google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA 4

SEMINA YA MAHUSIANO
SOMO: MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIFANYE SEX KABLA YA NDOA 4
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE

Watu waliozaliwa na Mungu hawatendi dhambi ila anajilinda dhidi ya yule muovu. maneno yanazalisha hisia, watu wanaweka maneno utani bila kujua yanaweza kuanzisha hisia za kimapenzi.

“Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” 1 Yohana 3:9

4. Jiweke chini ya mamlaka na mtu ambaye unaogopa kama akijua unakosa

Kwenye haya maisha kama hakuna mtu unaye mwogopa inasababisha kuleta hasara kwenye maisha yako. Kama una Mungu bila kuwa na mtu unaye mwogopa hauwezi kumwogopa Mungu. Mungu anamwekea mtu mamlaka ili uweze kumwogopa na  kwa kufanya hivyo utamwogopa Mungu pia.

“Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake. kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.” Warumi 13:1-7

Kuna wakati unafika sasa unakuwa na uhuru ambao unaweza kufanya chochote bila kulazimishwa. unatakiwa uamue kujiweka chini ya mamlaka kwa mtu ili aweze kuwa mbadala wa Mungu na anaweza kuwa mzazi wa kiroho. Mtu anapopewa uhuru wa kupitiliza bila mtu wa kumwogopa inaweza mtu kushindwa kufika sehemu fulani au kwenye mafanikio yake

“Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?” Waibrania 12:9

 Ni jukumu lako ukae chini ya mtu au mamlaka. Pale unapo jiweka chini ya mamlaka inakusaidia uweze kuwa na maisha imara. uta mwogopa Mungu pale una pokubali kuwa chini ya mamlaka kwa mtu.

“Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?” Mwanzo 39:9 

Unapokuwa chini ya mamlaka inakusaidia kushinda kila vishawishi vya watu wabaya. Kuwa chini ya mamlaka inaambatana na utii, kwa kuvunja mapenzi yako na kufuata mapenzi ya mtu mwingine. Kwa kuwa chini ya mamlaka inatusaidia kupata njia kuishinda changamoto. Ni lazima uwe na mtu ujiweke chini ya mamlaka na hususani kwa mtu aliye kuzidi umri kwasababu kuna mambo mtu huyo ameyapitia ili aweze kuwa njia ya safari unayoiendea.

Mungu anaweza kukulinda kwa kumuweka mtu ambaye unaweza kumtii au kuwa chini ya mamlaka ili uweze kwenda njia ipasayo kuiendea. Thamani ya mtu anayeongozwa ni kubwa kuliko mtu asiyeongozwa.

“Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa” Mwanzo 21:10

Pale unapo kataa kuwa chini ya mamlaka inaweza kukusababishia wakati utakapo fika utahitaji msaada lakini kwasababu ya kushindwa kuwa chini ya mamlaka inakusababisha usifike pale unapo takiwa kufika

“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa. Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.” Mathayo 23:37-39

Unapokuwa chini ya mamlaka unatakiwa kupokea maarifa kwa mtumishi wa Mungu ili uweze kuwa imara. Ni rahisi mtu kupotea kwasababu ya kutokuwa chini ya mamlaka.

“nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu. Yeremia 3:15

Kwenye maisha kunawakati una hitaji mtu wa kukuongoza ili uweze kwenda kwenye njia yako. Mtu anavyojiweka chini ya mamlaka yule anyemwongoza anaweza akamwangalia na kujua nanma anvyo weza kujitambua. kunawakati unaweza ukajiona kuwa wewe ni thamani kuliko wengine na kujiona hakuna haja ya kuongozwa au kuwa chini ya mamlaka. ndio pale mtu anapoanguka na kushindwa kuwa imara, ni salama uwe na mtu unaye mwogopa ilikuweza kuwa imara. 

Tuogope kuwa na uhuru wakupitiliza na tukubali kuwa chini ya mamlaka ilituweze kuwa imara kwasababu uhuru unaharibu watu. “ILI TUWE IMARA TUNATAKIWA KUKUBALI KUWA CHINI YA MAMLAKA” AMEN

"BONYEZA HAPA KUANGALIA SEMINA YA MAHUSIANO"

Post a Comment

0 Comments