UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 05.01.2025
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
UTAMBULISHO WAKO
Mungu hamchagui mtu kwa sababu ya wema ila anachagua mtu ili kutimiza kusudi lake la kuchagua. watu wa rohoni wanajua mambo mengi sana kuliko wewe. pamoja na watu kuomba kwa bidii ila kuna jambo moja watu wengi hawaifahamu ambalo jambo hilo ni utambulisho ya kuwa wewe ni nani.
“Basi akatuma mtu, naye akamleta
kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la
kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Ndipo
Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho
ya BWANA ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka,
akaenda zake Rama.”1samweli16:12-13.
Kuna namna Mungu anatakiwa kujua utambulisho wako na
kuna namna shetani na vibwengo vyake vinatakiwa kujua kuwa wewe ni
nani,wachawii wanajua kuwa wewe ni nani na anajua utambulisho wako.
“Ndipo
Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi,
nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko
mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. ”1samweli28:7
Watu
wa mambo ya rohoni wanajua kuhusu mtu,kuna wakati mtu anapitia mambo magumu na
kuona kuna mambo yanayokatiosha tamaa ila yote huwa Mungu anakuandaa kwasababu
maandalizi ya Mtu yanachukua muda mrefu ili kukufanya kuwa imara na kumfanya alitimize
kusudi la Mungu, Yesu aliandaliwa kwa miaka 30 ila muda aliyo ifanyakazi ni miaka
mitatu tu na akaondoka kwenda mbinguni.
Masomo
ni ya muhimu na tena ya faida ila hai kuhakikishii ukuu, ukuu una kuja kwa mtu
kwasababu umesha pangiwa na Mungu. Mwanadamu anayebalisha maneno akiuwa sehemu Fulani
anakuwa hanamsimamo huyo mtu hafai kuwa kiongozi.
“Basi
walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na
elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja
na Yesu.” Matendo 4:13
Mtu
dhaifu akizungukwa na watu wenye nguvu huyo mtu ni mwenye nguvu,mtu mwenye
nguvu akizungukwa na watu dhaifu huyo atakuwa dhaifu ,mtu mwenye nguvu
akizungukwa na watu wenye nguvu wenzake anakuwa jabali au mtu imara.nguvu ya
asiye na akili hujipendekeza na mtu mwenye akili anajitegemea kama mkiwa watu
wenye nguvu mnaweza mkafanya tafa na kutokutikisika.
“Tangu
siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao
wenye nguvu wauteka.” Mathayo 11:12
Kwenye ulimwengu kunamambo kuwa
yana nguvu yapo matano:
I. i Nguvu
ya Mungu
II. ii Nguvu ya Pesa
III. iii Nguvu yaElimu
IV. ivUmaarufu
V. vMamlaka
Mungu
huingia ndani ya mtu ili aweze kulifanya kusudi lake kwasababu Mungu hana
mwili.
“WEWE NI MZAO MTEULE, WEWE NI
KUHANI WA KIFALME ,TAIFA TAKATIFU,WEWE UNAMILIKIWAA NA MUNGU,UME NUNULIWA KWA
DAMU YA YESU,WEWE UNAMILIKI NCHI.”
0 Comments