Mungu maana pasipo Mungu akunakitu kinacho wezekana.

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” wafilipi 4:13

Laana inaweza kubadilisha maisha ya mtu kutoka yale ambayo Mungu amekusudia kufanya na kuwa na maisha mabaya. Laana pia inakuondoa kwenye Maisha ya baraka kama ili vyokuwa kuwa nyoka baada ya kuwadanganya Adamu na Hawa na Mungu akamlaani yule nyoka.

“BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mwanzo 3:14-15 

Kuishi maisha mabaya yanatokana na kuwa na kitu sio cha kwako na kuwa kama mtumwa. kuna wakati mtu aliye okoka Mungu anarusu mambo mabaya yampate ili aweze kuwa imara na kukuongozwa ili kwenda kwenye kumiliki usiwe na haraka inakuhitaji uwe mvumilivu ili kuweza kupata kile Mungu alicho kuitia. Kuna wakati mtu kwenye maisha anapitia wakati mgumu. anayapitia ili uweze kwenda kwenye wokovu.

Mtu aliokoka kuna mambo magumu au ya dhiki anapitia ili kuweza kupima na Imani kwa Mungu. laana ya kichawi ni laana inayo kuzuia usiende kule Mungu alipokukusudia. Maombi yanakufanya upigane vita ili uweze kuwaangamiza watoa laana na kuharibu kila laana. Laana inaletwa pale wanapojua kuwa mtu ana nguvu. ulimwengu waroho ni unaona kila kitu kwenye ulimwengu wa mwili.

“Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa” Hesabu22:6

Mtu anayekujua kwa namna ya rohoni ndiye ayekujua. ndio maana wachawi wanaona mtu alivyo kwa namna ya rohoni na kutoa laana ili kuzuia lile kusudi la Mungu alilo itiwa. na laana huwa inaelezwa sehemu fulani. Inakubidi upigane vita ili kuweza kuzuia laana hiyo.

“Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu;Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu,Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.” Hesabu 24:17

Maneno huvunjwa kwa maneno, neno linaweza kutengua maneno. Maneno yanaweza kubatilisha mashauri ya giza au ya kichawi kuna mambo hayaitaji elimu bali yanahitaji mkono wa Mungu. wachawi watoa laana ili kuzua kile kitu ambacho Mungu amekikusudia.pale Mungu anapokulinda anabatilisha laana kuwa baraka

“Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.” Hesabu 23:11

Maneno yanavunja laana na kuiendeleza ile baraka ambayo Mungu amekuitia.

“Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!” Hesabu 23:23. AMEN

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments