Sunday, May 26, 2013

SADAKA ZA MASHETANI

Mch,Josephat Gwajima.
Tangu agano la kale Mungu alikua anatolewa sadaka,na sadaka ilikua inatumika kama mkataba kati ya mtu na Mungu katika lile jambo ambalo anataka Mungu amfanyie.

Mchungaji Josephat Gwajima
Mfano, Ibrahim alimtolea Mungu sadaka,na Mungu akamfanya kuwa baba wa mataifa,Yakobo alimtolea Bwana sadaka na Mungu akafanya nae agano la kumlinda na kumfikisha salama kule alikokua anakwenda. Unapomtolea Mungu sadaka unaingia kwenye mapatano na Mungu juu ya suala ambalo unataka Mungu akufanyie.

Leo sio lengo langu kuongelea sadaka hizo ambazo mtu anamtolea Mungu,bali lengo langu ni kuzungumzia sadaka zinazotolewa kwa mashetani,sadaka hizo ndizo ambazo zimepelekea maisha ya watu wengi kufungwa.
1 Wakorintho 10:20 “..wavitoavyo sadaka
kwa mashetani wala si kwa Mungu..”
 Hapa tunaona mashetani wanaweza kupokea sadaka kama ambavyo Mungu anavyoweza kupokea sadaka.

Kwanini mashetani wanapokea sadaka?
Kama ambavyo Mungu anapopokea sadaka linafanyika agano la mtu na Mungu katika lile jambo ambalo anataka amsaidie,ndivyo ilivyo kwa mashetani wanapopokea sadaka inakua kwa ajili ya kuwafunga watu na kuwashikilia katika matatizo ya aina mbali mbali

Mambo matatu kujua kuhusu sadaka ya mashetani;

Ø  Kuna sadaka ya kishetani
Ø  Mafundisho ya kishetani
Ø  Meza za kishetani
Dunia inaendeshwa na wivu,wanadamu wanakawaida ya kuoneana wivu hasa pale anapoona mwenzake anafanya vizuri kuliko yeye kwasababu hiyo wivu unampelekea mtu kufanya kitu chochote.
Watu wengi wanapomuona mwenzao anaendelea vizuri wana kawaida ya kwenda kutoa sadaka kwa mashetani ili kuweza kumrudisha yule mtu chini.

NI MUHIMU KUELEWA!!
Kila mtu asiye upande wa Bwana yuko upande wa adui(shetani),ndo sababu wachawi na waganga wa kienyeji wote watumishi wa shetani.
Watu wanapomuonea mtu wivu wanamuendea kwa mganga wa kienyeji ili kumfunga yule mtu,wanawafunga ili mambo yake yaharibike.
Ndio sababu kuna baadhi ya watu wana matatizo ya aina mbali mbali,kwa mfano kuna baadhi ya wanafunzi wakisoma wanaelewa lakini wakifika kwenye mtihani hawakumbuki chochote,hii ni kwasababu wanakua wamefungwa na waganga.

Sadaka za waganga wa kienyeji
Mtu anapoenda kwa mganga ili kutaka jambo lifanyike kwa mtu mwingine,mganga ana kawaida ya kuagiza sadaka kama kuku,mbuzi,ng’ombe au kitu chochote kinachotoa damu.Mganga wa kienyeji hawezi kuomba matikiti maji,au machungwa kwasababu kinachotakiwa ni damu ya agano ili kuweza kumfunga mtu,na wakati mwingine wanamchanja mtu chale ili damu ya mtu yule mwenyewe itumike kama sadaka.
Sadaka inapopelekwa kwa mganga ni kwa ajil i ya kutengeneza mkataba kwa ajli ya kumfunga mtu.Waganga wa kienyeji ni watumishi wa shetani asilimia mia moja na kazi yao ni kuwafunga watu wengine katika vifungo vya aina mbalimbali.
Sadaka inapopelekwa kwa mganga wa kienyeji na kuchinjwa mganga anawaita mashetani ambao wanaichukua ile sadaka na kuagizwa kwenda kumfunga mtu kulingana na maelekezo ya mganga,na hapo ndipo mtu anaanza kuwa na matatizo.
Ndio sababu ukristo sio kwenda kanisani kusalishwa bali ni kuwafungua wote waliofungwa na Ibilisi na kuwaweka huru,ndio sababu wakati yesu yuko duniani alifanya kazi kubwa ya kuwafungua waliofungwa.
Mashetani wanapenda sadaka za aina mbali mbali kama damu na udi,baada ya kupokea sadaka mashetani hao wanaenda kwa mtu nakuanza kusababisha matatizo ya aina mbali mbali.

