google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NILIPATA KUTOKA NDOTONI (Part 5)

 

ALHAMISI, 13.08.2020
BISHOP DR. JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: NILIPATA KUTOKA NDOTONI


NDOTO YA DANIELI AKIWA BABELI

Daniel 7:1-3

“Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo. Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.”

NDOTO YA YUSUFU NA MARIAM

Mathayo 1:18-20

“Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.” 

Hii ndoto inatufundisha jambo fulani kwamba kijana kamchumbia mtu mara mchumba wake akawa mjamzito. Hii ndoto inaonesha maamuzi magumu akiwa disappointed, Mungu anamletea ndoto ili kumuongoza kutenda jambo wakati mgumu sana kwako. Mungu anaweza kutuongoza kutenda jambo kinyume na mapenzi yetu.

Hapa tunajifunza kwamba unataka kuamua jambo na umeamua kabisa Mungu anakutokea kwenye ndoto anakwambia usiamue hivyo, jifunze kusikiliza sauti ya mungu kwa upesi. Usiseme japo Mungu amesema na wewe unaendelea tu.

NDOTO YA MAMAJUSI WA MASHARIKI

Mathayo 2: 10-12

“Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.”

Hawa walifika wakakutana na mtu akawaambia kwamba wamjuze na yeye, hawa wanajua lile ni jambo zuri, kumbe yule jamaa alikuwa ana hila ili akamuue. Ndoto inatufundisha kumbe kuna watu watakupeleleza ila lengo lao ni lengo baya. Wataongea na wewe kana kwamba wanapenda kufanya kama unavyofanya kumbe wana hila, huwezi kujua hila yao mpaka uonyweshwe na Bwana.

Unamuona mtu mwanakondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu. Hawa wanaongea na mfalme wa nchi kabisa kumbe ana hila. Kuonywa kwenye ndoto sio lazima uambiwe wewe hapana unalala unamuota mchungaji anakwambia usifanye hivyo ndivyo Mungu anaonya. Usitegemee mtu alivaa nguo nyeupe ndio akuonye, ni mtu tu na wala usimfuate huyo mtu yeye alitumiwa tu na Mungu.

Mungu anakupa ndoto ya kuacha ambacho kitakuangamiza na kukupa njia nyingine. Ndoto hii imemuokoa Yesu. Herode alisubiri hawakurudi, mpaka ukapita kama mwaka hivi, Herode akauliza mtaa aliozaliwa Yesu akapiga mahesabu na kupiga mahesabu ya mitaa yote aliyopita mamajusi.

Cha kushangaza huyu ni mfalme na ana jeshi, ila anaogopa katoto. Herode anajua ni wewe tu ndio hujui, Herode anajua ni katoto tu ila kana hatima kubwa.

NDOTO YA YUSUFU NA FAMILIA YAKE KUHUSU KUKIMBILIA MISRI

Mathayo 2:13

“Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.”

Mungu ana heshimu mamlaka ya familia, hutakiwi kumbishia mume wako. Ndiyo maana ni muhimu sana kuolewa na mtu anayejua cha kufanya kwa sababu anaweza kuamua kuondoka kumbe ametokewa na malaika wa upande wa pili, wakikutokea hawa mume anaondoka anahama kanisa, kazi nk. Mariamu alipokuwa mwenyewe malaika alimtokea mwenyewe, ila alipoolewa malaika anamtokea Yusufu, haongei na Mariamu. Ingekuwa malaika wa siku hizi anatokea mama hawana utaratibu.malaika anayeongea na mke ujue sio malaika wa kwenye biblia, ndio inaitwa roho ya yezebeli. Inaongea na mwanamke sio wanaume, mwanamke anakuwa imara kuliko mwanaume. Kama ni mume na mke wakianza kuzungumza na mkeo ukiwa haupo, mmeharibikiwa. Jambo jingina mwanaume kaa karibu na mkeo ili wakimsemesha na wewe uwasemeshe kuwa wamekosea.

Utajiuliza kwani Mungu hana nguvu za kuwalinda?hapana sio adui wote ni lazima upigane nao adui mwingine ni lazima umtoroke.

Ndiyo maana Mungu sio kwamba alishindwa kuwaokoka ila aliona vita ni kali sana, kuna wakati wa kushushwa kwenye kikapu, kupita katikati yao inakuwa hekima ya mwanzi, upepo ukipita inalala chini kisha unarudi. Wakati mwingine mungu anaruhsu upishe upepo sio muda wote ni wa kurudisha ngumi. Mungu akutokee kwenye ndoto ukwepe vita hiyo kwa jina la Yesu.

Sio kwa sababu amesema torokeni basi ndio unaondoka mchana tu ila unatumia njia za kawaida za kutoroka, angalia kuwa makini nyata kisha toka usiku, usiseme kwa sababu  Mungu kasema basi ndio uende tu ukasema ataniokoa.

NDOTO YA YUSUFU NA FAMILIA YAKE KURUDI ISRAELI

Mathayo 2:19-20

“Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.”

