UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 25.01.2026
ASKOFU DKT JOSEPHAT
GWAJIMA
SOMO: FAIDA ZA KUMTUMIKIA MUNGU
![]() |
Biblia inasema:
“Akasema, Basi sasa iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii. Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.” Yoshua 24:23–25
Kumtumikia Mungu hakumaanishi
ibada ya maneno pekee, bali ni kuwatumikia watu kwa vitendo. Kumtumikia Mungu
ni kuwatumikia watu. Mfano, mtu anaomba ili apate nguvu ya kuwaombea wengine.
Mtumishi wa Mungu anaweza kuwa mtumishi wa serikali, mhandisi, daktari, au
mfanyabiashara, ilimradi atumie nafasi yake kuwahudumia watu. Huduma hiyo
humletea thawabu kutoka kwa Mungu.
Zipo faida nyingi za kumtumikia
Mungu. Dunia imejaa watu waliotumia nguvu na nafasi zao kuwatumikia wengine, na
historia yao imehifadhiwa kwa vizazi na vizazi. Mfano mzuri ni Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania, aliyeishi kwa ajili ya
watu. Hadi leo, kumbukumbu yake bado inaishi. Unapoishi kwa ajili ya watu,
unaendelea kuishi katika kumbukumbu zao.
Si kila mtu mwenye maisha magumu
ametenda dhambi. Wapo wanaotamani maisha bora lakini hawajapata fursa. Mtu
aliye katika magumu hastahili kuongezewa mzigo, bali anahitaji kutiwa moyo na
kusaidiwa ili asonge mbele. Mungu humbariki yule anayewainua wengine.
Faida za Kumtumikia Mungu
“Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. ”Kutoka 23:25-26
- Bwana
atabariki chakula chako
Unapomtumikia Mungu, anabariki chakula chako kwa kuondoa mabaya yote yaliyomo ndani yake ili kiwe salama na chenye manufaa kwa afya yako. - Bwana
atabariki maji yako
Mungu huondoa kila tatizo lililomo katika maji unayokunywa na kuyafanya yawe salama kwako - Bwana
atakuondolea magonjwa
Kumtumikia Mungu kunakufanya uishi chini ya ulinzi wake dhidi ya magonjwa. - Hakutakuwa
na kuharibika kwa mimba
Hii inawakilisha mambo unayoanza lakini hushindwa kuyakamilisha. Unapomtumikia Mungu, hataruhusu mtu wala jambo lolote likuzuie, atakupa uwezo wa kuanza na kufika mwisho. - Hakutakuwa
na utasa
Mungu hukupa uwezo wa kuzaa mawazo, biashara, na mipango itakayokuletea ustawi na faida katika maisha yako. Ameweka ndani ya mwanadamu uwezo wa maendeleo.
Unapomtumikia Mungu, atakulinda, atakuongezea miaka ya kuishi, na kukuhifadhi katika hatari na changamoto mbalimbali.
Unapomtumikia Mungu, atakulinda, atakuongezea miaka ya kuishi, na kukuhifadhi katika hatari na changamoto mbalimbali.
Unaweza kumtumikia Mungu huku
ukiendelea na taaluma yako. Kumtumikia Mungu hakuzuii mtu usiendelee kufanya kazi
au fani yako. Biblia inatoa mifano ya watu waliokuwa na taaluma zao, lakini
bado walimtumikia Mungu kwa uaminifu.
1. KORNELIO
Kornelio alikuwa mwanajeshi,
lakini pia alikuwa mtauwa na mchaji wa Mungu.
“Palikuwa na mtu Kaisaria, jina
lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia; mtu mtauwa, mchaji wa
Mungu, yeye na nyumba yake yote…”
Matendo 10:1–5
2. LIDIA
Lidia alikuwa mfanyabiashara wa
rangi za zambarau, lakini pamoja na biashara yake, alikuwa anamcha Mungu.
Hivyo, si lazima kuacha shughuli zako ili umtumikie Mungu, unaweza kufanya kazi
zako huku ukiendelea kumtumikia Mungu kwa uaminifu.
3. SHIFRA na PUA
Vivyo hivyo, wazalisha wa
Waebrania walimtumikia na kumcha Mungu na hawakutii amri ya mfalme wa Misri:
1. DANIELI
Danieli alikuwa kiongozi mkubwa
serikalini, lakini pia alikuwa mtumishi wa Mungu. Alikuwa makamu wa tatu wa
rais, nab ado alimtumikia Mungu.
“Yuko mtu katika ufalme wako,
ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake…” Danieli 5:11
Hitimisho
Siri ya kuwa na nguvu ni
kujizungushia watu wenye nguvu. Mtu dhaifu akijizungushia watu wenye nguvu,
naye huimarika nakuonekana mwenye nguvu. Lakini mtu mwenye nguvu akijizungushia
watu dhaifu, huanza kudhoofika. Akili kubwa kuliko zote ni kukubali kusikiliza
hata wale usiowapenda. Sikiliza watu mbalimbali, kusanya mawazo tofauti, ndipo
utakapokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yenye hekima.
Hekima kubwa kuliko yote ni
kukubali kusikiliza Mawazo ya watu wengine, alafu unachakata yaliyo bora
unayachukua na kuyafanyia kazi. Hii itakusaidia kufanya maamuzi yaliyo bora
zaidi.


0 Comments