google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATUKIO YA KICHAWI NA MASHETANI KATIKA UZAO WA WANADAMU

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA PASAKA 19.04.2026
ASKOFU DKT GERSHOM MWAKILA
SOMO: MATUKIO YA KICHAWI NA MASHETANI KATIKA UZAO WA WANADAMU

Mtu huwaza kuwa Shetani ndiye anamletea matatizo na shida katika maisha yake, lakini hamuoni shetani isipokuwa anaona sura za watu anaowafahamu. Baba yetu alitufundisha kuwa matukio ya kichawi yanatokea kwa mkono wa Malaika; Malaika hawa ni mashetani wasababishao matukio ya kichawi. Mashetani hawa walishushwa baada ya kushindwa vita Mbinguni. Vita hii ilikuwa kati ya Mikaeli na Malaika zake dhidi ya Joka na Malaika zake

“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufunuo 12:7-9

Joka pia huitwa ibilisi au shetani audanganyae ulimwengu wote. Shetani ni Malaika wasioilinda enzi yao (Yuda 1:6); ni Malaika waliokosa wakatupwa na wamewekewa mipaka (2 Petro 2:4). Malaika hawa hufahamika pia kama Ibilisi na Malaika zake (Mathayo 25:41).

Wapo Malaika wa Mungu na Malaika wa Shetani. Malaika wa Shetani ni Malaika wa giza ambao ni mawakala wa matatizo kwa wanadamu. Kila tukio alipatalo mtu, limesababishwa na malaika; kama ni tukio zuri, limesababishwa na Malaika wa nuru, na kama ni tukio baya, limesababishwa na Malaika wa giza.

Wakati mwingine Shetani hujifanya kama Malaika wa nuru ili afanikishe kusudi lake. Shetani anautaalamu wa kujigeuza awe kama malaika wa Nuru. Kuna watu wengi wameharibikiwa kwasababu ya shetani kuwapotosha kwa matendo na njia zionekanazo machoni kama njia za nuru lakini mwishoni watu hao wanaharibikiwa. Mfano, tukio hufuata mtu, naye akadhani ni jambo jema kwake liletalo nuru lakini mwisho wa jambo hilo ni mbaya. Shetani ni mwenye hila anayejua namna ya kutumia hila zake.

 “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”2 Wakorintho 11:14-15,

 na pia katika kitabu cha m Mithali 16:25, Ayubu 2:1, na  Waefeso 6:11

Malaika wote wanatabia zinazofanana; -

i.             Malaika wanaweza wakatokea ghafla na kupotea ghafla.

Malaika wa Mungu wanauwezo wa kuonekana na kupotea hapo hapo hata kama kuna ulinzi mkali, mfano, kuna mageti, mbwa, masai; ulinzi wa namna hii hauwazui. Mashetani huingia bila kizuizi chochote na kuleta uharibifu kwa mtu.

Yupo atulindaye, naye tunamhitaji wakati wote - Zaburi 121.

ii.           Malaika wanaweza kuvaa umbo lolote.

Malaika wanaweza kuwa mti, wadudu, mtu, kitu, au chochote sawasawa na uhitaji wa siku hiyo.

iii.         Malaika hawatendi kazi mpaka wawe wametumwa.

Malaika ni roho watumikao ambao wanasubiri kuagizwa na kwenda kule waagizwapo; hii ni kwa Malaika wa Bwana na mashetani. Mtu mwenye kuurithi wokovu anayo mamlaka ya kuwatuma Malaika. Wachawi pia huwatuma mashetani.

Mfano1; Malaika wa Bwana walitumwa kwa Yusufu kuhusu mkewe Mariamu kuwa atachukua mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.” Mathayo 1:18-20

Mfano2: Daniel alitokewa na Malaika Gabrieli katika ndoto (Daniel 9:20-27).

Malaika wa Mungu wanatumwa na Mungu na watumishi wake, vivyo hivyo, Malaika wa giza wanatumwa na Shetani na watumishi wake

“Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” Waebrania 1:13-14.

Yupo Mungu atutiaye nguvu tuwapo katika dhiki; Yesu alitiwa na nguvu alipokuwa kwenye dhiki. Mungu hutuma Malaika zake.

Mungu huketi katika sifa. Wana wa Mungu humsifu Mungu kwa nyimbo za sifa ili ashuke kuwahudumia. Shetani naye hutukuzwa na watumishi wake katika kazi zao na mashetani hupanda ili kutoa huduma ya kishetani. Ukimuona mganga wa kienyeji, mchawi, mpiga mafundo na wengine wa aina hiyo, ujue hao wanafanya kazi ya shetani.

Wana wa Mungu hutumia Neno la Mungu pekee lenye nguvu kumuhudumia kila mtu sawasawa na shida yake. Mara tu litamkwapo Neno, Malaika Mbinguni hushuka kuwahudumia wana wa Mungu

 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” Waebrania 4:12

Uzao wa wanadamu na uzao wa kishetani.

