Na Mchungaji Kiongozi Josephat
Gwajima
Kila mtu aliyeokoka ni askari wa
jeshi la Yesu, hivyo kama askari wa Yesu tunatakiwa kufuata kile ambacho Mungu
anatuagiza, 1Timotheo 2:4; sisi ni
wanajeshi wa jeshi la BWANA, Filemoni
1:2; Hivyo mkristo mwenzako aliyeokoka ni askari mwenzako. Ndio maana katika biblia kila mahali Mungu
alipojitambulisha alitumia jina la BWANA wa Majeshi. 1Samwel 15:2; 2Samweli 7:8. Utajiuliza majeshi haya ni yapi; haya
ni majeshi ya Yesu ambayo ndio sisi tuliookoka. Mambo ya Nyakati17:7; Isaya 1:24;3:15; 10:24; 14:13;
Mara tu unapookolewa Yesu ambaye
ni Bwana wa majeshi anatuagiza kutii amri yake. Malaki 3:17; 4:3; Mathayo 28:18-19, hapa BWANA wa majeshi
anatoa Amri ya kuifuata. Kumbe kuwabatiza watu ni amri ya BWANA wa majeshi, hivyo
tuna jukumu la kutii amri ya Yesu Kristo. Na unapookolewa Mungu anakutarajia
utii amri ya mkuu wa majeshi Yesu Kristo.
MAANA YA NENO UBATIZO
Neno “ubatizo” linatokana na neno
la kigiriki linaitwa “babto” au zamisha; hili neno Babto limetumika mara nyingi
sana katika biblia Yohana 13:26. Yesu
alisema ambaye nitachovya naye tonge ndiye atakaye nisaliti” kumbe kuzamisha
tonge katika mboga ndio mana rahisi ya kubatiza yaani chovya au kuzamisha.
Kwahiyo kutokana na maana ya neno ubatizo tunaweza kujua kuwa ili mtu abatizwe
anatakiwa awe kwenye maji tele.
UBATIZO WA KIBIBLIA
Yohana 3:23; kwa maana hiyo ya ubatizo ndio maana tunaona Yohana
alibatiza mahali penye maji tele. Huwezi kuzamisha mtu ndani ya bakuli au
birika, ni lazima maji yawe tele ili mtu aweze kuzama. Hivyo ubatizo wa
kibiblia ni wa kumzamisha mtu ndani ya maji.
Na ndio maana katika kitabu cha Matendo
ya mitume 8:26; hivyo ubatizo wa Kibiblia wote wawili hutelemka majini,
hapo unaweza ukajiuliza je ulipobatizwa wote wawili mlitelemka majini? Kama sivyo
basi ujue haukuwa ubatizo wa Kibiblia.
Na jambo lingine la kuangalia
huyu towashi alihubiriwa, akaamini na kubatizwa. Unaweza ukalinganisha kama
ulipobatizwa uliamini kwanza na je wote mliingia majini, na ndio maana mstari
wa 29” unasema “kisha walipopanda kutoka majini” kumbe ubatizo wa kibiblia
hutelemka majini na kupanda kutoka majini.
KWANINI WATU WANABATIZA NDANI YA BAKULI AU BIRIKA
Watu wengi wanayapindisha
maandiko, lakini biblia inatuagiza kutumia neno la Mungu kwa halali, 2Timotheo 2:15. Na ndio maana utaona
watu leo wanatumia maandiko vibaya kuwabatiza watu katika bakuli, bila
kutelemka majini. Haya ndio maandiko ambayo watu huyatumia kupindisha ukweli, Hesabu 8:5-7; Mungu alimwambia Musa
anyunyize maji ya utakaso, lakini huu si ubatizo bali ni utakaso. Na watu wengi
waliokuwa wamefanyiwa hivi ni wale waliokuwa wameshika maiti, ilikuwa mtu
ashikapo maiti anakuwa najisi mpaka amwagiwe maji ya farakano. Kimsingi huu
haukuwa ubatizo wa kibiblia, bali ulikuwa utakaso tu na si ubatizo wa kibiblia.
MTU YUPI ANAYETAKIWA KUBATIZWA
Huyu ni mtu aliyetubu dhambi,
kama hujatubu dhambi ubatizo wako si wa kibiblia. Matendo ya Mitume 2:37, hivyo kanuni ya Mungu ni kwamba mtu anatubu
kwanza ndipo anabatizwa, lakini maeneo mengi watu hubatizwa wakiwa watoto
wachanga ambao hawawezi kutubu. Hivyo kama ulibatizwa ukiwa mtoto mchanga, huo
sio ubatizo wa kibiblia. Marko 16:15-16,
Na ndio maana Yesu aliagiza kwa kusema aaminiye na kubatizwa, kumbe kinachoanza
ni kuamini alafu unabatizwa.
