google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUBOMOA MADHABAHU ZA MATESO

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 10.05.2026
ASKOFU DKT GERSHOM MWAKILA
SOMO: KUBOMOA MADHABAHU ZA MATESO

Madhabahu hutumika kuimarisha ama kudhoofisha jambo fulani kwenye maisha ya mtu. Yapo mateso katika maisha ya mtu ambayo yanasababishwa na madhabahu za kishetani. Madhabahu ikibomoka mateso katika maisha yako yanaondoka. Neno madhabahu limeandikwa mara 363 kwenye biblia. Kuna madhabahu ya Mungu ambayo watu wa Mungu huiendea, lakini pia kuna madhabahu ya Shetani ambayo watu wa shetani huiendea.

“Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.” Maombolezo 3:3

 

MADHABAHU NI NINI?

1. Madhabahu ni mahali ambapo ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili unakutana. Ulimwengu wa roho una pande mbili, ambazo ni ulimwengu wa nuru na ulimwengu wa giza.

2. Madhabahu ni mahali ambapo viumbe kutokea rohoni hupewa ruhusa kutenda kazi katika ulimwengu wa mwili. Madhabahu ina ruhusu viumbe wa rohoni kutenda kazi mwilini.

“Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.” Luka1:10

3. Madhabahu ni mahali ambapo maagano yanafanyika na yanaimarika. Mfano, maagano ya ndoa huanzia madhabahuni. Na ili maagano ya ndoa yavunjike, ni lazima iwepo na madhabahu nyingine itakayo husika.

Maagano ni kama mkataba kati ya mtu na mtu. Mfano, ukiingika makataba wa kupanga kwenye nyumba fulani na mkataba ukisainiwa, mwenye nyumba hawezi tena kuingia kwenye hiyo nyumba bila ruhusa ya mpangaji. Ndivyo hivyo kwa Mungu na wanadamu, ili yeye kuja katika maisha yako ni kupitia wewe kumkaribisha Yesu aingie ndani. Ndiomaana mtu akitaka kuokoka huenda madhabahuni kwaajili ya kuweka agano la wokovu na Mungu.

4.           Madhabahu ni daraja kutoka kwenye ulimwengu wa mwili kwenda kwenye ulimwengu wa roho na kutoka kwenye ulimwengu wa roho kwenda kwenye ulimwengu a mwili.

 

MADHABAHU NA SADAKA

Kila madhabahu inahitaji sadaka. Sadaka ni njia ambayo mtu anaweza kuitumia kujiungamanisha na madhabahu fulani. Kwa kila agano ambalo Mungu hufanya na watu wake, hujenga madhabahu na kuagiza sadaka itolewe kwenye madhabahu hiyo ili kujiungamanisha na agano hilo.

Nuhu baada ya gharika kuisha, aliposhuka kwenye safina alijenga madhabahu na kuweka sadaka juu yake ili kufanya agano na Bwana. Unapotoa sadaka katika madhabahu fulani, unajiungamanisha na agano la madhabahu hiyo. Hivyo ukifanya agano katika madhabahu ya Mungu, Mungu anashuka na kuhusika na maisha yako katika biashara, afya, ndoa na jambo lolote linalokuhusu.

Mungu ni mwaminifu kwenye agano lake. Shida ya watu ni kwamba kama hana vitu anamtumainia Bwana, ila akishapata vitu anamsahau aliyemwezesha kupata. Anasahau kurudi mahali ambapo agano lilifanywa na linaimarishwa.

 

MADHABAHU NA HALI YA MTU

Hali yoyote uliyonayo imeachiwa kutoka kwenye madhabahu fulani, ama madhabahu ya Mungu au ya Shetani. Mambo kama furaha, amani, ushindi, uaminifu, upendo na mafanikio hutoka kwa Bwana. Mateso, shida, taabu, magonjwa hutoka kwenye madhabahu za giza. Kila alichonacho mtu amepewa.

