Kwenye biblia shetani
anaitwa mshitaki wa ndugu. Ufunuo 12:10. "Nikasikia
sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu
wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu
zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.".1Petro 1:8
Mahakama nyingi hazifanyi kazi usiku, lakini
mahakama ya mshitaki huyu inafanya kazi saa ishirini na nne, .
Mtu hawezi kufungwa mpaka
kuwepo na mashitaka, kwa kawaida mtu anapokamatwa na polisi huwekwa mahabusu, halafu
polisi huandaa hati ya mashitaka na mtu hupelekwa mahakamani, kwenye mahakama za
juu hati ya mashitaka huandaliwa na mkurugenzi wa mashtaka (DPP). Na hati zinaandaliwa ili mtu afungwe.
Sasa shetani ndiye
mkurugenzi(wa rohoni) wa mashtaka. Zaburi
109:6, ‘Uweke mtu mkorofi juu yake,
Mshitaki asimame mkono wake wa kuume’. kuna washitaki wakorofi.
Mashitaka dhidi ya Yesu, pilato alikuwa mgumu
kushughulikia swala hilo sababu hakukuwa
na hati ya mashtaka. Matendo 25:27 "Kwa maana naona ni neno lisilo maana kumpeleka mfungwa,
bila kuonyesha mashitaka yale aliyoshitakiwa".
Mtu
hawezi kufungwa isipokuwa ameshtakiwa.
Hakuna gereza analoweza
kuingia mtu bila mashitaka. Polisi ni
watekelezaji wa sheria, ukifanya kosa unakamatwa, na ofisi wa DPP inaandaa
mashtaka, hivyo hata katika ulimwengu wa roho kuna idara kabisa ya kuandaa
mashtaka na mtu hawezi kufungwa na magonjwa,umasikini au shida ya namna yoyote mpaka yawepo mashitaka.
Kisa cha kweli
Mwaka juzi shetani alinitokea
na kuniambia kwa kuwa tumeshampiga sana, basi sasa kila mtu achukue nyaraka
zake twende mahakamani, mim nikawaza mahakama gani anayozungumzia..? kama ni ya
Mungu, Mungu ni baba yangu na anakaa ndani yangu.. pia nikagundua unapoenda na
shetani mahakamani lazima uwe makini la sivyo utaweza kuishia jela.
Kolosai
2:3-14 "akiisha kuifuta ile hati
iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu;
akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa
ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo
tena, akaigongomea msalabani;"
Yesu alipokuwa msalabani pia alifuta hati za mashtaka kulingana na
hukumu zake Yesu!
Iko hivi mfano Mungu amesema mshahara wa dhambi ni mauti, sasa
wewe unapotenda dhambi mashetani wanaandika na wanaangalia kwenye sheria za Mungu
wako wanaangalia mfano umezini, wanaenda mbele za Mungu na kushitaki kuwa huyu
amezini na wewe umesema mshahara wa dhambi ni mauti tunaomba tukaitimize hiyo
sheria.
Mungu akikaa kimya wanajua ndo imekubalika, mashambulizi yanaanza. Mungu aliwahi kunionyesha jinsi mashetani
yanavyoshtaki…
Shetani ni mkurugenzi wa
mashtaka, mapepo ni watekelezaji wa hayo mashtaka. Biblia inasema Mungu si mwepesi wa hasira,
ila pia hawezi kumwacha mtenda dhambi bila adhabu.
Yesu alipokuwa duniani aliletewa mwanamke
aliyekuwa akizini, na wakamwambia kwa taratibu za kiyahudi huyu mtu anatakiwa
apondwe mawe hadi kifo. Yesu
hakuwakatalia ila akawaambia ambaye hana dhambi awe wa kwanza kumponda mawe,
wale mafarisayo wakaondoka mmoja mmoja ndipo Yesu akamwambia Yule mwanamke
washtaki wako wako wapi? Kama wameondoka basi na mimi siwezi kukushitaki enenda
kwa amani.
Kwa hiyo kilichomponya yule mwanamke ni wale washitaki wake kuondoka. Washitaki ndio chanzo cha tatizo. Hivyo hata wewe kwa jinsi unavyokuwa na
washitaki wengi ndivyo kwa jinsi hiyo hiyo matatizo makubwa yatakavyokupata, kwasababu
wana tabia ya kuweka kumbukumbu
Kuna idara maalum ya kumbukumbu, ambayo
wanapotaka kukushughulikia wanayachukua na kuyapeleka kwa Mungu! Yaani hiyo ni idara ambayo inasimamiwa na
mapepo maalum wanatunza toka makosa ya mababu zako. Hakuna gereza bila mashitaka.
‘Kwa
jina la Yesu leo napiga watunza kumbukumbu wote, kwa jina la Yesu’
Kuna wengine wamefungwa toka
tumboni kutokana na madhambi ya mababu na mabibi zao! Mfano bibi alikuwa mchawi, wanachofanya
mapepo wanakwenda mbele za Bwana na kutoa mashtaka kuhusu familia
yako. Wanamwambia kwa kuwa bibi yake
alikuwa mchawi na aliwazuia wengi kuolewa na huyu haturuhusu kumzuia kuolewa,
Mungu akinyamaza tayari ndo tiketi ya wao kukuvuruga. Mungu hawezi kukuadhibu ila mashetani ndo
hutunza kumbukumbu na kwenda kukushtaki mbele za Bwana kwa kutumia sheria za
Mungu. Ndio mana inatokea mtu yanampata
mabaya wakati hakutenda kosa lolote
"Kwa
jina la Yesu, nashambulia watunza kumbukumbu wote wanaotunza kumbukumbu za
familia yangu na ukoo wangu"
0 Comments