Tumeona mambo kadhaa yanayoendana
na ubatizo wa kibiblia, yaani unatubu kwanza, ndipo unabatizwa. Matendo ya Mitume 8:12, Biblia
inaendelea kusema kuwa wakaamini wakabatizwa, huwezi kusema umebatizwa kama
hujaamini bado. Matendo ya Mitume
8:35-38, katika biblia hakuna aliyebatizwa bila kuamini kwanza, na ndio
maana Filipo alimwambia Yule towashi kwa habari ya ubatizo “ukiamini
inawezekana” kumbe ubatizo wa kibiblia unaamini kwanza ndipo inawezekana
kubatizwa. Ni swali la kujiuliza kuwa ulipobatizwa uliamini kwanza. Matendo
ya mitume 19:1-…
UBATIZO UNAWEZWA KUFANYWA KWA MTOTO MCHANGA
Mtoto mdogo hawezi kuamini, na
kwa maana hiyo hawezi hata kutubu dhambi zake. Mama au baba wa ubatizo hawezi
kutubu kwa niaba ya mtoto, huu ni usanii na si ukweli kabisa. Mtu anatakiwa asikie
mwenyewe na atubu mwenyewe pasipo kujibiwa na mtu. Kwahiyo jibu la swali hili
kuhusu ubatizo kwa watoto wadogo ni kwamba hakuna ubatizo kwa watoto wadogo,
kwasababu hawezi kuamini, na pia ukimzamisha mtoto katika maji unaweza ukamuua.
Kwa maana hiyo; kama ulibatizwa
ukiwa mtoto mchanga, huo haukuwa ubatizo. Na hata ukiamua kubatizwa ubatizo wa
KIBIBLIA sio kwamba unabatizwa kwa mara ya pili bali ni mara ya kwanza, ule wa
kwanza haukuwa ubatizo. Katika biblia mama au baba awezi kumuaminia mwanaye imeandikwa,Ezekieli 18:20. Kuwa baba hawezi
kuchukua uovu wa mwanaye. Hata hivyo dhambi ya mtoto haihesabiwi kwasababu
akili yake haijaweza kuitambua sheria bado, hivyo dhambi inaweza kuwepo lakini
haijaanza kuhesabiwa kwasababu hawaijui sheria bado.
Kwa asili, mtoto anakuwa
amezaliwa na asili ya dhambi, lakini haihesabiwi, Warumi 5:12-13 kumbe dhambi haisebawi kwa mtoto kwasababu haijui
sheria na wala haijawa wazi kwake. Warumi
4:15. Matendo 2:38; Biblia
inasema kwa siku moja walibatizwa wakiwa na umri tofauti tofauti. Hivyo sio lazima kubatizwa ukiwa na umri kama
wa Yesu bali awe mtu mwenye uwezo wa kuijua sheria.
NANI AKUBATIZE
Katika biblia waliobatizawalikuwa
ni wanafunzi wa Yesu, na si wa musa mfano: Wasabato ni wanafunzi wa Musa na si
wa Yesu. Kama ulibatizwa katika kanisa ambalo si la watu waliookoka maana yake
ulibatizwa na mtu ambaye sio mwanafunzi wa Yesu. Hivyo huo haukuwa ubatizo wa
kibiblia. Ubatizo wa kibiblia hufanywa na mwanafunzi wa Yesu na si vinginevyo.
UWEZEKANO WA KUBATIZWA MARA MBILI AU ZAIDI
Ubatizo wa kibiblia unafanya mara
moja tu, hivyo kama ulishawahi kubatizwa ubatizo wa kibiblia unafanyika mara
moja tu. Lakini kuna mtu alibatizwa kabla ya kuamini, kibiblia hujawahi
kubatizwa na ukibatizwa unakuwa ni mara ya kwanza. Mfano ulibatizwa ukiwa mtoto
mchanga au ulibatizwa na mtu ambaye si mwanafunzi wa Yesu ule haukuwa ubatizo,
lakini ukibatizwa sasa unakuwa umebatizwa kwa mara ya kwanza.
Unapoamiua kubatizwa leo unakuwa
umebatizwa kwa mara ya kwanza kwasababu hakuna ubatizo kwa mtu ambaye alikuwa
hajaokoka bado, hajaamini au alikuwa bado mtoto.
MAANA YA KIROHO YA UBATIZO
Ø Ni
kufa, kuzikwa na kufufuka pamoja na Bwana Yesu Wakolosai 2:12; hivyo katika ubatizo tunazikwa na kufufuliwa pamoja
na Yesu Kristo.
Ø Ni
kutimiza haki yote; Na ndio maana Yesu alikuwa Mungu lakini alipokuja duniani
alikwenda kubatizwa, hakustahiri kubatizwa lakini alibatizwa ili awe kielelezo
kwetu. Ili sisi tumfuate yeye, unapokuwa umebatizwa unakuwa umetimiza haki yote
ila kama hujabatizwa utakuwa hujatimiza haki yote
Ø Ni
ishara ya kumkiri Yesu hadharani. Kuna tofauti kati ya kumwamini na kumkiri
Yesu Yohana 12:41-42. Lakini
unapobatizwa ni kumkiri Yesu kuwa BWANA na mwokozi.
Maswali
Utajiuliza mbona yule mwizi
msalabani alimwamini Yesu akaenda mbinguni bila kubatizwa?. Jambo la kujiuliza
hapa je wewe upo msalabani, na haujapata nafasi ya kubatizwa?, Yule mwizi
hakupata nafasi ya kubatizwa ndio maana alienda mbinguni lakini kwasasa una
nafasi ya kubatizwa unatakiwa ubatizwe kibiblia.
Ukibatizwa lazima ubadilishe jina?
Kimsingi kuna majina ambayo ni
lazima ubadili mfano, tabu, makoye,
sikuzani n.k lakini kama jina lako lina maana nzuri hakuna haja ya kubali jina.
Na ndio maana katika biblia watu wa Mungu wengi walibadilishiwa majina yao.
0 Comments