google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KARAMA YA MUNGU HAINA MAJUTO - SEHEMU YA NNE

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 15.09.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KARAMA YA MUNGU HAINA MAJUTO - SEHEMU YA NNE

Mungu akikuitia jambo hawezi kubadilisha. Habadilishi kwa sababu ya maneno au watu kukuchukia, Mungu akikupa amekupa. Kila mtu anakusudi lake ambalo Mungu amempa ili afanye kazi hapa duniani. Kila mtu kuna karama ambayo Mungu amempa iweze kumsogeza kwenda sehemu fulani ili atimize kusudi aliloitiwa. 

Kabla ya kuzaliwa ulikuwepo na kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu ulikuwapo. Kila mtu alikuwa kwa Mungu naye amemtuma kwa ajili ya kazi fulani na kila kilicho toka ndani ya Mungu sikuzote lazima kitashinda. Neno la Mungu ndilo litiao uzima.

“BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo yake ya kale. Nalitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla haijawako dunia” Mithali 8:22 

Wewe unaweza kusahau kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako lakini pamoja na hilo haimaanishi huna kusudi la Mungu. Mungu anakukumbusha kusudi lako kwa kupitia neno la Mungu alilomuekea mtumishi wake. Neno la Mungu ni maneno ya uzima, pale unapoanza kuelewa neno la Mungu unaanza kuelewa asili yako ya mbinguni maana Mungu anakuwa anongea wewe ili ufanye kusudi lako. 

Kuna watu wa aina mbili, kuna watu wenye nia ya ki Mungu na kuna wenye nia ya kishetani. Wewe ni wa Mbinguni na umetumwa kwa kazi maalumu ambapo baada ya kufanya kazi hio utarudi utarudi ulipotoka yaani Mbinguni.

Pale tunapofanya kusudi la Mungu tunapata faida na baraka. Wewe na mimi tupo hapa duniani hadi kazi tulizopewa kufanya zitakapoisha.

“Alipozithibitisha mbingu nalikuwako; Alipopiga duara katika uso wa bahari; Alipofanya imara mawingu yaliyo juu; Chemchemi za bahari zilipopata nguvu Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi; Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku Nikifurahi daima mbele zake;” Mithali 8:27

Kuna mambo mengine yamefichwa machoni pako ili kufanya kile Mungu alichouagiza kwa kupitia mtumishi wake kwa kuhubiri neno la Mungu. na pale tunapo sikia na kuelewa neno na kuwa na hisia ya kitu hicho hujue Mungu anasema na wewe unatakiwa uchukue na kufanyia kazi ili uweze kupata matunda kwenye Maisha.

Wewe unaweza kuwa adui ambaye hapendi ufike pale Mungu alipo kusudia, anaweza kuwa rafiki yako au mtu karibu. Unatakiwa uombe mara kwa mara ili umshinde adui huyo.” MIMI NA WEWE TULIKUWEPO KABLA YA KUUMBWA KWA MISINGI YA ULIMWENGU” AMEN.

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments