google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UMEPEWA UWEZO WA KUANZA NA KUMALIZA


UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 22.09.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: UMEPEWA UWEZO WA KUANZA NA KUMALIZA

kila mtu anafahamu kuwa biblia ni neno la Mungu. kwa kupitia neno la Mungu ni Mungu anaongea na sisi kwa kupitia watumishi wake tangu zamani ila hadi sasa Mungu anaongea na watu kila siku kila saa na pia anawatumia watu ili Mungu aweze kuongea na wewe wakiongozwa na Roho mtakatifu. 

“Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”2 Petro 1:21

Hakuna kitu kisichowezekana kama usipokuwa na hofu. Maana mtu mwenye hofu hawezi kuwa na Imani.

“Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Marko 11:23-24

Lipo jambo ambalo kila mtu Mungu amemuwekea ili aweze kufanya hapa duniani na baada ya kuifanya atarudi alipotoka. Unatakiwa kuomba ili kuweza kuharibu mipango ya shetani katika ulimwengu wa roho ili uweze kutimiza hatima yako. Kila jambo ambalo Mungu aliokuwekea lipo ndani yako. Chanzo cha kitu kinatokana na mtu mmoja. Kwa kuingia kwa dhambi chanzo ni kwa mtu chanzo ni mtu mmoja na wokovu uliingia kwa kupitia mtu mmoja ambaye ni Yesu. 

“Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe” 1wakoritho7:10

Kuna mambo ukifanya Mungu anafanya kwa kupita wewe Mungu anakuwekea shauku ya kutaka kufanya jambo hilo.

“Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. Mwanzo15:24

Chochote kilichowekwa na Mungu ndani yako hauwezi kufa hadi litimie kusudi la Mungu kwenye Maisha yako. Mungu anamtumia mtu ili aweze kukupeleka kwenye kusudi lako. Mungu anajiunganisha na watu na pia shetani anajiungamanisha na watu na watu hao mmoja ametumwa na Mungu ili aweze kukupeleka kwenye hatima yako na mwingine ametumwa na shetani ili aweze kuizuia kusudi la Mungu kwenye Maisha yako.

Kwa kupitia watumishi wake wakiongozwa na Roho mtakatifu ndio pale Mungu anaongea na mtu ili aweze kufanya kile Mungu alicho kuongoza kwenye maisha yako na mtu hawezi kufa hadi pale kusudi la Mungu litimie kwa maana umepewa uwezo wa kuanza na kumaliza. kila mtu amewekewa ushindi wake kabla haijaanza kutokea. Uumbaji umeumbwa na Mungu kufanikiwa asili ya kufanikiwa imekewa ndani ya mtu kwasababu jambo lako lishaamuliwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu. Mungu anaweza kutumia kinywa cha mtu pale mtu anaongea ndio Mungu anaongea.

“Ndipo mfalme Ahasuero aliponena, akamwambia malkia Esta, Ni nani huyu, tena yuko wapi, ambaye moyoni mwake alithubutu kufanya hivi? 6Esta akasema, Ni mtesi, tena ni adui, ndiye huyu Hamani, mtu mbaya kabisa. Mara Hamani akaingiwa na hofu mbele ya mfalme na malkia. Esta 5:16

Mtu yoyote atakaye jaribu kuizuia kusudi la Mungu lazima ataangamia. Watu hao huwa wanaweka mipango au mitego ili kuzuia kile kitu alicho kipanga Mungu. kile Mungu alichokuifaidhia Mungu hakiozi na hakuna mtu wa kuizuia.

“Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba” Danieli 6:13

Kila mitego alioweka yule adui juu yako wataingia wenyewe na kuangamia na kila mtego walio weka juu yako Mungu atakuepusha na kila mtego. Mtu wa Mungu hawezi kuangamia lakini wao watangamia. Uwezo wa kuanza na kumaliza umepewa na hakuna mtu wa kuizua. Na hakuna mtu wakuzia hatima yako.

“Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu. Danieli 6:24

Kama kuna jambo ukiwa na amani ya kukifanya usitake kupata ushauri wa mtu, kwa maana mtu atakushauri sawasawa na hatima yake. “UMEPEWA UWEZO WA KUANZA NA KUMALIZA NA HAKUNA MTU WA KUZUIA” AMEN

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments