SOMO: SHERIA MBILI ZA ROHONI
TAREHE: 19/10/2014
NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima |
Ulimwengu tunaoishi
umegawanyika kwenye sehemu mbili; ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili. Mambo
huanzia kwenye ulimwengu wa roho na kisha hudhihirika katika ulimwengu wa
mwili. Mtu anapofanikiwa rohoni baadae anafanikiwa mwilini. Unapopatwa na
matatizo mfano magonjwa elewa kuwa matatizo hayo yameanzia rohoni. Unapoanza
kuomba na kushambulia lazima utambue kuwa unashindana na ulimwengu wa roho. Imeandikwa;
“ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu
ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12
Mama mchungaji Grace Gwajima |
Kumbe kabla ya udhihirisho wa baraka katika maisha yako
lazima ubarikiwe rohoni. Ulimwengu wa roho ni dhahiri kabisa, hivyo kama
ambavyo tunaona miji katika ulimwengu wa mwili ndivyo ilivyo katika ulimwengu
wa roho. Hivyo ukibarikiwa kwenye mji wa Dar-es-salaam rohoni baadae
utabarikiwa kwenye mji huo katika ulimwengu wa mwili. Kujua mistari mingi ya
biblia sio ishara ya kuwa mtu ni wa kiroho zaidi, Mungu ni roho hivyo ni lazima
tumwabudu katika roho na kweli. Imeandikwa.
Viumbe ambavyo makazi yake nikatika ulimwengu wa roho ni
Mungu, malaika, mashetani ambao ndio wale malaika walioasi. Viumbe wa kimwili
ni kama wanadamu, kuku, simba, miti.
Katika ulimwengu wa roho, kuna sheria mbili zinazouongoza.
Mambo yote huanzia katika ulimwengu wa roho, hasa katika ndoto. Zipo sheria
mbili, zinazoongoza ulimwengu wa roho.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima Akifundisha Sheria mbili za Rohoni |
1.
UWEZO
WA KUBADILI MAUMBO.
Ili mawakala wa shetani ambao ni wachawi waweze kwenda
kuroga lazima watoke ndani ya miili yao na kuvaa umbo jingine ili
wasitambulikane. Kwa kuwa anakuwa rohoni anaweza kuvaa umbo lolote, kugeuka
kuwa kitu chochote mfano paka, mbwa, kunguru. Furaha ya mchawi ni kukusikia
ukiendelea kusema jana kulikuwa na paka analia kama mtoto kwenye dirisha langu.
Imeandikwa;
“Baada ya hayo
akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika
njia kwenda shamba.” Marko 16:12
Yesu aliwatokea wanafunzi wake akiwa na sura nyingine,
lakini kwa kuwa alikuwa rohoni, alionekana kuwa na sura nyingine. Yesu ana sura
nyingi, kama umezoea kumuona kama daktari leo ana sura nyingine. Akitaka
kukutokea kama mmea atakutokea kama ua la sharoni, akitaka kukutokea kama
mnyama atakutokea kama simba wa kabila la Yuda, akitaka kukutokea kama kinywaji
atakutokea kama maji ya uzima. Lazima utambue kuwa Mungu anaweza kukutokea kwa
sura nyingine tofauti na ile uliyoizoea.
Mchungaji Gwajima akimsifu na kumwabudu Mungu. |
UKIRI
Leo, katika jina la Yesu; Yesu unitokee kwa sura nyingine.
Nimezoea kukuona kama mponyaji tu, leo nitokee
kama mfariji, kama mfalme wa wafalme, kama mwamba wa kale. Leo Yesu nitokee kwa
sura nyingine sawasawa na tatizo nililonalo. Amen.
“Yesu akamwambia,
Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza
bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami
nitamwondoa.” Yohana 20:15
Ni rahisi sana watu wasiokufahamu kukuamini kuhusu mambo ya
imani kuliko mtu aliyekuzoea mfano mama yako au ndugu uliokua nao. Hawawezi
kuamini kirahisi; ndiyo maana Yesu alimtokea mama yake kwa sura nyingine kama
mtunza bustani, ili aweze kumwamini. Aliweza kufanya hivyo kwa sababu alikuwa
rohoni. Watu wamemzoea Yesu wa kuponya magonjwa tu lakini Yesu anatokea kwa
sura nyingine nyingi ili mambo yaweze kutokea na watu wamwamini.
