google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWISHO WAKO ULISHAAMRIWA

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 23.02.2025
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MWISHO WAKO ULISHAAMRIWA

Mwisho wako ulishaamriwa na Mungu tayari, yeyote anayejaribu kukuzuia basi atauharakisha kuelekea kwenye utukufu.

“Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.” Zaburi 139:16

Utimilifu wa lolote jema maishani mwako basi hilo si lako ni Mungu amefanya kupitia maishani mwako.

"Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi." zaburi 121: 2

Unaomba kwa sababu kuna matukio lazima yatokee kukupigisha hatua kwenye kule ulikoamriwa kuwa, wewe ni mkuu sana na ukuu wako hauanzi leo ulishaaamriwa tangu siku  uliyozaliwa.

"Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu."wafilipi 4:6

Mungu ana kitabu chake ambacho limeandikwa jina lako, kila ulicho nacho Mungu amekupa ili kukusaidia kufika mahali ambapo unatakiwa kufika.

Wewe una mwanzo wako na wewe una mwisho wako, yale unayopambana nayo tayari yalishaandikwa, kwenye ulimwengu wa roho kuna jina lako wewe, mwisho wako ulishaamriwa huwezi kutengeneza bidii nyingine ingawa bidii ni ya muhimu. Wewe ulivyo hivi na sura yako  na jina lako, kule mbinguni kuna jina lako, ulishaandikiwa utazaliwa wapi, na atakayekusaidia mpaka ufike unakotakiwa kufika.

“Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. 'Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.” Luka 24:44-45

Mungu akitaka kukutumia hakuoneshi mahali utakapopita kwa sababu akikuonesha utakataa kwenda, kama kwa Yusufu alikuja kuwa waziri mkuu lakini hakujua hapo katikati angepitia kuwa utumwa, anapelekwa gerezani.

"Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao akamwambia Yusufu,Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake."Mwanzo 41: 40-42

Yako mambo yanayokuhusu wewe saa ikifika kila kitu kinakaa kwenye mstari ili tu uwe unayetakiwa kuwa, Mungu akitaka upite mahali si wewe unayepita, ni yeye anapita kupitia ubinadamu wako, kuna wakati mwisho unaweza kuchelewa, unajiuliza nina bidii lakini mbona sifanikiwi, kuna sehemu Mungu anataka upite, liko tukio linatokea litakutembeza kwa shida huku unalia huku umenuna lakini wewe tembea unaelekea kwenye kusudi ulilopangiwa.

"Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu."2 wakoritho 3:5

Mungu huwa anaficha kitu ndani ya mtu, usimuone mtu hana kazi ukafikiri hana kitu, ukuu hauko mbinguni ukuu uko nao, uko ndani na ukuu ule utaanza kudhihirika vipande vipande, unaweza kuwa na mtu ukamfukuza kazini kwa sababu unahisi ni mzembe halafu wakati wake wa kuinuliwa ukifika utashangaa, halafu mara nyingi huwa hawafananii, unapopata mtikisiko haimaanishi Mungu ameiahirisha ndoto yako , ndoto yako iko pale pale.

"Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. "1samweli2:8

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA YA JUMAPILI"


Post a Comment

0 Comments