UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
SEMINA YA MAHUSIANO ALHAMISI 13.09.2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA 3
Mungu hawezi kumlazimisha mtu aishi
maisha fulani, unachagua mwenyewe. Maisha ya mtu ni machaguo aliyoyafanya jana,
juzi na siku zilizopita.
“Angalia, nimekuwekea leo mbele
yako uzima na mema, na mauti na mabaya;” Kumbukumbu la Torati 30:15
Mungu hata akitaka usiharibike ni
maamuzi yako ndio yatakayoamua hatima yako. Mungu alimuonya Kaini kuwa dhambi
iko inamuotea mlangoni lakini Kaini akaamua kuifuata hio dhambi.
“BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini
una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata
kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe,
walakini yapasa uishinde.” Mwanzo 4:6-7
Matokeo ya maisha ya mtu
hayatokei papo kwa papo, inaweza kuchukua muda mrefu sana hadi kuja kudhihirika.
Kitu kibaya ni kuwa unaweza kusahau hata wewe mwenyewe mbegu ya matokeo
unayoyaona uliipanda lini. Umri wa ujana ni umri ambao umeficha mbegu
zinazopandwa, ambazo matokeo yake utayaona baadae sana. Matokeo hutaweza
kuyaficha hata ukijaribu namna gani.
3. Usifanye Urafiki
na Mtu ambaye Hana Dhamira kama ya Kwako.
Chagua rafiki ambaye ana amini
kile unachokiamini. Marafiki ni wa muhimu na epuka urafiki na mtu anayeona sex
kabla ya ndoa ni kawaida. Tabia nyingi za watu zinaanza na marafiki, marafiki
wanaweza kukujenga au kukuharibu. Kama kuna mtu atakuathiri maisha yako kwa
ukaribu sana ni rafiki.
“Usifanye urafiki na mtu mwenye
hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia
zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.” Mithali 22:24-25
Kwenye mazungumzo ya marafiki
kumejaa nguvu ya kukushawishi kufanya mambo ambayo hata wewe hukuwaza kufanya
na baada ya muda utakuwa kama rafiki yako.
“Msidanganyike; Mazungumzo mabaya
huharibu tabia njema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi;
kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.” 1 Wakorintho
15:33-34
Biblia ya kiingereza inasema;
“Don’t be fooled by those who say
such things, for “bad company corrupts good character.” Think carefully
about what is right, and stop sinning. For to your shame I say that some of you
don’t know God at all.” 1 Corinthians 15:33-34
Bad company inayozungumzwa hapa ni watu ambao
ni wa karibu kwako kama marafiki. Watu wengi wanaharibika kutokana na kushindwa
kuachilia na kukaa mbali na marafiki wabaya kwa sababu tu mlisoma pamoja au mna
historia kwenye jambo fulani. Hutaweza kukaa na mtu muhuni alafu ukategemea akujenge
kwenye mema..
“Maneno mabaya yasitoke vinywani
mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji
yao, ili yawafae wale wasikiao.” Waefeso 4:29
Marafiki wanaweza kugeuza mtazamo
wako ukaona mambo mabaya kuwa ni mambo mazuri.
“Aibaye mali ya babaye au mamaye,
na kusema, Si kosa Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.” Mithali 28:24
- Mambo
anayoongea
- Mambo
anayoyawaza (anayotafakari)
- Mambo
anayoyatenda
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.” Yoshua 1:8
Mambo mabaya nayoongea na
marafiki yakikuingia kinachofuata unaendea njia ya uharibifu.
- Marafiki wa duniani (hajaokoka) ambao wanaziendea njia za dhambi.
- Marafiki wa kanisani wenye tabia za kidunia. Sio kila mtu wa kanisani inabidi pia awe rafiki yako.
Kuna watu ambao Paulo anawataja
sio wa kuchangamana nao.
“Sisemi msichangamane kabisa na
wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye
kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini, mambo
yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni
mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au
mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.” 1 wakorintho 5:10-11
Mfano wa mtu aliyefuata ushawishi
wa rafiki yake mbaya kwenye Biblia ni Amnoni, Amnoni alishauriwa vibaya na
rafiki yake kulala na ndugu yake Tamari.
“Ikawa baada ya hayo, Absalomu,
mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni,
mwana wa Daudi, akampenda. Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya
umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni
vigumu kumtendea neno lo lote. Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake
Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu
sana. Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme, unakonda hivi siku
kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia, Nampenda Tamari, umbu la ndugu
yangu, Absalomu. Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na
babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje,
nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile
mkononi mwake.” 2 Samweli 13:1-5
Ili uwe salama
usifanye sex kabla ya ndoa epuka kwa nguvu zote marafiki wasio na nia moja kama
wewe kwenye masuala ya sex.
0 Comments