Hivyo ili uweze kufanya jambo la rohoni lazima uvae sura
nyingine. Imeandikwa;
“Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi
katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa
kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,” Ufunuo 1:9-10
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,” Ufunuo 1:9-10
Roho inaweza kuvaa sura yoyote ndiyo maana Yesu alimtokea
Yohane katika sura nyingine kwenye kisiwa cha Patmo. Imeandikwa;
“Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre,
alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake
akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga
mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,” Mwanzo18: 1-2
Kumbe roho inaweza kugeuka na kuwa kitu chochote, na
kufanaya kazi kama wanadamu. Imeandikwa;
“Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa
moto wa miali.” Zaburi 104:4
Unaweza ukakuta upepo mkubwa sana umevuma na ukaleta maafa
makubwa. Wanasayansi wakauita janga la asili, wakalipa jina na kupima spidi
yake na kutoa majibu ya maafa yaliyotokea. Lakini kumbe ndani ya upepo ule
kulikuwa na mtu. Lazima utambue kuwa kuna upepo
unaosumbua hali ya maisha yako ndo maana unaona taabu na misukosuko; na
yupo aliyejigeuza kuwa huo upepo.
Yesu aliposema na tuvuke ng’ambo, shetani aliyajua hayo na
kutikisa chombo. Tambua hata wewe kwenye maisha yako ukiona umepanga kufanya
jambo lolote la maendeleo na mara gafla matatizo yanaanza kuibuka jua yupo
anayetikisa chombo chako. Usikubali, pigana maana ni upepo uliotengenezwa ili usifike unakokwenda au
usifanye unachotakiwaa kufanya. Imeandikwa;
“Ndipo Farao naye akawaita wenye akili
na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.” Kutoka 7: 11-12
Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.” Kutoka 7: 11-12
Hii haimanishi kuwa mashetani wana uwezo wa kutengeneza
chura, au nyoka au fimbo ila tu waliagiza mashetani mengine yajigeuze kufanyika
chura, nyoka au fimbo. Kama ambavyo malaika wa nuru wanavyoweza kuvaa maumbo, mashetani pia wanaweza kuvaa sura na maumbo ya
kitu na kutimiza kusudi. Imeandikwa;
“Wala si ajabu. Maana
Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.” 2Wakorintho 11:14
Wenye matatizo mbali mbali wanafunguliwa kwa jina la yesu. |
1. Majoka amabao ni roho ya uovu
walioanguka kutoka mbinguni baada ya uasi.
“Kulikuwa
na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka
naye akapigana nao pamoja na malaika zake;” Ufunuo 12:7
2.
Mizimu.
Haya ni mashetani waliotawala ukoo kwa muda mrefu. Sio roho za watu waliokufa
kwenye ukoo bali ni mashetani ambayo yanaufahamu ukoo kwa undani.
3.
Miungu.
Ni mashetani waliopewa makafara kwa muda mrefu na wakapewa nguvu na kuwa miungu
4.
Majini.
Hawa ni mashetani wenye asili ya kiarabu. Hupatikana kwenye sehemu zenye
tamaduni za kiarabu.
Imeandikwa;
Nikaona roho tatu za
uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika
kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Ufunuo 16:13
Akalia kwa sauti kuu,
akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na
ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
Ufunuo 18:2
Nguvu kubwa ya mashetani ni ule uwezo wa kutokutambulikana.
Wanapotoka ndani ya miili huwa wananuiza na kuvaa maumbo bandia. Wachawi huwa
wanakaa na kukusikiliza kama
umewatambua, kutokuwatambua kwako ni furaha kwao maana wanajua kuwa kuna jambo
limefanyika na wamefanikiwa.
Maelfu ya watu wakiwa ndani ya bonde la kukata maneno |
UKIRI
''Kuanzia leo lazima
kila atakayekuja kuniroga nitamuona kwa jina la Yesu. Kila aliyegeuza umbo
naamuru nimuone katika umbo lake la asili kwa jina la Yesu.''
Wapo watu ambao ukiongea nao husema kuwa wanasikia miguu
inawaka moto au misumari ndani ya masikio. Wasilolijua watu hawa ni kuwa
mashetani yamevaa umbo la moto au misumari na kukaa ndani ya miili yao. Inawezekana,
unajisikia kumtukana mume au mke wako
lakini baada ya kufanya tendo hilo wewe mwenyewe unashangaa ilikuwaje.
Wameuvaa mdomo wako ndio maana. Inawezekana umeuwekea uso wako kila aina ya
urembo lakini bado unaonekana kama babu. Yupo aliyevaa umbo la babu na kukaa
kwenye uso wako. Ukiona nchi inayumbayumba lazima ujue kuna chanzo chake kiko
katika ulimwengu wa roho. Ukishinda vita ya rohoni mwilini waweza kushinda bila
hata kuwa na silaha rasmi.
