UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI – 15.03.2026
ASKOFU DKT. JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MSAADA UTOKAO JUU
![]() |
Biblia inasema: “Wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo,
wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.”
(Kumbukumbu la Torati 18:11).
Mauti haiji tu bila sababu, bali huletwa na mwenye nguvu ya
mauti ambaye ni shetani. Shetani hutumia watu wake, yaani wachawi, ambao
wanaweza kusababisha mtu kuwa na hofu ya mauti au hata kifo chenyewe.
Neno la Mungu linasema: “awaache huru wale ambao
maisha yao yote, kwa hofu ya mauti, walikuwa katika hali ya utumwa.”
(Waebrania 2:15).
Wachawi wanaweza kutengeneza viumbe wa kichawi ambavyo mtu
anaweza kuviona kama vitu vya kawaida, ilhali vimetengenezwa kwa nguvu za
kichawi. Pia wanaweza kusababisha matatizo mbalimbali kama magonjwa, ajali,
mauti, mikosi, au kukataliwa katika maisha.
Wakati mwingine huunda viumbe wa kichawi kama wanyama au
hata watu kwa madhumuni yao ya kichawi.
Mara nyingi wachawi hutengeneza matatizo juu ya mtu, na mtu
huyo huona kana kwamba ni matatizo ya kawaida, bila kujua kwamba nyuma yake
kuna nguvu za kichawi zinatenda kazi. Wakati mwingine matatizo hayo yanaweza
kusababisha kifo, na baada ya hapo mtu huyo kudaiwa kufanywa mtumwa wa kiroho
au msukule kwa ajili ya kuwahudumia wachawi.
Mchawi ni nani?
Mchawi ni mtu anayehusishwa na nguvu za giza, na hutumika na
shetani kwa lengo la kuwatesa au kuwadhuru watu. Sifa kubwa ya wachawi wanaweza
kutambua nyota ya mtu na kujua hatima au mafanikio yake ya baadaye. Katika
Biblia pia kuna simulizi kuhusu mamajusi waliotambua nyota ya kuzaliwa kwa
Yesu. Sifa nyingine ya wachawi wanaweza kuingilia nyota ya mtu na kuitumia kwa
manufaa ya watu wengine.
Wengine huamini kuwa mafanikio ya maisha ya mtu yanahusishwa
na nyota yake. Hivyo kuna watu ambao hawajasoma sana lakini wamefanikiwa
maishani, na wengine husema kwamba mafanikio hayo yanahusishwa na nyota yao, si
tu elimu waliyonayo.
Katika biblia kuna mfano unaoonyesha jinsi mtu
anaweza kufungwa au kuzuiwa na nguvu za kiroho kwa muda mrefu. Wachawi wanaweza
kuweka kile kinachoitwa mipaka au “fensi” za kichawi, ambazo humzuia mtu
kufikia maeneo au hatua fulani katika maisha yake. Mara nyingi mtu akitafuta
suluhisho, huenda kwa mganga wa kienyeji bila kujua waganga nao ni wachawi.
Njia mojawapo inayofundishwa katika imani ya Kikristo ya
kupambana na nguvu za giza ni kwa kumwomba Mungu na kutaja jina la Yesu. Kulitaja
jina la Yesu kuna nguvu ya kuvunja mamlaka ya nguvu za giza.
Chanzo kikuu cha matatizo mengi ya kiroho hutokana na
dhambi. Shetani hupata nafasi ya kumtesa mtu pale anapokuwa katika hali ya
dhambi.
Njia za kujikinga na nguvu hizo ni pamoja na:
i. Kuondoa dhambi ya asili
Dhambi ya asili ilianza tangu wakati wa Adamu na Hawa. Ili mtu ajikinge dhidi
ya nguvu za shetani, anatakiwa kutubu dhambi zake na kumwomba Mungu msamaha.
ii. Kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako
Mtu anapomkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake,hupata faida
mbalimbali za kiroho, zikiwemo:
a. a. Jina lake kufutwa katika kitabu cha hukumu na
kuandikwa katika kitabu cha uzima wa milele.
b. b. Mungu kuwa Baba yake (Mwana wa Mungu).
c. c. Wachawi hawatakuroga tena.
d. d. Utapata ulinzi wa Mungu


0 Comments