UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 11.01.2026
ASKOFU DKT JOSEPHAT
GWAJIMA
SOMO: HATIMA YAKO IMESHAMULIWA NA
MUNGU
1. SHAULI LA MUNGU LITASIMAMA
“Mna hila nyingi moyoni mwa mtu;
Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.” Mithali 19:21
Hila ni uwerevu wa uongo, kwenye
biblia inatonesha ndani ya mtu kuna ujanjaujanja lakini pamoja na hayo yote
kusudi la Mungu ndio litasimama.
“Shauri la BWANA lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.” Zaburi 33:11
Pamoja na hila zote alizonazo mtu
ndani ya moyo wake ila Mungu ndio shauri lake ndio litakalo simama. Sehemu uliozaliwa
haiamui mwisho wako utakuwa vipi bali shauri la Mungu litasimama kwasababu yeye
amekutoa Mbinguni na kukuleta duniani ambapo kazi yako ni kufanya lile kusudi
lake ambalo yeye amekutuma. Mungu anakushushia maahali popote ilo haiamui
hatima yako bali yeye ndiye anaye ifahamu.
Mungu anamleta mtu Duniani kutoka
mbinguni akiwa roho na kuingia ndani ya mwili ambao baba na mama wameutengeza
na mtu huyo anashushwa na Mungu kutoka mbinguni na kuingia ndani ya mwili ili
uweze kulifanya kusudi la Mungu. Sheria ya dunia ili uweze kufanya jambo lolote
ukiwa kwenye dunia ni lazima uwe na mwili.
“Kwa sababu mwili hutamani
ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana,
hata hamwezi kufanya mnayotaka.” Wagalatia 5:17
Wewe ulikuwepo kabla ya kuumbwa
kwa misingi ya ulimwengu. Nikukumbushe Yesu alikuwepo kabla ya kuzaliwa ambapo alikuwa
anaitwa Mungu neno. Ambapo alishuka kutoka Mbinguni na kuingia ndani ya mwili
na kuzaliwa duniani kwa ajili ya kusudi la kuokoa ulimwengu na dhambi zao.
“Alikuwako ulimwenguni, hata kwa
yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake,
wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika
watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu,
wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.” Yohana
1:10-11
Mwaume kwenye ulimwengu wa mwili
ni mtu ambaye anajinsia ya kiume na yeye anambegu naye anakutana na mwanamke na
wanatengeneza mwili naye Mungu anamleta mtu na kuingia ndani ya mwili ambao
umetengenezwa na mwanaume na mwanamke.
Kuna watu unawaona leo ni watu
waovu ila kuna wakati unafika Mungu anawarudisha kwake naye anawafanya sawasawa
na kusudi lake alilowaitia Mungu ndio maana ukielewa maana yake hauto wachukia
watu kulingana na tabia zao.
Kuna watu wamezaliwa katika
mazingira magumu ila pamoja na hayo yote wamefanikiwa sio kwa uweza wao ila
ilikuwa ni mpango wa Mungu. Hata kama mtu amezaliwa kwa wazazi walevi ila
haiondoi mpango wa Mungu naye Mungu anajua ni namna gani anaweza kumtoa mtu
pale alipo.
“Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.” Yeremia 1:4-8
Hakuna mtu wa kukuondoa duniani
kama haujamaliza kusudi la Mungu ambalo amekuitia inakubidi usiogope kwa maana
kama ukifa alafu kusudi la Mungu halijatimia maana yake Mungu amefeli na kwa
asili ya Mungu hajawahi kufeli, kwahiyo huwezi kufa hadi kusudi lake Mungu
litimie alilokuitia.
Mwili una exiperdate ambapo mtu muda
wake wa kukaa duniani umeisha na Kwenda Mbinguni Kwenda kutoa hesabu alioifanya
kile alicho mtuma. Watu ambao Mungu anawatumia amewatengeza. Kuna changamoto
unapitia unakuta watu wanakupinga ila pamoja na hayo yote Mungu anakuruhusu
upitie ili akutengeneze kwa ajili ya kusudi lake Mungu.
“Ee Mungu, laiti ungewafisha
waovu!Enyi watu wa damu, ondokeni kwangu; Kwa maana wakuasi kwa ubaya,Adui
zako wakutaja jina lako bure.” Zaburi 139:19-20
Mwanzo wako uliokuwa duniani
unatengenezwa Mbinguni. Mungu angalii mtu wa nje bali anamwangalia mtu wa ndani
ambaye amemchagua kwa ajili ya jambo alilomtuma. Daudi alichaguliwa na Mungu
sio kwa sababu ya mwili wake bali yeye wa ndani ambaye Mungu alichagua kwa
ajili ya kulifanya kusudi lake la kuwa Mfalime kabla ya kuumbwa kwa misingi ya
ulimwengu.
“Mwana wa haramu asiingie katika
mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa
BWANA.” Kumbukumbu 23:2
Kuna mambo mtu anapanga mipango
unafikiri anayepanga ni wewe ila ni Mungu ndie anayepanga akiwa ndani yake.
Kuna viumbe wa kichawi ambapo muda wako ukifika kwaajili ya kufanya lile kusudi la Mungu kazi yao ni kukuficha usiweze kufanya lilekusudi kwa wakati sahihi ambalo Mungu aliamua ufanye inabidii uwaondoe kwenye ulimwengu wa kwenye njia yako na kufanya kusudi la Mungu.


0 Comments