UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 01.02.2026
ASKOFU DKT GERSHOM
MWAKILA
SOMO: BARAKA ZA KORESHI
Isaya 45:1–2
“Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono
wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake; nami nitalegeza viuno vya
wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda
mbele yako na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande
milango ya shaba na kukata-kata mapingo ya chuma.”
Koreshi
ni mfano wa mtu anayemtumikia Mungu kwa uaminifu. Kumtumikia Mungu ni
kuwatumikia watu kwa upendo, haki na uadilifu. Hivyo, Koreshi ni yule
anayewasaidia wengine kutoka katika utumwa wa aina mbalimbali na kuwaweka huru,
huku akitimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yake.
Kufanya
mapenzi ya Mungu ni kuishi na kutenda kulingana na kusudi aliloliweka Mungu
ndani ya kila mtu. Maandiko yanaonyesha kuwa Mfalme Koreshi aliwaacha huru wana
wa Israeli kutoka utumwani. Hii inatufundisha kuwa kila mwanadamu ana kusudi
maalum alilopewa na Mungu, ambalo anapaswa kulitimiza. Mfano mkuu ni Mungu
alivaa mwili katika Yesu Kristo ili kutimiza kusudi la ukombozi wa wanadamu.
Zipo
baraka zinazomfuata mtu anapoamua kwa dhati kumtumikia Mungu. Baraka hizo ni
pamoja na uponyaji, heshima, kuongezewa siku za kuishi, na kufanikiwa katika
kazi na mipango ya maisha.
Ezra
1:1–3
“Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno
la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha
roho yake Koreshi… akasema, BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za
dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu…”
Maandiko
haya yanaonyesha kuwa Mungu alimwamsha Koreshi kutekeleza kusudi lake. Vivyo
hivyo, Mungu humwamsha kila mtu anayejitoa kumtumikia ili awe chombo cha
kutimiza mapenzi yake duniani.
Baraka
za Koreshi
Zifuatazo ni baraka alizopata Koreshi, ambazo pia humpata mtu yeyote anayechagua kumtumikia Mungu kwa uaminifu:
- Kushikwa
mkono wa kuume na Bwana
Mungu hulinda, huokoa na huongoza kutoka hatari, dhiki, aibu, tabu na mauti, hadi mahali salama. - Kutiishwa
kwa mataifa mbele yako
Mungu huondoa hofu na kukupa heshima mbele za watu. - Kulegezwa
kwa viuno vya wafalme ili milango ifunguke
Mungu huondoa vikwazo na kufungua milango ya ushindi katika maisha yako. - Bwana
kukutangulia mbele yako na kunyoosha njia zako
Hutengeneza njia hata pale ambapo haikuwepo, katika kazi, ndoa, elimu na maeneo mengine ya maisha. - Kuvunjwa
kwa milango ya shaba na mapingo ya chuma
Mungu huondoa vikwazo vigumu vinavyokuzuia kufikia kusudi lako. - Kupata
hazina za gizani
Mungu hukupatia baraka zilizofichwa na mafanikio ya kudumu.
Kwa
hiyo, mtu anapoamua kumtumikia Mungu kwa moyo wote, Mungu huondoa vifungo
mbalimbali katika maisha yake na kumwezesha kutimiza kusudi lake.


0 Comments