Hii ndio sababu kama Mkristo unatakiwa ugundue shetani ni adui na tunatakiwa kushindana nae kila siku (waefeso 6:12)
Kuna kuwa na uhusiano kati ya sadaka iliyotolewa na tatizo la mtu alilonalo,mpaka uweze kuivunja nguvu ya sadaka ile ndio unapopata ufumbuzi wa tatizo lako.Sadaka inakuwa na kawaida ya kusimama kuunganisha kati ya mtu na tatizo lake

Sababu gani inaoufanya ukristo uwe na nguvu leo duniani??
Kitu kinachoupa Ukristo nguvu leo duniani ni kutokana na sadaka ambayo Mungu aliitoa pale msalabani kwa kumtoa mwanae.Sadaka ya damu ya Yesu ndiyo inayofanyika kama mkataba kati yetu sisi na Mungu,na kazi ya hiyo sadaka ni kutusamehe sisi makosa na dhambi zetu,kutuponya magonjwa,kukombolewa, kuwa huru.nk.
Ndio inavyokua kwenye sadaka za mashetani zinakua na nguvu ya kusababisha tatizo kuendelea kuwa kwenye maisha ya mtu,hii ndio sababu watu wanazunguka sehemu mbali mbali kuombewa bila kupata ufumbuzi,mpaka utakapoweza kuivunja nguvu ya sadaka hyio kwa damu ya yesu ndipo utakapo pata ufumbuzi sahihi.
Mashetani  yanapoingia kwa mtu huwezi kujua kama yameingia lakini utakachogundua ni kuona mambo yanaanza kwenda vibaya kila unalokua unafanya linakua halifanikiwi

Mtu anayeenda kanisani anaweza pia kufungwa na shetani
Mfano:

Ø  Paulo alizuiwa na shetani, Matendo 13:8
Mtume Paulo alikua anahubiri lakini mchawi alitaka kupindisha  injili aliyokua anahubiri
2 Wathesalonike 2:18
Paulo alizuiwa na shetani kwenda kuhubiri injiri
Ø  Shetani alisimama pembeni ya Yoshua aliyekua kuhani mkuu na kushindana nae. Zakaria 3:1.

Ndio sababu biblia inasema usimpe ibilisi nafasi,unapompa ibilisi nafasi hata kama umeokoka anapata nafasi ya kukufunga,njia ya kumshinda shetani kwa asilimia miamoja ni kwa kufunga milango yote hasa ya dhambi katika maisha yako.
Unapotoa sadaka kwa Mungu kunakua na mapatano ya kimungu ili Mungu asimamie ustawi wako na maendeleo yako ,ndivyo  walivyo mashetani wanapopewa sadaka wanakua na nguvu ya kusimamia matatizo katika maisha ya mtu,hii ndio sababu kuna watu wana mapepo ambayo yamekataaa kuachia maisha yao kwasababu sadaka hazijavunjwa.

Namna ya kuvunja sadaka
Sadaka iliyotolewa katika maisha yako inaweza kuvunjwa kwa kutumia jina na damu ya Yesu,unatakiwa uombe kwa kutumia jina la Yesu na damu ya Yesu kuvunja kila sadaka iliyotolewa katika maisha yako ili kukufanya uharibikiwe,unaharibu kila nguvu ya sadaka iliyosababisha taabu na shida katika maisha yako.

Kwanini wahawi wanatumia damu?
Uhai wa wa mwanadamu uko katika damu yake,na uhai wa mnyama uk ndani ya damu yake.
Walawi 17:11 “..Kwakua uhai wa mwili uko katika hiyo damu ..”
Waganga wa kienyeji wanapotumia damu kufanya maaagano damu ile inasimama kwa gharama ya uhai wa kiumbe kilichotolewa damu hiyo.

Mambo ya kufahamu kuhusiana na damu
Mwanzo 4:10 “Akasema umefanya nini?sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi..”
Ø  Damu ni uhai
Ø  Damu ina sauti
Ø  Damu inaweza kulia
Damu zinazotelewa kwa waganga wa kienyeji zinakua zinanena mambo mabaya katika maisha yetu kila siku ndio sababu mtu aliyotolewa sadaka kwa mganga wa kienyeji matatizo aliyonayo yanakua na kawaida ya kuongezeka siku baada ya siku.
Sababu kwanini lazima tunyamazishe damu ni kwasababu damu nyingine zote katika maisha yetu zinatakiwa kunyamaza kimya na damu ya Yesu iweze kunena yale ambayo inatakiwa kunena katika maisha yetu
Waebrania 12:24 “..na Yesu Kristo mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyiza inenayo mema kuliko ile ya Habili”

Damu ya Yesu inanena ushindi katika maisha yetu leo,inanena uponyaji,inanena ukombozi na mafanikio katika maisha yetu katika jina la Yesu

No comments:

Post a Comment