Ikiwa ni siku ya ufunguzi wa mkutano wa Ufufuo na Uzima unaondelea katika viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro mkutano huo umeanza kwa maajabu ya namna mbali mbali na ya kushangaza.
Akifungua katika mkutano huo, mchungaji Josephat Gwajima alieleza kuwa Mungu amewaita watu kwa namna tofauti tofauti na anawatumia kadiri apendavyo, akasema yeye ameitwa na Mungu kuwarudisha watu wote waliokufa katika mazingira ya kutatanisha.
Aliendelea kusema kuwa yeye hapingi watu kufa lakini anachokataa ni kusema mtu amekufa wakati amechukuliwa na wachawi na yuko chini ya uvungu wa kitanda cha mtu.
Akasema huu ni wakati wa Bwana kuwarudisha watu wote waliochukuliwa katika mazingira ya kutatanisha na katika mji wa Morogoro ni wakati wa kushuhudia kwa macho yao mambo ambayo Mungu atayatenda kwa kuwarudisha watu waliochukuliwa katika mazingira tata.
Mchungaji aliwahoji baadhi ya watu waliochukuliwa msukule kutoa shuhuda zao, watu hao ni sehemu tu ya watu zaidi ya mia tano waliorudishwa kutoka msukuleni
Wakati mchungaji Gwajima akielezea jinsi dada Nives alivyofufuka kutoka katika wafu, alimuita mdogo wake Nives ambaye anajulikana kwa jina la Dericdady ambae ndie aliyemuombea dada yake wakati amekufa na akafufuka ili awaonyeshe watu namna alivyoomba wakati dada yake amekufa.
Wakati kijana huyo akionyesha jinsi alivyoomba wakati wa kumfufua dada yake ndipo watu mbali mbali waliokua na mapepo walipagawa mapepo jambo ambalo liliwashangaza wengi waliokua wakitegemea kuona mambo kutotokea mpaka mchungaji aombe
Baada ya kuwahoji watu hao Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima alifundisha kuhusu DAMU INENAYO kwa ufupi, alisema ni vizuri kujua kwamba damu inauwezo wa kunena, akitolea mfano damu ya Habili alisema damu ina mambo makubwa matatu
- Damu inanena
- Damu inaponena Mungu anaweza kusikia
- Damu inaweza kulia
Mchungaji Josephat Gwajima hali akiwa amejaa Roho mtakatifu aliwaamuru watu wote waliokua na mashetani kukimbia mbele, hapo ndipo maajabu yalipoanza kutokea na Kuuona uweza mkuu wa Yesu ukijidhihirisha kupitia mchungaji Josephat Gwajima
Alphani Kiloko
alikua ana matatizo ya
kuanguka mara kwa mara na baada ya hapo alikua hajui nini kinachoendelea ,
baada ya maombezi alifunguliwa na kuwekwa huru kabisa kwa jina la Yesu.
|
Sehemu ya umati wa watu waliopita mbele wakati wa maombezi |
Makutano wakiondoka uwanjani mara baada ya mkutano |
0 Comments