Naitwa Flora nimezaliwa mwaka 1992 ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Debora
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja. Sikuzaliwa nikiwa mlemavu nimezaliwa nikiwa mzima
kabisa.
Mwaka 1999 nilipo kuwa na umri wa miaka
nane niliumwa mguu mmoja wa kushoto
(niliparalaizi) nilikaa ndani muda mwingi sana bila kupelekwa hospitali kwa sababu wazazi wangu walikua hawana uwezo
wa kifedha wa kunipeleka mimi hosptali, nilikaa ndani zaidi ya miezi mitatu
baada ya kukaa ndani miezi yote hiyo nikaja kupelekwa hosptali.
Lakini kila wakinipima hawaoni ugonjwa unao nisumbua wakati huo mguu wangu umepooza kutoka kwenye nyonga
kwenda chini kama nikitaka kusogeza kitu na sogeza kwa mkono na wakati huo wote
nilipo kuwa kitandani mguu wangu ulikua umeshaanza kuwa mfupi kwahiyo nikisema
nisimame ni vidole tu ndio vinafika chini.
Nikapelekwa hospitali ya KCMC mwaka 2002
nilipo kuwa darasa la pili nikaumwa tena
mguu mwingine wa kulia na ukapooza kutoka kwenye nyonga kwenda chini kwahiyo
miguu yangu yote ikapooza ikawa haifanyi kazi
ilipofika mwaka 2003 na mwaka 2004 nikaanza kuumwa mgongo, mgongo ulikua
umenyooka tu kipindi hicho nilikuwa nasoma nikawa nawambia wenzangu mgongo
unaniuma sana nikapelekwa hospitali lakini ugonjwa haukuonekana nikaanza tu
kutumia dawa lakini hospitalini
nimeambiwa sina ugonjwa wowote unaonisumbua.
Nimekunywa sana madawa lakini hakuna hata dawa iliyo nisaidia
mwaka 2005 nilikuwa na urefu huu huu sikuweza kurefuka tena lakini tulipo kuwa
tunatoka shule tulikutana na matangazo kuhusu mkutano wa injili lakini katika
matangazo yale yakulia yameandikwa maneno tarajia
muujiza wako baada ya kusoma nikawambia wenzangu siku ya mkutano nitakuwa
kama nyie, nikawa na shauku sana moyoni mwangu, siku ya tatu kabla ya mkutano
nikafunga nikamwambia Mungu naomba
uniponye ili nikutumikie maana nikiwa katika hali hii siwezi kukutumikia,
nikamwambia Mungu ukiniponya nitakutumikia nanita tangaza sifa zako milele na
milele.
Ilipofika siku ya mkutano tukaenda na
wenzangu wakaniambia sasa unaenda na magongo au na baiskeli nikawambia twendeni
na baiskeli, mkutano ulikuwa na watu wengi sana sikuweza kusogea sehemu ya
mbele nilikua mbali sana wenzangu wakaniambia sasa itakuwaje utasogeaje pale
mbele nikawaambia msiogope mkono wa Mungu sio mfupi nitapokea hapa hapa nitasimama na nitaacha
magongo.
Ilipofika saa kumi na mbili jioni maombezi
yakaanza, mchungaji wa kwenye mkutano alikuwa anaitwa Michael Elivin alikua
katoka Sweden, maombezi yalipoanza mchungaji akasema kama unaumwa shika sehemu
unayoumwa na mimi nikashika miguu yangu nilipokua nimefumba macho na mchungaji
akiwa anaendelea kuomba ghafla nikaona radi na mwanga mkali umepita machoni
mwangu nikasikia mwili wangu mwepesi nikanyanyuka
hapo ndipo nilipo pokea muujiza wangu.
Kwenye ujana wangu watu wengi walikuwa
wakiniuliza sana sasa Frola utaolewaje? Utabebaje mimba? Utatembeaje?, Mimi
nikawambia nitaolewa kwa sababu Mungu alisema si vyema mtu huyu awe pekee yake.
Na waliponiuliza kuhusu kuzaa nikawambia imeandikwa hapatakuwa na mtu tasa wala
mwenye kuharibu mimba. Katika maombi yangu nikawa namwambia Mungu anipe mume
ambaye anamjua wewe.
Mwaka 2016 Niliota ndoto kipindi nipo mbeya
tupo kwenye kagari kadogo tunaendeshwa
lakini gari kubwa likatuangukia nikaamka
kutoka ndotoni nikajiuliza nini maana ya
hii ndoto ilipofika asubuhi nikawasimulia wenzangu tulioenda nao kufanya huduma
lakini nikawa najiuliza maswali
mengi kwa nini nimeota hivi na hii ndoto inamaana gani lakini nikasema itakuwa
ndoto tu, lakini ningejua nini maana ya ndoto nilioota yasingenikuta yaliyo
nikuta.
