UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 09.02.2025
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO:
KUTAKA KWA MAOMBI
![]() |
Mungu huwa ana mambo amekusudia juu ya mtu, ambapo huweka kutaka mambo hayo ndani ya mtu huyo. Pale mtu anapo omba, ili Mungu aweze kumjibu ni lazima awe ndani ya mtu huyo naye anamwekea shauku ya kutaka. Shauku ni jambo la rohoni ambapo Mungu anaingia ndani ya mtu ili kulitimiza kusudi lake.
“Kwa maana ndiye Mungu atendaye
kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake
jema.” Wafilipi 2: 13
Mungu kuna wakati anamtumia mtu kuja kwako ambaye yeye ana maelekezo kutoka kwa Mungu kuhusiana na njia yako. Mtu huyo huwekewa shauku ya kukusaidia. Inakubidi kumkubali mtu huyo na usimdharau maana Mungu anasema na wewe kupitia mtu huyo. Kila jambo la Mungu lina wakati wake.
“Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu,
ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na
majivu.” Danieli 9: 3
Kila shauku ya Mungu inahitaji akili ya Mungu. Akili
ndiyo dira inayo kuonesha unaenda wapi. Mfano ulikuwa unashauku ya biashara ina
kubidi uwe na akili ya Mungu ya kukuongoza kwenye biashara yako. Akili ni kujua cha
kufanya, namna ya kufanya na wakati wa kufanya.
“Naam, nilipokuwa nikinena katika
kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa
upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Akaniagiza, akaongea nami,
akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.” Danieli 9: 21-22
Shauku ni jambo jingine na akili ni jambo jingine. Kuwa
na shauku ni ya muhimu na akili ya Mungu ni ya muhimu, inakubidi uwenavyo vyote. Baada
ya kuwa na shauku, inakupasa uombe ili uweze kupokea akili ya Mungu ya kutimiza
shauku uliyowekewa. Chochote kilicho anzishwa na Mungu kinamhitaji Mungu kukitimiza maana yeye ni Alfa na Omega yani mwanzo na mwisho.
“Mwanzo wa maombi yako ilitolewa
amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari
habari hii, na kuyafahamu maono haya. Muda wa majuma sabini umeamriwa juu
ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza
dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na
kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.” Danieli 9: 23-24
Mambo yote ambayo unashauku nayo ni lazima uyatake kwa Maombi. Usipoomba hautapata na utaishia kuonea wivu wengine. Wivu hutokea pale mtu amekosa lile jambo alilolitaka, na kuchukia kwasababu
jirani yake analo. Mtu mwenye wivu ni sawa na mchawi
asiyekuwa na vifaa. Mtu mwenye wivu anapo shindana na mtu wa Mungu ni lazima mtu wa Mungu atashinda. Kama ilivyokuwa kwa Yusuph, ndugu zake walimwonea wivu na kutaka kumuua ila walishindwa kumuua. Hakuna mtu wa kuondoa shauku ambayo Mungu
ameweka ndani ya mtu kwamaana kila kilicho zaliwa na Mungu hushinda ulimwengu.
“Iweni hodari na moyo wa ushujaa,
msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda
pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.” Kumbukumbu la torati 31: 6
Laana ya mtu
mwenye mamlaka ina nguvu. Laana ni maneno yanayo mfanya mtu asifike sehemu fulani. Pale unapofanya jambo la kumuumiza mtu mwingine bila hatia unajitengenezea laana.
“Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema,Na alaaniwe Kanaani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake..” Mwanzo9: 22-26
0 Comments