UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 01.03.2026
ASKOFU DKT
JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MASHIMO YA KICHAWI
![]() |
Mashimo ya
kichawi ni ya rohoni, yaani hayawezi kuonekana kwa macho ya kawaida lakini yapo
na ni halisi.
Shetani
huwa haumbi chochote ila anaiba vitu vya Mungu nakuvitumia kwa uharibifu. Watu
huwa na vipaji mbalimbali ambavyo Mungu huwapa ili wamtumikie, lakini Shetani anaweza
kumchukua huyo mtu nakutumia vipaji vyake kwa uharibifu. Hivyo watu hao ni watu
ambao wameibiwa na wanatumia vipaji vyao kwa kazi ya Shetani.
“Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa;
wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo,
wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.” Isaya 42:22
Kuna
matatizo mtu anayapitia kwenye maisha yake, ila ni kwa sababu vitu vyake vina
milikiwa na shetani. Kuna mtu anapata magonjwa ya moyo kumbe wachawi wanautumia
moyo wake kwa ajili ya kazi zao. Kuna mtu mtu ni tasa ila kumbe wachawi
wanatumia tumbo lake la uzazi kwaajili ya kuzalisha katika ulimwengu wa kichawi.
“Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara
mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu, Ili kurudisha roho yake itoke
shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.” Ayubu 33:29-30
Ili
uweze kufanya vita na wachawi ni lazima upigane ukiwa rohoni. Unapoomba unakuwa
upo katika ulimwengu wa roho, nawe unakuwa unapigana vita na wachawi hao na
kuwaokoa watu watu waliotekwa.
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya
majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12
Kuongezeka
au kupungua inategemea na watu unaoambatana nao. Ukiwa unawatu wenye tabia ya uovu,
basi baada ya muda utakuwa muovu. Lakini kama umejizungushia watu wenye tabia
njema na wana nguvu na wewe utakuwa na tabia njema. Ukiwa mwenye nguvu ukajizungushia
wenye nguvu nawe utakuwa Jabali. Ukiwa mwenye nguvu ukajizungushia wenye
udhaifu nawe utakuwa dhaifu.
NAFSI
ILIYOIBIWA.
Mtu
anaweza kuibiwa nafsi, na nafsi yake ikawekwa kwenye mashimo. Ndani ya nafsi ya
mtu kuna mambo manne yanayounda nafsi ya mtu. Mambo hayo ni:
a) i. Nia
b) ii. Utashi
c) iii. Hisia
d)iv.
Kumbukumbu
Wachawi
wanaona kilichopo ndani ya nafsi ya mtu, nao wanakiiba na kukitumia kwaajili ya
kazi zao. Kuna mtu ndani yake amewekewa utashi na Mungu, wachawi wanaiba ule utashi
wa mtu huyo na kutumia kwa ajili ya kazi zao za kichawi. Kuna mtu anatumia
utashi wako kichawi na anafanikiwa.
Nafsi ya mtu inaweza kuchukuliwa kichawi, alafu wachawi wakatumia nafsi ya mtu huyo kumfanikisha mtu mwingine.


0 Comments