google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NILIPATA KUTOKA NDOTONI (Part 3)

 

JUMANNE, TAREHE 11.08.2020
BISHOP DR. JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: NILIPATA KUTOKA NDOTONI     
                         
Bishop Dr. Josephat Gwajima

 NDOTO YA TATU

Mwanzo 31:22-29

 “Basi akakimbia yeye na yote aliyokuwa nayo; akaondoka akauvuka mto, akaelekeza uso wake kwenda mlima wa Gileadi. Hata siku ya tatu Labani akaambiwa ya kwamba Yakobo amekimbia, akatwaa ndugu zake pamoja naye, akamfuata mwendo wa siku saba. Akampata katika mlima wa Gileadi. Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari. Labani akamfikia Yakobo, na Yakobo alikuwa amepiga hema zake katika mlima, na Labani na ndugu zake wakapiga hema zao katika mlima wa Gileadi. Labani akamwambia Yakobo, Umefanya nini? Umenihadaa, ukawachukua binti zangu kama mateka waliotwaliwa kwa upanga. Mbona umekimbia kwa siri ukanihadaa, wala hukuniambia, nipate kuagana nawe uende zako kwa furaha, na nyimbo, na ngoma, na kinubi?Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.”

Mungu anaweza kukutokea kwenye ndoto ili akuonye. Kuna maamuzi ambayo unaweza kufanya kwako ukaona nisahihi lakini mbele za Mungu umekosea ndio maana  Mungu anakuja kwenye ndoto kukuonya juu ya mambo au jambo unalotaka kufanya au kulitenda juu ya mtu fulani.

Mungu anaweza kukuokoa na watu wenye hasira juu ya mtazamo waki Mungu uliouchukua katika maamuzi yako.

 NDOTO YA NNE:

YUSUFU NA NDUGU ZAKE:

Ndoto ya Yusufu inahusu utawala...

 Mwanzo 37:5

“Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia;”

Yusufu alichukiwa na ndugu zake kisa ndoto zake na maneno yake. Yusufu aliota ndugu zake wana mwinamia ukiwa na future kubwa na ukaiongea mbele za watu watakuchukia.

Kuna ukuu mwingine unaitaji maandalizi Mungu anakuletea ndoto iliunze kujianda juu ya ukuu wako, Maarifa yanatafutwa Mungu ni Mungu wa maandalizi.

Tunamambo makubwa ya kutenda lakini miili yetu ina ukomo ndio maana Mungu anakuletea ndoto iliufanye maandalizi Mungu anaweza kukuelekeza sehemu iliukaone maandalizi. Mungu akikuonyesha ndoto ya maisha yako ya badae usiseme

Hata ukisingiziwa jambo na mtu jua kabisa  anakupigisha hatua moja kwenda hatua nyingine, Kila mtu ana ndoto yake unapo ota ndoto na ikajirudia mara mbili jua kabisa hiyo ni ndoto ambayo Mungu kaithibitisha na itatokea kwa haraka zaidi

Maneno aliyo sema yusufu kipindi anamwambia Farao juu ya ndoto yake. Kwenye maisha kila mtu ana ndoto anayoiota kwa namna yake

Mwanza 41:32

“Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.”

Kuna wakati mtu anakuota kwasababu Mungu ameamua kumtumia mtu akuote kwasababu wewe ulikuwa busy unaweza ukaota ndoto sehemu nyingine naikatokea Sehemu nyingine

NDOTO YA TANO

YUSUFU NA FAMILIYA YAKE

                                                            

Mwanzo 36:9-12                                        

“Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri. Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reuli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau. Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi. Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.”

Yusufu akawambia Baba na Mama yake kwamba aliota nyota kumi na moja ziki muinamia. Mungu ana kanuni yake katika familia kila mtu anaye takiwa kupata ndio ana kosa na asiye takiwa kupata naye anapata.

 Ukitakiwa kupata unatakiwa uwe makini sana maana vita yako ni kubwa sana .Mungu anawapa wale wenye unyenyekevu na wale wanaojiinua huwanyima.

NDOTO YA SITA:

MNYWESHAJI NA MWOKAJI

Mwanzo 40:1-16

“Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri. Farao akawaghadhibikia maakida wake wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji. Akawatia katika lindo nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu. Mkuu wa askari akamwekea Yusufu watu hao, naye akawahudumu, nao wakakaa siku kadha wa kadha katika kifungo. Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika. Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie. Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu. Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva. Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake. Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake. Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii. Kwa sababu hakika naliibiwa kutoka nchi ya Waebrania, wala hapa sikutenda neno lo lote hata wanitie gerezani. Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu.”

Mungu anaweza kukuletea mtu ili kukutoa mahali ulipowekwa, hata kama kesho yako ni kubwa lazima matatizo yata kupata usimuone mwalifu ameletwa kwako ukamuona mkosaji sana kumbe ni Mungu kakuletea ili akutoe mahali ulipowekwa. 

Mungu anaweza kukuletea watu kwajili yakukuvusha mahali ulipo, kanuni ya ki Mungu ni kumkumbuka yule aliye kusaidia.

Unapo ota ndoto sio jambo ulilo liota litakupata maana yake umepewa taarifa kwajili ya kuligeuza jambo baya ambalo uliloliota lisikupate

NJIA ZA KUTAMBUA NDOTO NA KUIFANYIA KAZI

1/ Unatakiwa kubaini ndoto unayo iota  kama ni mbaya unatakiwa uivunje kwa haraka ili isikupate au isitokee.

2/ Ndoto ulioiota kama ni nzuri unatakiwa kuiita iliikufikie kwa halaka

Ndoto mbaya ni kwamba ulimwengu wa giza wamekuchorea mchoro ili jambo baya likupate, mchoro unao uona kwenye ndoto ndio mchoro ulio tengenezwa kwenye ndoto unauona kwenye ulimwengu wa roho. Mungu hawezi kukuletea ndoto ambayo haija hakikishwa.

Mungu akikuonyesha jambo unatakiwa kulifatilia katika ulimwengu wa mwili .usiogope kuingia mahali kisa ugumu uliokuepo maana Mungu anakuonyesha na kukuletea mtetezi katika njia yako. Kuna mtu Mungu anamtuma kwajili ya kukupigisha hatua ilikukufikisha katika ndoto yako.

Post a Comment

1 Comments

  1. Titanium bikes and bikes for sale - The iTanium Arts
    Shop the titanium melting point best titanium bikes, bikes, accessories titanium pot and best accessories at The titanium necklace mens iTanium Arts. Choose rocket league titanium white octane from our wide variety of models & styles of snow peak titanium motorcycles.

    ReplyDelete