MAOMBI
Ewe jini, joka,
mzimu, uliyegeuka umbo na kuja kwangu, lazima nikuone katika jina la Yesu. Ninaaamuru
wapigwe katika jina la Yesu. Ninasimama kama askari wa jeshi la Bwana, naangusha ngome za balaa,
ngome za mikosi, ngome za magonjwa katika jina la Yesu. Mimi nakataa kutawaliwa
na mashetani katika jina la Yesu.
Kuanzia sasa roho yoyote iliyogeuka na kuwa balaa, talaka,
mikosi, magonjwa, naivunja katika jina la Yesu. Kwa jina la Yesu, kuanzia leo
chochote kilichotumwa kwangu, nilichokinunua kwa fedha yangu ila ni shetani
aliyevaa umbo, nakiangamiza katika jina la Yesu. Kitu chochote, au roho yoyote,
iliyo ndani ya nyumba yangu naivunja, nairudisha ilikotoka katika jina la Yesu.
Amen!
2.
UNAMFUMBA
MTU ASIKUTAMBUE.
Sheria ya pili ni kuwafumba watu ili wasiwatambue. Yani,
uendelee kuamini kuwa vitu uvionavyo kwa macho au ndotoni ndivyo vilivyo. Akili
ya mtu ikifungwa mtu akiona hatambui kama ni wachawi au mashetani. Yawezekana
kila ukilala na kuota ndoto ukiamka unaanza kusema uliyoyaota ambayo yako
katika sura bandia. Inatakiwa uwafunge
ili wasijifiche wakija uwatambuae katika jina la Yesu. Bila kuomba huwezi kupokea uwezo wa
kuwatambua. Imeandikwa ;
“Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili
Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu,
nitalifanya” Yohana 14:13-14
Maelfu wakimsifu Mungu katika bonde la kukata maneno.. |
MAOMBI
Katika jina la Yesu namteketeza mtu yeyote
aliyejigeuza sura ili anitese, ninamfyeka katika jina la Yesu.
Kila atakayekuja katika umbo lolote
lazima nimjue katika jina la Yesu, ninawafunga
wasinitambue kama mimi nimewaona. Kuanzia leo naamka kutoka kwenye usingizi wa
kiroho, akili yangu iwaze kutawala, iwaze biashara katika jina la Yesu .
Kuanzia leo naanza kutambua kazi yangu, naanza kuelewa kazi ya kufanya,
biashara ya kufanya, katika jina la Yesu.
Nawashambulia mashetani wote katika
jina la Yesu, mashetani walioshikilia familia yangu, kazi yangu, ndoa yangu,
biashara yangu katika jina la Yesu. Ninawaangamiza katika jina la Yesu.
Nawaangamiza maadui zangu wote katika jina la Yesu. Natumia mamlaka aliyonipa
Yesu, ninawafyeka wanaozuia kazi yangu ninawafyeka wanaozuia ndoa yangu, ninawafyeka
wanaozuia huduma yangu katika jina la Yesu. Nawashambulia kwa damu ya
mwanakondoo. Imeandikwa;
“Kila silaha itakayofanyika juu yako
haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa
mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu
mimi, asema Bwana.” Isaya 54:17
Nawafyeka
katika jina la Yesu, mtu yeyote aliyesimama kwenye njia zangu kunizuia
nisifanikiwe, kuzuia nisisonge mbele, kunizuia nisipate ajira, nafunga uwezo
wako wa kujigeuza na kuwa balaa, mikosi,
kuwa matatizo ,kuwa mtego, nawashambulia katika jina la Yesu.
Naharibu uwezo wenu katika jina la Yesu,
nang’oa madhabahu zenu katika jina la Yesu. Nawatiisha, nakata mamlaka zenu, kila
kiumbe kinachotumika kuharibu maisha yangu nakishambulia katila jina la Yesu.
Naharibu uweza wenu wote katika jina la Yesu.
Natangua yote mliyoyapanga katika jina
la Yesu. Imeandikwa;
“yeye uyatangua mashauri ya
wadanganyifu na mikono yao isipate kutimiza makusudi yao.”
Kila vibarua wa shetani mnaovaa sura
bandia nawaangamiza katika jina la Yesu, navunja kila laana ya familia iliyonipata
kupitia viumbe wa rohoni mnaojibadilisha sura na kuniroga. Ninawafyeka katika
jina la Yesu.
Kila nguvu ya giza inayotawala maisha
ninailaani katika jina la Yesu, kila balaa zinazotawala maisha yangu nazivunja
katika jina la Yesu. Nakiri leo niko huru, maisha yangu yako huru katika jina
la Yesu. Amen!
Hakika Mungu ni mwema kwa watu wanaomtumainia yeye. |
1 Comments
Barikiwa mtumishi wa Mungu.
ReplyDelete