UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 10.11.2024
ASKOFU BARAKA
THOMAS TEGGE
SOMO: NAMNA HII HAITOKI ILA KWA
KUFUNGA NA KUOMBA
Katika hii dunia kuna matatizo mengi ya kukabiliana nayo, Na matatizo sio ya kuyakimbia ila ni kutafuta namna ya jinsi utakavyo kabiliana nalo. Maisha yako mengi hapa duniani utakuwa unakabiliana na matatizo mengi. Hata Mungu alipokuwa mtu alikutana na changamoto nyingi za maisha kama vile kuzaliwa kwenye holi la ng’ombe.
Kuwa mtu mzima ni kuwa na uwezo wa kuishi na matatizo na
hakuna mtu atakae fahamu kuwa unatatizo na maisha mengine ya kawaida
yanaendelea kama hakuna kitu kimekupata, Watu wanaacha kufanya kile
walichoitiwa kwa kukwepa matatizo.
“Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao
wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.” Warumi 15:1
Baadhi ya matatizo hapa duniani chanzo chake ni viumbe wa kiroho ambao ni mashetani, watu wasio na miili ambao wanaishi kwenye ulimwengu wa giza na ni watu wanaokufahamu kwa karibu kujua taarifa zako. Na ili kutatua matatizo hayo inakubidi uombe ili kushindana nao kwenye ulimwengu wa rohoni.
“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” Luka 10:19
Ni kosa kubwa sana kupuuzia mambo ya kiroho baada ya kuwa
umefanikiwa. Watu wengi wa Mungu wameharibika kwa kuacha kuyafanya mambo ya
Mungu baada ya kufanikiwa laikini watu wa dunia hii huendelea kuyafanya yale
yalio wafanya ili wafanikiwe na kufanya kila masharti wanayopewa kwenye
ulimwengu wa giza.
“Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu
huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa
mioyo yenu yote.” 1Samweli12:20
Maisha ni ya rohoni na mambo yote yanaanzia rohoni
matatizo na suruhisho la matatizo vyote vinapatikana rohoni, Maisha haya usipo
jua kuutumia ulimwengu wa roho hutafanikiwa kutatua matatizo yanayo kupata Itabidi
ujue namna ya kushugurika na viumbe wa kiroho wanao kuletea matatizo.
“Nao
walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, Bwana,
umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi
huanguka motoni, na mara nyingi majini. Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze
kumponya. Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka,
nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku
kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi
hatukuweza kumtoa?Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa
maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia
mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana
kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.” Mathayo 17:14-21
Kila
tatizo la mtu alilolipitia nyuma yake kuna viumbe wa kiroho wanao sababisha
matatizo kwa mtu huyo na zipo njia tofauti tofauti ya kulitatua mengine kwa
kusifu na kuabudu na mengine kwa kufunga na kuomba.
Iko
mamlaka ya rohoni na nguvu ya rohoni ambayo mtu wa Mungu anamamlaka juu ya hiyo
nguvu inayo weza kutatua tatizo ulilo nalo lililo sababishwa na viumbe wa
kiroho.
“Wakafika
ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Na alipokwisha kushuka chomboni, mara
alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake
yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata
kwa minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo,
akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu
aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako
makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. Na alipomwona
Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti kuu,
akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu
usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza,
Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. Akamsihi
sana asiwapeleke nje ya nchi ile. Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la
nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe,
tupate kuwaingia wao. Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia
katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia
baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. Wachungaji wao wakakimbia,
wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.
Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili
zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.” Marko5:1-15
Mashetani
wanauwezo wa kumfanya mtu afanye mambo kwa kuvuviwa akili na mashetani na mambo
hayo sio mazuri machoni pa Mungu na wanadamu kwa akili za kawaida hayawezekani
mtu kuyafanya akiwa na akili zake timamu hata kama hana Mungu, Usipo jua
kushughulika na viumbe wa kiroho utafanya mambo nje ya akili yako kwa kuvuviwa
akili na viumbe wa niroho wapo kwenye
ulimwengu wa giza inakubidi kuomba ili
kuweza kupata akili nzuri
“Ndivyo
utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu”
mithali 3:4
“KWA NAMNA HII HAIWEZEKANI ILA
KWA KUFUNGA NA KUMBA” AMEN
0 Comments