UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 12.01.2025
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
UTAMBULISHO WAKO 2
Ukijua wewe ni nani ina nguvu kuliko kuomba, namna utambulisho wako ni unanguvu sana kuliko mbele ya maadui zako, kwenye ulimwengu waroho wachawi na mashetani wanajua kuwa wewe ni nani. Wapo watu wanaona sio kwamba wanaomba ila wame shushwa kutoka mbinguni kwa ajili ya kuwa macho ya Mungu hapa duniani.
“Naye
Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa
nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na
katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaifanyiza tena madhabahu ya
BWANA, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa BWANA.” 2Mambo ya nyakati15:8
Wana
wa Mungu wapo wa aina tofauti tofauti wa kwanza ni yule aliye mkiri yesu kuwa
bwana na mwokozi wa Maisha yako yaani kuzaliwa mara ya pili, mtu mwingine ni
malaika ambaye yeye pia ni mwana wa Mungu. mtu akitoka ndani ya mwili anakuwa
malaika na ukiwa malaika hakuna kuoa wala kuolewa wote ni walewale kwa maana
ganda la nje ambaye ni mwili huwa vinahitaji mambo hayo ambayo ni kuoa au kuolewa
mtu wa ndani huwa hana mambo mengi kwa
maana wote wana fanana.
“Kwa maana watakapofufuka katika
wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.” Marko 12:25
Mwana
wa Mungu ni wewe ni mtu wa ndani upo ndani ya mwili kwa ajili ya kufanya kazi
ya Mungu aliyo kuagiza, kuna mambo huta ya omba kwasababu ni stahiki yako
ambaye ni mwana wa Mungu ambayo ni lazima apate kutoka kwa Baba wa mbinguni ambaye
ni Mungu wetu. kanuni ya baba na mwana akimwomba mkate je mtoto atapewa jiwe
hapana ila atapewa mkate
“Au
kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au
akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa
watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa
mema wao wamwombao?” Mathayo 7:9-11
Ukitembea
kwenye utambulisho wa Mungu kuna mambo huna lazima wa kuomba ila ni lazima
upate kile unacho stahiki kwasababu ni mwana wa Mungu, ukitembea kwenye
utambulisho huwa unakuwa wewe na Baba wote mnafanana kwa sababu ukionekana wewe
ameonekana Mungu. ukitembea kwenye utambulisho wako shetani hauwezi kukandamizwa.
Wewe ni mrithi wa Mungu ili uweze kuwa mrithi wake ni lazima ujitambue,kwasababu
ukiwa mtoto hauwezi kuwa mriithi hadi utakapo kuwa,kuwa mtoto ina maanisha kuto
jitambua asili yako kuto kuwa na maarifa ya Mungu.
“Kisha
wana wa Yusufu wakanena na Yoshua, wakasema, Kwa nini umenipa mimi kura moja tu
na fungu moja kuwa ni urithi wangu, kwa kuwa mimi ni taifa kubwa la watu, kwa
sababu BWANA amenibarikia hata hivi sasa?” Yoshua 17:14
Ukitembea
kwenye utambulisho wako kile unacho kihitaji utakipata na hakuna kuonewa na
wana wa ibilisi na hawezi kuku karibia.pale mtu anapokufa kuna tengana mwili na
mtu ambaye ni roho. Watu wengi wanateswa na shetani kwasababu ya kutoitambua
utambulisho wako kuwa wewe ni mwana wa Mungu
“Watu
wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi
nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya
Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.” Hosea4:6
Kwenye Agano la kale mtu aliye pakwa mafuta anaitwa mpakwa mafuta.ila kwenye agano jipya mpakwa mafuta ni kujazwa roho mtakatifu.Neno la Mungu nizaidi ya mafuta ya upako,wala mchanga wala maji ya upako kwa maana neno ni Zaidi ya vitu vyote.
“Vyote
vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote
kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa
nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.” Yohana 3:5
kwasababu Ndoto ni kiashiria cha utakuwa nani
badae, ila na mkakati unatakiwa kuwan nayo ili kuweza kuielekea kwenye ubadae, mwana
wa Mungu anangalia watu wote kuwa sawa kuwa wote kuwa wana wa Mungu na hakuna
kitu cha kuwa tofautisha anaweza akawa dhehebu lolote au dini ya kislam kwa
wote wanawito ambao wamepewaa.
“Naye
Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya
sanduku la agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za
amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.”1Wafalme 3:15
Uchumi
wa nchi ukiimarika watu wote wa nchi uchumi wao utaimarika na kazi ya Mungu ita
songa mbele.mcha Mungu yoyote ni lazima Moyo wake kuelekea juu ya nchi,kurhani tukufu ni maandiko matakatifu ila yametamkwa
kiarabu ila ni yale kwenye biblia mfano Yohana ni yahya. Bbaba na Mama ni wazazi
wa mwili wako, Mungu ni mzazi wa roho yako.
“Kumcha
BWANA ni tumaini imara;Watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha BWANA ni
chemchemi ya uzima,Ili kuepukana na tanzi za mauti” Mithali 14:26-27
Wewe
ni mtu hatari kwenye ulimwengu wa Roho kwa sababu pale unapo mkiri Yesu kuwa
bwana na mwokozi wa Maisha yetu kuna
mambo umeyafanya ni kama yafuatayo
I. i Kusulubiwa pamoja na Yesu
Pale
unapo mkiri yesu kwenye ulimwenu wa roho unakuwa umesulbiwa pamoja na Bwana
Yesu.
I. ii. Kufa pamoja na Yesu
Pale
unapomkiri Yesu kwenye ulimwengu wa Roho una kuwa umekufa pamoja na yesu.
II. iii. Kuzikwa pamoja na Yesu
Pale
unapo mkiri Yesu unakuwa unazikwa pamoja Yesu kwenye ulimwengu wa Roho.
I. ivKufufuka pamoja na Yesu
Pale
unapomkiri yesu kuwa bwana na mwokozi wa Maisha Yetu kwenye ulimwengu wa Roho
una fufuka pamoja na Yesu.
II. v Unaketi kwenye mkono wa kuume wa Mungu Baba
Pale
unapo mkiri Yesu kuwa bwana na Mwokozi wa Maisha Yetu unaketi pamoja na Mungu
kwenye ulimwengu wa roho.
III. vi Kila alipo Mungu wewe upo
Kwenye
ulimwengu wa roho kila alipo Mungu upo pamoja naye
0 Comments