UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 04.01.2026
ASKOFU DKT GESHOM
MWAKILA
SOMO: NDOTO NA MAISHA YA MTU

Mungu anaongea namtu kwa njia
mbambali anaweza akaongea kwa njia neno lake lakini anaweza akaongea kwa njia
ya Mawazo au kwanjia ya ndoto. Ndoto ni vile mtu anavyo tamani kuwa. Kuna ndoto
nyingine unazipata ukiwa umelala hayo yote Mungu anakuwa anaongea na wewe.

Kuna mtu anatakiwa awe wa aina fulani
ila hawezi kuwa kwasababu ya kupuuzia ndoto ambayo Mungu amemuonesha. Kwenye biblia
ndoto imeonekana kwa watu mbalimbali ikiwa ambapo Mungu alikuwa anaongena watu
kwa njia ya Ndoto ili watu waweze kutii
maagizo ya Mungu anayowaambia kwenye ndoto.
“Lakini Mungu akamjia Abimeleki
katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu
uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.” Mwanzo 20:3
Ndoto haziangalii mazingira, Mungu
anaweza kuongea na mtu mahala popote bila kujali mazingira uliopo. Kwenye
Biblia yakobo anaoneshwa na Mungu kwa njia ya Ndoto akiwa anaonesha na Mungu
kuwa atalindwa popote atakapo kuwepo. mwota ndoto anauwezo wa kubadili majina kutoka
kuwa la kawaida hadi kuwa kuwa lenye ukuu.
“Akafika mahali fulani akakaa
huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali
pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota
ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika
mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.” Mwanzo
28:10-12
Makusudi ya Mungu hayabadili yanaweza
yakabidilika vitu lakini huwezi kubadili makusudi ya Mungu. Mwota ndoto anaweza
kubadili jina lake kutokea la kawaida hadi kuwa la ukuu. mwota ndoto huwa
atapeliwi kirahisirahisi. Mtu akibadilisha jina mara moja Mungu anasajili Jina
hilo mbinguni.inakubidi ulinde kinywa chako kwa kile unacho kizungumza. Huko ulikiota
ndoto unatakiwa kunatendo ulifanye kwa ajili ya ukumbusho.
“Yakobo akaondoka asubuhi na
mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha
kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale
Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.” Mwanzo 28:18-19
Ndoto ya tatu inahusiana na ya pili
kwasababu ndoto ya mtu ni uhalisia usipoo tii ndoto unayoiota kuna mambo
unayakosa ambayo Mungu amekuagiza ufanye kwa ajili ya kusudi lake. uapoota
ndoto unatakiwa ufanye maamuzi ya haraka ya kufanya ili uweze kulitumikia
kusudi la Mungu kwa wakati sahihi.
Mtu yeyeote anayetaka kumtesa
muota ndoto lazima Mungu ataingilia kati na kushughulika na yule anayemtesa na
kumlinda mwota ndoto ili kuyafanya yale alioyomwambia mtu ili yatokee. Kuna watu
ni adui wa Ndoto ambapo kazi yao ni kuzuia usifanye sawasawa na ulivyo kuagiza
Mungu. Mwenye ndoto huwa hawindi kwesababu Mungu huwa anashughulika na watu
wanao wawinda watu wa Mungu.
Mungu huwa anaongea na Baba na
baba anaongea na Watoto, Watoto huwa hawana Mungu ila Watoto wanakuwa wana
Mungu wa baba yao. baba anaweza akawa wa kimwili au wa kiroho ila inatubidi
kufuata maagizo ya wazazi wetu wa kiroho maana baba anapoongea na wewe hujue
Mungu anaongea na wewe kupitia baba.
Kwa kutuoa sadaka inakufanya
umiliki hiyo ndoto. Ndoto ndio inayo amualila mtu maisha yake yatakuaje baadae.
mashambulizi mengi huwa yanashambuliwa ndotoni. Unawweza ukawa unaota unashambuliwa
au unalishwa mavyakula kuna mambo unakuta yanazuiliwa. Inabidi kuyazuia
mashambulizi kwa kuomba.

0 Comments