Kumbe hakuwepo herode pekee yake wakikuwepo na wengine pia, kumbe baadaye wanaokutafuta baada watatoweshwa na Bwana.

Kuzaliwa kwa Yesu kunaanza na ndoto, mamajusi ndoto, Yusufu ndoto, kurudi ni ndoto, tangu Yesu alipozaliwa zinazoongoza maisha ya Yesu ni ndoto, unakuwa wa ajabu kudharau ndoto. Mungu akupe ndoto ya kukuongoza.

NDOTO YA YUSUFU NA FAMILIA YAKE KWENDA GALILAYA

Mathayo 2:22-23

“Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.”

Hakwenda Bethlehemu alikozaliwa yesu, nisikilize vizuri, Yusufu na Mariamu walikuwa wanakaa Nazareth, lakini Yusufu nyumbani kwao ni Bethlehemu, kaisari akatoa tangazo la sensa, Yusufu ikabidi arudi Bethlehemu, walipofika Yesu akazaliwa hapo ili andiko litimie, ikabidi mfalme wa nchi atoe tangazo akishurutishwa kwa sababu andiko lisitanguke (Bethlehemu u mdogo mika …)

Mungu ikabidi asiongee na Yusufu maana ana maisha mazuri Bethlehemu hivyo ikabidi Mungu atumie kiongozi wa nchi, kumbe kiongozi wa nchi anaweza kuwa hajaokoka ila anaweza kutamka maneno bila yeye kujua. Tangazo linatoka kumbe amevuviwa na Roho.

Sasa walikuwa wanarudi hawakurudi Bethlehemu wala Misri ila wakarudi Nazareth, ndiyo maana Yesu Kristo wa Nazareth. Wayahudi walijua kuwa Kristo atakuja kuzaliwa na atakuja kutuokoa, ila atatokea Bethlehemu. Hivyo Kristo alivyotokea Nazareth ilibidi roho mt awachanganye ili kuleta wokovu.

Wangejua kuwa anatokea Bethlehemu basi wasingemuua, ndiyo maana Yesu akauwawa. Walichanganywa na Bwana, adui zako wachanganywe na Bwana kwa jina la Yesu.

Mungu haihitaji kupiga radi wala tetemeko ila muujiza unaweza kuwa kugeuzwa sura na uonekane sura tofauti iwe ya mfanyabiashara mkubwa. Usitegemee muujiza mkubwa.

NDOTO YA MKEWE PILATO

Mathayo 27:17-19

“Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo? Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda. Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.”

Wakati mwingine watu wanakupangia mabaya, hii ndoto ilitokea baada ya masaa tu ndiyo maana ukiota ndoto mbaya ukiamka irudishe ilikotoka hapohapo, maana hujui ajali itatokea lini, lile tukio haliwezi kukupata kabisa ikiwa utaomba. Usipoomba utakuwa kama yule mwokaji wa mfalme.

NDOTO YA YAKOBO KUHUSU KUBARIKIWA

Mwanzo 28:10-12

“Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.”

Yakobo anakimbizwa na Esau, Isaka amekuwa mzee ana utajiri mwingi, mpaka watu wakamuhusudu, akiwa anataka kufariki akataka kubariki wanawe. Baraka huwa haitoki hivi hivi, unafanya kitu. Baraka lazima uhangaikie, watu wanasema nibariki, nitamkie neno, lazima uhangaikie. Anasema amebarikiwa hajaondoka na mifugo wala ng’ombe ila neno moja tu. Esau alijua hivi si Baraka, ila neno ambalo linaenda na wewe milele.

Watu kwenye ulimwengu wa leo anajua kuwa hizo ndizo Baraka, maneno juu ya Yakobo ndiyo aliyomfanya Yakobo awe juu ya labani, alienda mikono mitupu na akarudi na mali, Yakobo angeenda popote bila mali angerudi na mali. Ukipewa baraka ya Mungu hata kama uende jangwani jangwa litatengeneza maji.

Kama ukinyang’anya vyote mtu mwenye baraka anavyo vyote, baraka ya Mungu hutajirisha ni yale maneno mtu anatamkiwa na mtu wa Mungu. Baraka inapotamkwa kwako inakupa vyote.

Esau Analia kwa uchungu kwa sababu baba yake hakuweza kutamka tena akitamka mara moja afu basi, sasa anamkimbiza Yakobo ili amuue,akihisi labda maneno yatamrudie yeye.

Tunajifunza kwamba maneno yanayotamkwa na mtu wa Mungu juu yako ni ya thamani kweli, una nyumba lakini mgonjwa, una ndoa una amani, ila baraka ya Mungu inaleta vyote. Kuna watu wana hela nyumba lakini hawalali, wana hela lakini hawali vyakula vyote.

Baraka ya Mungu ni yale maneno kutoka kwa mtu wa Mungu, ambayo yanadumu milele yote.

Post a Comment

1 Comments

  1. Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo akubariki Sana Askofu Gwajima. Jumbe zako zimenibariki Sana huku janibu za Magharibi mwa Kenya. Kaunti ya Bungoma. Ningependa nifunzwe kupiga majeshi.

    ReplyDelete