Nikaota tena ndoto
tulikua tumelala mimi na mama yangu mlezi na msaidizi wangu wa ndoa
tukiwa tumelala nikaota ndoto hatua kwa
hatua matukio yote ndani ya ndoto, jinsi ilivyo kuwa tulikuwa barabarani
tukapata ajali lakini nilipo amka nikasahau kuomba kabisa juu ya ile ndoto,
tukaenda kanisani tukafunga ndoa.
Lakini moyoni mwangu nilikua sina amani
kabisa yaani nikamwambia mume wangu mbona sina amani moyoni mwangu lakini mume
wangu hakusema chochote zaidi ya kunitia nguvu, tulifunga ndoa ilipofika saa
mbili usiku tulitakiwa kuondoka kutoka
Katesh kwenda Babati, tulipoanza safari yetu usiku ule lakini bado nilikua sina
amani nikamwambia mume wangu tusiondoke usiku huu lakini kuna ndugu ambao waliokuwa
wametufata kwaajili ya kuondoka nao.
Sikuwa na cha kufanya ilinibidi tu niondoke
nao lakini nilikua sina amani kabisa,
safari ilianza usiku ule bado nilikua na hofu sana kabla hata hatujafika mwisho
wa safari yetu tulipata ajali mbaya sana kama nilivyoota kwenye ile ndoto,
ndivyo ilivyotokea maana sisi tulikuwa ndani ya gari ndogo aina ya Noah, ghafla
tuka angukiwa na lori kubwa likaangukia gari yetu tukapelekwa hadi kwenye
mtaro.
Nilipopata ufahamu nikajikuta nimesujudu na
mkono wangu wa kulia umeingia kwenye stering na mkono wangu wa kushoto
nimeulalia, nilipopata ufahamu cha kwanza nikaikumbuka ile ndoto nikasema mbona
kama hiki kitu kimejirudia.Niliomba rehema sana kwa Mungu kwa sababu ya ile
ndoto kwa maana nilijua Mungu alinionyesha lakini sikuomba.
Wakati naomba mume wangu akazinduka kutoka
usingizini akauliza nini kimetokea, nikamwambia mume wangu tulia hapa hatakufa
mtu hapa kwa jina la Yesu. Wakati huo vichwa vyetu mie na mume wangu vilikuwa
karibu karibu kwahiyo akitikisa yeye kichwa ananiumiza na mie.
Wakati tukiendelea kuomba hapo dakika
chache watu wakawa wameshajaa wanafanya process za kutusaidia, lakini tulikaa
zaidi ya masaa sita hatujaokolewa kwa sababu gari yetu ilikuwa imekandamizwa
sana.
Wale watu wa kutusaidia wakaanza kutuokoa
mmoja kwa kutumia shoka, wanakata gari na shoka wakikubahatisha wanakuvuta nje.
Ilipofika saa nane usiku nikamwambia mme wangu kama kuna kinafasi cha kutikisa
mguu, basi tikisa ili watu huko nje wajua kuwa tuko hai. Mme wangu akanambia
hawezi kabisa lakini mimi kwa ujasiri kabisa nikatikisa mguu nikashangaa mguu
umekubali nikaanza kuita Yesu! Yesu!.
Watu wakauona mguu wangu wakashangaa kweli,
hawakuamini kama kutakuwa na watu hai ndani ya gari, wakaleta tena shoka
wakaanza kukata ili kutuokoa, wakamvuta mme wangu wakamwokoa.
Nikawa nimebaki pekee yangu, lakini cha
kushangaza sana sisi tulikuwa tukiomba msaada watu wa nje walikuwa hawatusikii
kabisa lakini wao wakiongea sisi tulikuwa tunawasikia.
Watu wakaendelea na jitihada za kuniokoa na
mimi bahati mbaya sana mpini wa shoka ukavunjika, nilishtuka sana.Baadae
walifata shoka nyingine wakakata gari wakanivuta wakanitoa.
Katika ajali ile walifariki watu saba ndugu
wa mume wangu walikuwa wanne na wengine waliokuwa katika safari moja na sisi,
ajali ile ilikua mbaya ilikua haistahiri mtu kupona kabisa lakini kwa mapenzi
ya Mungu hadi leo tupo hai basi wote tuliokolewa walio kuwa wamekufa walipelekwa
mochwari na sisi majeruhi tulipelekwa hosptali.
Tulipo rudi nyumbani nikajua yote yameisha,
lakini ndugu wa mume wangu walinyanyuka na
kuanza kumsema mume wangu ameoa freemason,
amekuja kwenye familia yetu kuuwa watu,
niliumia sana.
ANGALIA IBAADA NZIMA YA JUMAPILI NA USHUHUDA WA DADA FLORA HAPA👇👇
0 Comments