google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VITA YA IMANI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 24.11.2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: VITA YA IMANI


Mungu akitaka akupe huwa akupatii kitu ila anakupatia neno, Mungu akitaka jambo litokee anaongea kwanza neno kwa sababu anataka usikie na kuamini kwa maana Imani chanzo chake ni kusikia na kuamini. Imani ndio inaleta kitu kwasababu pale unapo amini ndio inamfanya mtu kupokea kitu chake kutoka kwa Mungu.

BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha; geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati. Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao. Kumbukumbu ya torati 1:6-8

Pale unapo sikia neno na kuliamini unakuwa unauhakika wa kupokea kitu. Pale unapo amini neno inakusaidia kupata kitu kutoka kwa Mungu, kuna wakati unaona kuwa haito wezekana ila pale unapo amini inakusaidia kupata kitu chako ambacho Mungu ametamka neno juu yako anaweza akamtumia mtu ili neno hilo kwa habari ya maisha yako likufikie.

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Waebrania11:1

Mungu anapo tamka neno inakubidi kulisikia kutamka na kuliamini kwa maana Imani inamsaidia mtu kupokea na kupata kile Mungu alicho kikusudia juu yako, lakini pale usipo amini inakufanya kushidwa kupokea kile Mungu alicho kukusudia juu yako, pale Mungu anapo tamka neno juu mtu inabidi mtu huyo amini ili kuweza kulipata kile Mungu alicho kukusudia juu yako.

Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu marko11:23

Kuna mambo huwezi kufanikiwa bila kuongozwa na Mungu na wala sio bidii, bidii haiwezi kukusaidia kama hauto ongozwa na Mungu. Pale unapoongozwa na Mungu hauwezi ukaanguka pale unapo mtanguliza inakusaidia wewe kwenda katika njia sahihi na jambo hilo Mungu anatamka neno inakubidi neno hilo hulisikie na kuamini

Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama. Zaburi 32:8

Kuna watu wana Imani na kuna watu wenye dalili ya Imani hii nisawa na mtu anaye umwa malaria anang’atwa mbu mwanamke lakini unaweza ukawa na dalili ya maralia lakini sio malaria.mtu amegawanyika katika vipande viwili kuna mtu wa ndani na mtu wanje na Mungu anaongea na mtu wa ndani na shetani anasema na mtu wa nje inakubidi usikie kwa mtu wa ndani ambaye ni roho ambaye ni wewe.

Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Mathayo 17:20

Pale unapo sikia sauti ya mtu wa nje inaweza ikawa watu wakakukatisha tamaa kwa kufanya hivyo itakufanya kuwa kushidwa kuyatimiza yale Mungu aliyoya kusudia juu yako, inakubidi ushindane nao kwasababu hao kazi yao kukuzuia/kufanya vita kwenye Imani yako, kuna mambo mtu anayafanya kwa kupenda hayo ndio hicho Mungu amekuwekea juu yako.

Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Mithali 1:10

Pale Imani yako inapokuwa imara inakusaidia kuyafikia pale Mungu alipokukusudia, ila pale Imani yako inapo tetereka inakufanya kushidwa kufikia kule Mungu alipo kukusudia, inakubidi usiangalie nyuma wala usiwe na shaka na Imani yako kwa maana pale unapogeuka nyuma utazama na Imani yako itatetereka.

Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mathayo 14:28-30

Inakubidi ufanye vita na maadui wanao fanya vita na Imani yako ili wewe uweze kuwa imara, pale unapo tamkiwa neno la unabii inakubidi ushindane nao wanao pigana vita vya Imani yako ili uweze kuamini na kuyaamini maneno ya Mungu pale una pata kitu chako usitafute ushauri kwa watu wengi kwa kuwa Mungu ndiye anayejua kesho yako

Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri; uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani 1timotheo 1:18-19

"TUKIAMINI NENO LA MUNGU INATUFANYA KUWA IMARA NA KUYATIMIZA MAPENZI YA MUNGU"AMEN

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"


Post a Comment

0 Comments