 “Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea.” Mwanzo 12:7

Unavyokuwa karibu na madhabahu ndivyo maagano yanaimarika zaidi. Madhabahuni ni mahali amabapo kuna nguvu, na unavyokuwepo kwenye madhabahu ni kama unachaji na kuwa na nguvu zaidi. Kuna mambo utahitaji fedha na mambo mengine utahitaji akili ya kawaida ili kuyafanya, lakini yapo baadhi ya mambo huwezi kuyafanya bila nguvu ya madhabahuni.

"Mwanzo 35:7"

Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.

 

AINA YA MADHABAHU

Madhabahu zipo za aina mbili kuna madhabahu za Mungu na madhabahu za kishetani. Madhabahu za kishetani hufanya kazi kama madhabahu za Mungu isipokuwa tu, zenyewe hutenda kazi katika uovu. Kwenye madhabahu za shetani kuna madhabahu zingine ndani yake. Kuna madhabahu zinazohusika kuloga viongozi katika nchi na zingine kuloga wananchi.  Lakini pia kuna madhabahu za hofu.

 

MADHABAHU YA HOFU

Hofu ni kinyume cha Imani. Mara nyingi kabla shetani hajaleta jambo lolote ovu, hutanguliza hofu ili kuua imani. Hofu ni kuogopa hata kwenye mazingira ambayo Mungu anatenda kazi. Silaha kubwa ya shetani ni mtu kuwa na hofu.  Unaweza ukawa shujaa lakini ukaishi maisha ya hofu.

Kama una hofu, ni lazima kiwepo kitu kinachokufanya uwe na hofu. Yawezekana kuna jambo liliwahi kukupata ama kuna hali iliwahi kukukabili ambayo ikazaa hofu ndani yako. Madhabahu za Bwana humfanya aliye na hofu akawa shujaa, aliye maskini akawa tajiri.

Ukiona mambo yako hayaendi sawa, iko madhabahu amabayo inahusika. Ukiwa na hofu hata mahali penye fursa utaogopa. Ukiwa na hofu hata mahali penye ajira utaogopa. Kuna madhabahu ambazo huzuia watu wasipate ajira au nafasi au cheo. Zipo madhabahu za hofu ambazo huipa nchi hofu.

Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.” Hesabu 12:5

Zipo madhabahu zinazozuia viongozi wasitoke kwenye mkoa fulani. Ziko madhabahu zinazozuia mtu asifike kwenye hatima yake. Kuna madhabahu zinazui watu wasiwe na afya njema. Kuna mdhabahu zilizojengwa kwenye taifa kuzui maendeleo katika nchi. Kuna madhabahu zinazolaza watu ambapo watu huwaza katika kiwango cha chini. Zinawafanya watu wasihoji mambo muhimu katika nchi. Na ili uweze kupata, ni lazima madhabahu hizo zivunjwe.

MAOMBI YA KUVUNJA MADHABAHU

“Kwa jina la yesu kwanzia sasa naziendea madhabahu zote za hofu zilizojengwa kuharibu maisha yangu kwa jina la Yesu, madhabahu za hofu zilizojengwa kuharibu afya yangu, madhabahu za hofu zilizojegwa kuharibu kazi yangu kwa jina la Yesu ninaziendea kwa damu ya Yesu. Madhabahu zote za hofu maala popote zilipojengwa kwa jina la Yesu ninaziendea kwa mkono wa Bwana nazivunja,nazivunja  nazibomoa kwa jina Yesu kama ambavyo Gidioni alivyoambiwa akabomoe madhabahu ya Bahari na mimi leo nimeambiwa nikabomoe madhabahu za kishetani zenye kutia hofu kwa Jina la Yesu mahala popote kwenye mkoa wangu au wilaya au kijiji au tarafa au nyumba ilipojengwa madhabahu ya hofu kwa jina la Yesu ninakwenda naibomoa kwa jina la yesu nnabomoa madhabahu ya hofu nazibomoa leo kwa jina la Yesu” Amen

BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA YA JUMAPILI

Post a Comment

0 Comments