Mkutano mkubwa wa Ufufuo na Uzima na mchungaji Josephat Gwajima umehitimishwa kwa tukio la aina yake lililosisimua watu waliohudhuria mkutano huo. Ni tukio la ajabu kutokea ikiwa ni siku moja tu mara baada ya mkutano wa Ufufuo na Uzima kuhamia katika jengo moja maarufu mkoani Tanga.
Pamoja na kufundisha kuhusu misukule, nyota, ndoto na kuhusu wafu; Mchungaji Gwajima alifundisha pia kuhusu majini na jinsi ya kuwashinda ambapo alisema wazi kuwa majini ni viumbe ambavyo ni vya rohoni na vinaweza kuvaa umbele lolote la binadamu au mnyama.
Sehemu ya Umati uliokuwa ukihudhuria mkutano wa Mchungaji Josephat Gwajima jijini Tanga. |
Wakati somo likiendelea kukatokea jambo la ajabu ambalo kwa tafsiri ya rohoni ilikuwa ni uthibitisho wa kile ambacho Mchungaji Gwajima amekuwa akifundisha katika jiji hilo la Tanga.
Mchungaji Gwajima alipokuwa akizunguka katikati ya makutano ili kuwafungua wenye vifungo, zilisikika kelele za watu zikipiga kelel kuwa kuna mtu amevaa ushungi yupo kwenye kona ya bati. jambo ambalo lilivuta hisia za wengi. Kwani mwanamke huyo alionekana na watu wote akiwa kwenye bati la nyumba moja ya ghorofa pembeni mwa jengo la kuabudia.
Ni kweli kuwa kwa ghorofa lile hakuna ambaye angeweza kupanda, wala kukaa kule juu na ukizingatia ni mwanamke. Watu wakiwa wametaharuki na wengine kuliitia jina la Bwana ghafla mwanamke huyo akatoweka mbele ya macho ya watu wote na kuweka hofu miongoni mwa watu wote.
NI NINI TAFSIRI YAKE?
Akiongea jumapili hii kanisani, Mchungaji Gwajima amesema jambo hili ni udhihirisho wa kile alichokuwa anakisema; na ya kwamba yeye alimwona mwanamke huyo kabla watu hawajamuona na kwa kuwa Mungu amekuwa amekuwa akimwonyesha viumbe vingi vya rohoni akahisi kuwa watu hawajamuona. Alisema, "Mungu amekuwa akinionyesha viumbe vingi vya rohoni wakati nahubiri na mara nyingi huwa sitaki kuwatia hofu watu hivyo hukaa kimnya bila kuwambia "
Kumbe ilikuwa ni uthibitisho wa Mungu kuwa viumbe hawa wapo na pia wanaweza kuvaa miili ya binadamu kama vile walaika walivyovaa mwili na kumwendea Ibrahimu na hawa wanavaa miili ili kutekeleza haja zao duniani. Majini ni halisi lakini kwa jina la Yesu wameshindwa kabisa na Tanga imekuja kwa Yesu.
Wakati huohuo eneo jipya la kuabudia la nyumba ya Ufufuo na Uzima - Tanga lipo katika hatua za mwisho za ukarabati ili lianze kutumika shuhudia pichani.
0 Comments