UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 18.01.2026
ASKOFU DKT JOSEPHAT
GWAJIMA
SOMO: KUSUDI LA MUNGU LITASIMAMA
2.KUSUDI LAKO NA UPINZANI WA
KICHAWI
![]() |
Mungu anapokuchagua kwaajili ya kusudi lake, kuna wakati maadui ni wengi wanaotaka kukuzuia. Ila hilo lisikukatishe tamaa kwa maana Mungu anaruhusu upite katika njia hiyo, ili aweze kukutengeneza kwaajili ya kuliendea lile kusudi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Mungu akitaka kumwinua mtu, hutumia mtu.
Mungu alipotaka kumwinua Daudi, alimtumia
Goliati ili aweze kulifanya lile ambalo wengine walishindwa. Yapo mambo yanayomtokea
mtu mwilini ambayo chanzo chake ni rohoni. Mambo haya humpata mtu ili kumpinga asitimize
kusudi lake, ingawa kusudi la Mungu juu ya mtu huyo ndilo litasimama.
Mashetani wanauwezo wakujua hatima yako. Wanauwezo kuona kesho yako, na kazi yao wanashindana na wewe ili usiende kwenye kesho yako ambayo Mungu ameikusudia. Kuna kitu kikubwa kimewekwa na Mungu ndani yako, na mashetani wanajua. Hivyo hufanya kazi ya kukutengenezea matukio ya kukuzuia ama kukukatisha tamaa ili usitimize wito wako. Kwenye ulimwengu wa roho hakuna bahati mbaya, kila tukio linalompata mtu linakuwa limetengezwa kukuzuia.
“Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu
mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu
wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama,
wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. Basi, njoo wewe,
nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda
nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana
najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa. Wazee
wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi
mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki. Akawaambia,
Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama BWANA atakavyoniambia; wakuu
wa Moabu wakakaa na Balaamu.” Hesabu 22:5-8
Unapotumwa na Mungu, unageuka
kutoka kuwa binadamu wa kawaida, badala yake anakuwa ni Mungu anaishi ndani
yako kupitia wewe. Hivyo, chochote
unachokuwa unafanya inakuwa sio wewe bali Mungu anafanya kupitia wewe. Unakuwa
ni mtu kabisa wa kawaida ila ndani yako, ni Mungu ndio anaeishi na kufanya
mambo kupitia wewe. Ukitembea ni Mungu anatembea! Ukibariki ni Mungu anabariki!
Yaani kila unalolifanya anakuwa ni Mungu anafanya kupitia wewe ili kusudi lake
litimie.
“Wakamwuliza, Ni nini basi? U
Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. Basi
wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi
yako? Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya
Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.” Yohana 1:21-23
Kuna wito ndani yako ambao hukusukuma
kupenda kufanya mambo fulani, ambayo ndio yanakupeleka kwenye lile kusudi la Mungu.
Ingawa huwezi kuona kwa wakati huo, ila ndo Mungu anakuwa anakupeleka kwenye
kusudi lako.
Unapoona maadaui wanakushambulia,
ni kwasababu ya ule wito ambao una nguvu ya Mungu ndani yake. Na hiyo nguvu
ndio inakushikilia ili uweze kuendelea mbele, hivyo hawawezi kukushinda
inakubidi usiogope maana una nguvu ya kuwashinda.
“BWANA akamwambia, Mataifa mawili
yako tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.
Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.” Mwanzo
25:23
Kwanini wakati mwingine kwenye
maisha unapitia wakati mgumu sana? Ni kwasababu wachawi, mashetani na wasoma nyota
wanakuwa wameona kesho yako, na kile Mungu alichoweka ndani yako. Hivyo wanashindana
na wewe ili usifikie kesho yako iliyoamriwa na Mungu. Mungu anapokuchagua haangalii
sifa ulizonazo, hangalii elimu ulionayo, haangalii umaskini ulionao, badala
yake humpa mtu sifa sawasawa na kusudi lake.
“Maana amwambia Musa, Nitamrehemu
yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si
katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule
arehemuye, yaani, Mungu.” Warumi 9:15-16
Hivyo, wachawi na mashetani wakiona
kile kilicho ndani yako, wanakutumia magonjwa ndani ya mwili wako ili ukate
tamaa. Wachawi hawalogi kwa kuangalia sura ama muonekano wako, wanapambana na
kile ulichokibeba ndani yako. Kile ambacho Mungu ameweka ndani yako. Kuna wanawake
matumbo yao yameandaliwa kuleta watu wa Mungu, hivyo mashetani hufunga matumbo
yao wasizae kwa urahisi. Maana wakizaa wanakuwa wametimiza lile kusudi la Mungu
la kuleta watumishi wa Mungu duniani.
“Naye alikuwa na wake wawili;
jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo
Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. Na mtu huyo
alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea
BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na
Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.”1Samweli 1:2-3
BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA YA JUMAPILI

.jpeg)
0 Comments