UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 12.02.2025
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
KULISIMAMISHA KUSUDI LA MUNGU
“Najua
ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.”Ayubu
42:2
Jambo alilo likusudia Mungu lipo milele, unapokuwa unasuburia kuna wakati unachoka ila wewe sio wa kwanza. unapaswa kuwa mvumilivu kwa maana hata ingechukua mda mrefu kwa maana kusudi la Bwana litatimia juu yako.
“Mna
hila nyingi moyoni mwa mtu;Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.Haja ya
mwanadamu ni hisani yake;Ni afadhali maskini kuliko mwongo. Kumcha BWANA
huelekea uhai;Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.” Mithali 19:21-22
Wewe kuna mambo unataka kuyapata lakini mambo hayo yapo kinyume na kusudi la Mungu. kila kilicho kuwa kinyume na makusudi ya Mungu juu yako haiwezi ikatimia.
kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.” Mathayo 26:39
Unae
oa au kuolewa naye ameunganishwa na kusudi la Mungu, Kumsikiliza mtu wa Mungu lina maana sana ni muhimu kuisikiliza. ni afadhali kuchelewa kufika
kuliko kuwahi ukaishia njiani na kupata ajali. Inakubidi kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya
kuitimiza kusudi la Mungu na usiwe na maamuzi ya harakaharaka.
“Maana
ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu
gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya
kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,” Luka 14: 28-29
Unaweza
ukawa umeokoka ila kuna wakati maamuzi yanaweza yakakufanya ukaharibu mwishoni. ukawa umeanza vizuri ukaja kuharibu mwishoni ina kupasa kuvumilia kwamaana ahadi
ya Mungu juu yako lazima itimie.
“Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho” Yakobo 5:7
Kusudi la Mungu limeungamanishwa na mtu unayekaanaye, Mungu akitaka kukuinua anakuunganisha na watu ambao watakupeleka kwenye kusudi la Mungu kwa maana binadamu hawezi kusimama peke yake. Ukitaka uwende kwenye kusudi lako na kilifikia inakupaswa kuambatana na wenzako,Mungu hana mwili akitaka akatakufanya kusudi lake ni lazima ajiunga manishe na binadamu. Familia ikiharibika taifa inaharibika kwasababu taifa chanzo chake ni familia.
“Kwa
hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja.” Mwanzo 2:24
Mungu hawapi sifa wenye sifa ila humpa sifa aliye mchaguae na amtakae, chunguza moyo wako mwenyewe maana Mungu anajua kila mtu hatakama watu wanakuona kuwa ni mwema ila Mungu anakujua wewe ulivyo. Miongoni mwa watu kuna watu wabaya lakini mwisho wa watu hao una fanana. Anayeogopa vita hawezi kwenda juu.
“Bali
ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya
Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie
katika nuru yake ya ajabu;” 1Petro 2:9
0 Comments