google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MJUMUISHO WA SEMINA YA NILIPATA KUTOKA NDOTONI

 
JUMAPILI, 16.08.2020
BISHOP DR. JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: NILIPATA KUTOKA NDOTONI

MWANADAMU ANA VIPANDE VITATU:

1) Roho

2) Mwili

3) Nafsi

Mwili wa mtu unatokana na mavumbi pumzi ilioingia ndani ya mtu ndio roho ya mtu ndio uhai  wa mtu .Mungu alipo kupulizia pumzi ndio alipotengeneza nafsi yako.

NAFSI NA VITU VITENDAVYO KAZI NDANI YAKE:

1/ Hisia za mtu

2/ Utashi

3/ Nia

4/ Moyo

Mtu anapokufa roho inatoka ndani ya mwili na nafsi inapotea ndani ya mtu, Kitu chochote kikikuingia kinakaa ndani ya nafsi na chochote unacho kisikia kinaingia ndani ya nafsi. Shetani akiamua kumfunga mtu anachagua kwa kumfunga mtu .Mwili wako umetengenezwa na muunganiko wa baba na mama yako lakini roho yako imetoka mbinguni.

WAISLAMU WANA AINA MBILI YA ELIMU:

1/ ELIMU AHELA (Nyota )

2/ ELIMU DUNIA (Faraq na Buruji)

Wewe umeshuka kutoka mbinguni kama ulivyo na hakuna  mtu wa kukuzuia wewe kufanya kitu unachotaka kufanya.

Mungu anajivunia watu majasiri, Mungu anatembea duniani kwa kupitia miguu  yako na anapo sema anasema  kwa kupitia midomo yako lakini ukikaa kimya na Mungu naye anakaa kimya.

ADUI WA MTU DUNIANI:

1/ Dunia

2/ Mwili

3/ Shetani

Mfanano kati ya Eliya Mtishibi na Yohana Mbatizaji, maana Eliya alipo kufa akaja Yohana mbatizaji kwaumbo la Yohana Mbatizaji  lakini ndani yake alikua na roho ya Eliya.

VITU WALIVYO FANANA ELIYA NA YOHANA MBATIZAJI:

1/ Wote walikuwa wana kaa Jangwani

2/ Wote walikua wana kula Nzige na Asali

3/ Wote walikua wana Mashuka ya Ngozi

4/ Wote walikua wana Kemea Makuhani na Wafalme

Unapozaliwa lazima uwe na  kiu ya kufanya kitu fulani lakini kama umezaliwa lakini ukawa hauna kiu ya kufanya kitu chochote basi jua wewe umeibiwa nyota. Ulipo shuka kutoka mbinguni ulitoka na kitu chakufanya duniani shetani apigani na wewe shetani anapigana na kitu ulicho kibeba ndani yako. 

Umetoka mbinguni kwa kusudi la Mungu ana ruhusu upinzani ilikukuwekea ujasiri ndani yako, mchawi anao uwezo wakuviona vitu ulivyo vibeba ndani yako. Makaburini kuna utajili  mwingi sana maana watu waliolala  na vitu walivyo toka navyo   mbinguni ndio maana  vita yako haipo mbali na wewe ila vita yako ipo ndani yako.

Hatima yako aifunguliwi na mitume peke yake ila Mungu anauwezo wa kuja kufungua hatima yako iliyo fungwa, usilipe ubaya kwa ubaya ila lipa ubaya kwa wema.

Mungu ana ruhusu shida ikupate  kwa muda kwajali ya kukunoa  kwa maisha yako ya badae, kuna mzigo uliotoka nao mbinguni ili uachie duniani.

Maisha yako ayabadilishwi na muonekano ulionao , Kuna mtu anahatima kubwa lakini ameshikiliwa na mashetani.

Mathayo 1:1-6

“Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;”

Kila Ukoo una kitabu chake ulipofikia leo sio kwa mapenzi yako ila ni kwa mapenzi  ya Mungu, ndio maana hadi leo upo. Mtu aliye mwaminifu kwenye mambo madogo anakuwa mwaminifu hata kwenye mambo makubwa.

Post a Comment

1 Comments

  1. Amen this blog spot is very impressive. Following closely

    ReplyDelete