google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUGEUZWA NA KUWA MTU MWINGINE

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 16.03.2025
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: KUGEUZWA NA KUWA MTU MWINGINE

Maisha hapa duniani ukiyasubiri yakuendee vizuri ndiyo upate furaha nikuvinje moyo hauwezi kupata furaha. kuna watu wanafuraha lakini mambo yao bado ni magumu ila siri yao kubwa ya furaha hiyo ni kuwa na Bwana.

“Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa BWANA.” Zaburi 122: 1

Mtu ni roho na huwezi kumpatia vya mwilini akawa sawa na mtoshelevu. Dunia imejaa watu wenye vitu lakini hawana amani na raha. Ukitafuta mambo ya dunia hii kwa nia ya kukupatia raha utapotea. njia sahihi ni kumfuata yeye maana hata tukiwa na makosa yeye anatupenda na yeye kwake kuna furaha.

“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.” Mathayo 11:28-30

Mtu ni roho na mtu awezi kupata ya mwilini na akaridhika kwa maana yeye sio mwili ila ni roho iliyo ndani ya mwili. kuna watu wanaela na bilionea na hawana raha na watu hao wanamisongo ya mawazo na kuwa kuwafanya kutopata raha liko pumziko ambalo mali haitoi  naye ni yesu.

“Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka,Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile;Ubovu ukaingia mifupani mwangu,Nikatetemeka katika mahali pangu;Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki,Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu. Maana mtini hautachanua maua,Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda;Taabu ya mzeituni itakuwa bure,Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi,Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe;”Habakuki 3:16-17

Kila mtu ambaye yupo kwenye uso wa dunia kuna jambo la ki Mungu ambayo ni sababu yeye yakuwepo duniani. Mungu kwa hekima yake hutengeneza matukio ambayo yanamtengeneza mtu kufika kule alipoitiwa. Kuna mtu aliakuwa na maisha ya kawaida mpaka pale anapokutana na mtu  ambaye Mungu amemchagua.

“na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.”Waefeso 1:11

Sauli alienda kwa ajili ya kutafuta punda tu lakini huko ndipo alipogeuza na kuwa mtu mwingine. Mungu hutengeneza matukio hata yale usiyokusudia  kuyapata ili ya kufikishe kwenye hatima yako. Mungu anatengeneza tukio umfikie mtu fulani anaweza kuwa hata usiyempenda ili akufanye kuwa mtu mpya.

“Hata Samweli alipomwona Sauli, BWANA akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu. Ndipo Sauli akamkaribia Samweli langoni, akasema, Tafadhali, uniambie, nyumba ya mwonaji iko wapi? Samweli akamjibu Sauli, akasema, Mimi ndimi mwonaji; tangulia mbele yangu ukwee mpaka mahali pa juu, kwa maana mtakula pamoja nami leo; kisha, asubuhi nitakuacha uende zako, nami nitakuambia yote uliyo nayo moyoni mwako. Na wale punda zako waliopotea siku hizi tatu, usijiudhi kwa ajili yao; maana wameonekana. Na yote yaliyotamanika katika Israeli amewekewa nani? Si wewe, na nyumba yote ya baba yako?”1samweli 9:17-20

Watu wa Mungu wote kwenye walio zungumziwa kwenye Biblia, walianza kama watu wa kawaida mpaka pale walipokutana na mtu fulani na tukio Fulani kumfuata. kumfuata mtu wa Mungu ni mafunuo binafsi  kwasababu unavyo mwona wewe ni tofauti unavyomwona mwingine. Kuna mtu anaweza kufanya chochote kwa ajili yako.

“Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.” Yohana 3:28-30

kuna mambo unamhitaji yesu kwa kupitia Roho mtakatifu. sio kila ushauri ni wa kusikiliza kutoka kwa watu kwa maana unaweza ukasikiliza ili uweze kutambua ni lazima uongozwe na roho mtakatifu naye atazungumza ndani ya mtu kufanya  kusudi la Mungu  ni lazima kulifanaya atakama watu watakutenga ila unapaswa kulifanya kusudi la Mungu bali njia sahihi ni Yesu pekee kwa maana ukiwa na Yesu umepata vyote.

“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Matendo 1:8

Ukiwa mnyenyekevu ni muhimu na inakupasa kuwa chini ya mamlaka. Ukiwa unapenda mtu wa Mungu na kumsikiliza nawe utageuzwa na kuwa mtu mwingine mafanikio ya mtu kwenye Maisha hayana uhusiano na elimu,familia, kabila  ukoo ndugu ila chanzo chake ni ulimwengu wa roho, roho wa bwana na atakapo kujilia kwa nguvu na kugeuzwa na kuwa mtu mwingine.

“Roho ya BWANA ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.” Waamuzi 14:16

Kuna watu unawaona hawastahihili lakini roho wa bwana akimjilia kwa nguvu kwasababu Roho wa Bwana ni Mungu mwenyewe ganda la nje aliitaji mabadiliko ila mtu wa ndani akiingiwa ndani ya Mtu naye anaweza kufanya mambo Zaidi ya watu wenye elimu kuna mambo Mungu anarusu ili kukutengeza nakukufanya kuwa imara

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Wafilipi 4:13

Mungu amechagua kufanya kazi ndani ya mtu unatakiwa kuwa mtiifu na mnyenyekevu hatakama haupendi style yake inakubidi kuifuata style ya mtu wa Mungu. Maisha yetu na hatima yetu ipo ndani ya mtu hata Mungu alivyo kuwa mtu aliwa kuwa na mtu alio ibeba hatima ndani yako na sio mtu unaye mtakawewe bali mtu aliyeletwa na Mungu.

“Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.” Mathayo 10:41

Mungu ameweka machaguzi mbele yako yaani uzima na mauti kubali kuongozwa na mtumishi wa Mungu ni uzima na kumkataa ni mauti na kukusababishia roho chafu kuingia ndani yako pale unapo omba unaiondoa roho chafu na roho wa Mungu anakuingia kwa nguvu.

“Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.”1 samweli 16: 23

Post a Comment

0 Comments