Kila aliyepo duniani ni ama amezaliwa na Mungu ama amezaliwa na shetani, hivyo, kuna wana wa Mungu na wana wa shetani. Kuna namna Mungu huongoza uzao wake, shetani pia. Kila mtu unayekutana naye, kula naye, kukaa naye, kufanya naye kazi, kwenye biashara, kwenye ndoa, au maeneo yoyote, ni ama mwana wa Mungu au mwana wa Ibilisi. Kanisani pia wapo wana wa Mungu na wana wa ibilisi, na ndiyo maana wana wa Mungu tumedhihirishwa kuzivunja kazi za Ibilisi

“atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.”1 Yohana 3:8.

Kila kilichozaliwa na Mungu ni Mungu na kila kilichozaliwa na Ibilisi ni Ibilisi, kama vile kila kilichozaliwa na nyoka ni nyoka na kilichozaliwa na mnyama ni mnyama. Uzao wa nyoka ni uzao wa kishetani. Katika kitabu cha Mwanzo 3:14-15, Mungu aliweka uadui kati ya uzao wa nyoka amba oni uzao wa kishetani, na uzao wa mwanamke ambao ni uzao wa Mungu. Hii inatuonesha kuwa tangu mwanzo kuna uadui kati ya uzao wa Mungu na uzao wa shetani na hata vizazi na vizazi. Uzao wa Mungu wana miili na wanaitwa wana wa Mungu, na uzao wa shetani wana miili na wao wanaitwa wana wa Ibilisi.

Uzao wa mwanamke umepewa mamlaka ya kuponda kichwa cha uzao wa nyoka. Hata hivyo hatupondi Kichwa cha nyoka kwa jinsi ya mwili; tunampiga kwa silaha zenye uwezo katika Mungu

“Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.”2 Wakorintho 10:3-6.

Kwa sababu hii, unapaswa, kama mwana wa Mungu, kufyeka kwa mamlaka uliyopewa, kuponda kwa mamlaka uliyopewa, kung’oa kwa mamlaka uliyopewa pando lolote lisilofaa; yampasa Mwana wa Mungu kutumia sauti ya mamlaka.

Mathayo 12:34-37 inatuonesha jinsi Yesu alivyoshangazwa kuona wana wa uzao wa nyoka wakiwa na muonekano tofauti na wanenayo. Uzao wa nyoka umefanana kila kitu na baba yao; wananena kama baba yao, asili ni kama baba yao, uongo nis awa na baba yao.

Ukiona mtu anakutendea ubaya ujue huyo ni wa uzao wa nyoka, anaweza akawa kazini kwenu, nyumbani au sehemu yoyote. Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema, na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. Uzao wa nyoka hutoa mabaya, na uzao wa Mungu hutoa mema. Wana wa Mungu tumepewa mamlaka juu ya uzao wa nyoka (Marko 16:17-18).

Mungu akizaa anaza Mungu, na kila kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Mungu anakutambua kuwa wewe ni mwana wa pendo lake na wewe ni mtoto wa Mungu. Wana wa Mungu ni uzao mteule ambao huushinda ulimwengu (1 Yohana 5:4, 1Petro 2:9). Wana wa Mungu wakitenda ni Mungu ametenda, wakisema ni Mungu amesema.

Siku zote utambulisho wetu kama wana wa Mungu unapaswa kuwa wazi na Dhahiri kuwa sisi ni wana wa Mungu (1 Yohana 3:1). Kwenye Biblia, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake namna ya kuomba ambayo inawatambulisha wazi kuwa wao ni wana wa Mungu; “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje”. Uhusiano wetu na Mungu ni wa Baba na wanaye (Wagalatia 3:26, Yohana 1:12).

Ushetani unatokea sana mahali ambapo pana wivu. shetani amehama kutoka kuwa pepo na sasa yupo kwenye hatua ya kuwa mtu. Shetani ana uwezo wa kuingia ndani ya mtu na kumfanya mtu aweze kufanya jambo la kishetani. Wapo watu ambao ukikutana nao na mambo wanayoyatenda ni Ibilisi kabisa (Yohana 8:44).

Kila mmoja hubeba kiu ya baba yake. Wana wa Mungu tumebeba kiu ya Baba Yetu, ambayo ni kufungua watu, kusaidia watu, kuombea watu, n.k; wana wa Ibilisi wamebeba kiu ya baba yao. Wana wa Mungu tunaye Roho wa Baba yetu asemaye ndani yetu (Mathayo 10:19-20).

Uwezo wa Malaika kuwa Mtu.

Kama tulivyoona hapo mwanzo, Malaika wana uwezo wa kujigeuza kuwa kitu chochote au hali yoyote ili kutimiza lengo Fulani (Waebrania 1:7).

-      Malaika aweza kuwa maji na kusababisha maafa (Ufunuo 16:5),

-      Malaika aweza kuwa moto na kusababisha maafa ya moto (Ufunuo 14:18),

Mfano wa maafa ni 1 Wafalme 18:38 (Eliya).

Kwakuwa Malaika aweza kuwa kama ilivyoelezwa, Malaika aweza pia kuwa mtu.

Mwanzo 18:1- ; -

-      Bwana kamtokea Ibrahimu.

-      Ibrahimu mbele ya macho yake anaona watu watatu.

-      Ibrahimu aliwakaribisha nyumbani mwake, wakanawa miguu na wakala chakula.

-      Ni malaika ambao wana tabia zote alizonazo mtu wa kawaida.

Bwana anaongea na sisi kila siku akiwa ndani ya mtu/watu. Sisi tunaona mtu/watu lakini ni Bwana.

Mwanzo 19:1- ; -

-      Malaika wawili nyumbani kwa Lutu.

-      Lutu aliwakaribisha saw ana walivyokaribishwa na Ibrahimu.

-      Walinawa miguu yao na walikula chakula.

-      Wenyeji wa Sodoma waliwaona kuwa ni watu na kutaka kuwatendea ubaya.

-      Wanaonekana ni watu machoni pa watu lakini wana matukio ya kipekee, Mfano; walinyoosha mkono watu wakawa vipofu.

Malaika wanaweza wakaoa na kuolewa kwasababu wanaweza wakawa Binadamu. Kuna watu upo karibu nao na kuonekana ni wema sana na wakarimu, na kama ni rafiki au mchumba wako ila kumbe sio binadamu ila kumbe ni malaika. Wakikutendea mabaya ni Malaika wa giza waliovaa umbo la binadamu, na wakikutendea wema ni Malaika wa nuru waliovaa umbo la binadamu.

Wapo wajumbe wa Mungu huja kwenye maisha yetu kama watu wa kutushika mkono kututoa kwenye dhiki ili kutupeleka sehemu sahihi, lakini wapo hukataa kushikwa mkono. Mfano ni mke wa Lutu; hata aliposhikwa mkono na wale Malaika aligeuka nyuma na kuwa jiwe la chumvi (Mwanzo 19:16, 26).

Yoshua 5:13 ; -

-      Mungu alituma askari wa mbinguni/Malaika akiwa na upanga ambayo ni silaha; ni kwa sababu Yoshua alikuwa vitani.

-      Malaika wa Mungu hututokea ili kutusaidia kwenye matukio yetu. Hututokea kama watu wa aina fulani inayoendana na hali au tatizo lililopo; kama biashara, huja kwa sura ya biashara

“Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.” Mwanzo 32:24

Malaika wanapokutana na Mtu humuachia alama au tukio fulani; hata kwa malaika wa kuzimu na wao wanatumia njia hiyo ya kusababisha alama za matatizo juu ya watu wa Mungu na lengo ni kuwazuia wasiende kule ambako Mungu amewakusudia waende.

-      Yakobo alishindana na Malaika aliyekuja kama mtu.

-      Malaika alimgusa Yakobo kwenye uvungu wa paja ili ateguke amwachie; Yakobo aliumia na kumwachia malaika.

Mtu huwa na udhaifu uliosababishwa na jambo la Malaika lakini Malaika wa giza hupofusha watu wasiweze kuona udhaifu huo.

Malaika wa Giza na Matukio ya Kichawi.

Mwanzo 32:1-2

Zaburi 78:47-49 – Kundi la Malaika waletao mabaya. Kila ubaya, hasara, huzuni, au mabaya yoyote yanaletwa na Malaika wa giza, mfano, mvua yam awe iliyoua ng’ombe.

2 Samweli 24:15 – Mwalaika mwenye kuwaharibu watu. Yupo katika sura ya mtu. Alinyoosha mkono wakafa watu elfu sabini.

Daudi alimuona Malaika; Malaika akivaa umbo la mtu anaonekana. Yapo magonjwa au hali Fulani mbaya katika maisha yanasababishwa na watu. Mfano, Malaika waletano mabaya huweka mipaka kwenye elimu, umasikini, umri wa kuishi n.k. Ni mtu kabisa anakutamkia maneno ya uharibifu ila nyuma yake kuna mjumbe/wajumbe wa uharibifu.

Mabaya yanatokana Kundi la malaika wa kuzimu, kila tatizo linalokuja kuna malaika wanaoleta mabaya juu ya mtu na wamevaa sura ya binadamu. Chanzo cha Ugonjwa kinatokana na malaika mmoja na kila atakaye pata Ugonjwa huo wanakuwa na tabia zinazofanana.

Mungu alishafanya maisha yetu yafanikiwe kabla hatujazaliwa. Yeye anatujua zaidi ya tunavyojijua. Wana wa Ibilisi wapo kutuharibia kila kitu lakini bado Mungu anatusaidia.

Ili Mungu akusaidie, ni sharti uwe mtoto wake. Ukizaliwa na Mungu unaushinda ulimwengu (1 Yohana 5:4). Ukimkiri Yesu unakuwa umezaliwa mara ya pili. Tukiwa wana wa Mungu tu tunaruhusa ya kuzivunja kazi za Ibilisi.

BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA YA JUMAPILI

Post a Comment

0 Comments