SOMO: KUFUTA MASHITAKA YAKO
BISHOP DR. JOSEPHAT GWAJIMA
TAREHE: 29.11.2020
Shetani siku
zote ni mshitaki wa ndugu hivyo huangaika usiku na mchana kutafuta namna ya
kutuangusha na kupata mamlaka juu yetu hivyo tunapokuwa tupo dhambini tayari
tunakuwa chini ya mshitaki wetu ambaye ni shetani anakuwa na mamlaka ya
kukufanya mgonjwa,au kufa kabla ya wakati kama vile mwenye shamba muda wowote
autakao hulivuna shamba lake. Lakini tunaporudi nakuomba msamaha mbele za
Mungu, kuoshwa kwa damu yake ndipo tunajiondoa chini ya mshitaki wetu maana
imeandikwa ‘….Na katika torati karibu mambo yote husafishwa kwa damu na pasipo
kumwaga damu hapana ondoleo..’ kwa maana hiyo tayari u msafi kabisa.
Mara nyingi
mahakamani kitu kikubwa ambacho hufanya mtu kushinda kesi ni pale anapokuwa na
mashaidi wengi wenye ushahidi sahihi. Kwenye biblia tunaitwa sisi ni mashaidi
wa Kristo. Ukisoma kitabu cha Waebrania
12:1 Inaelezea zaidi, lakini pia inasema kuwa wamwaminio nao pia wanamashaidi
wengi maana biblia inasema ‘.. tumezungukwa na mashaidi..’ hivyo shitaka lolote
uletewalo hakika yake utashinda.
·
Je!
Na Mungu huitaji mashaidi ?
Unapoamua kwenda rohoni
nakuanza kuomba maana yake unapeleka mashitaka yako kwa hakimu lakini ushaidi
wako ni yale maandiko kwamba ‘hatapatikana pooza wala kuaharibu mimba..’ ,
imeandikwa ‘..hakuna uganga juu ya israeli wala uchawi juu ya nyumba ya
Yakobo…’, ‘utafanywa kuwa kichwa na sio mkia’ tayari umebeba ushaidi wakutosha
kuweza kupewa haki yako kutoka kwa mshitaki.
Mungu huinua watu
kutimiza kusudi maalum, wala si mti au mwamba au bahari ila ni mtu pekee ambae
Mungu humvisha maono na muamko wa kupenya na kupasua milima, miamba mpaka
kusudi litimie. Isaya aliulizwa na Bwana unaona nini? Maana yake lazima kuona kwanza ndipo jambo litimie.
Watu ambao hawajaokoka
husema ‘mwenzetu ametutangulia mbele za haki’ lakini ukienda makaburini utakuta
mwili upo maana yake mtu halisi ambae ni roho ndiye aliyetoka na mwili ndio
uliofukiwa; ni kama vile karanga inavyotolewa kwenye ganda lake na ganda
kutupwa. Maana yake ni kwamba MTU SI
AKILI, SIO MWILI,BALI NI ROHO YENYE NAFSI ILIYO NDANI YA NYUMBA IITWAYO MWILI.
Kila mtu anamashitaka yake mwingine
hana mtoto,ni mgonjwa, au huna kazi kwa kawaida hayo ndio mashitaka yako kwa
maana si vile ikupasavyo kuwa. Katika maisha yako siku zote unapopata jambo au
ukasikia ndani yako wito usigeuke nyuma kusikiliza watu wanasema nini; katika
kufanikiwa lazima upambane vita bila kuogopa maana yoyote apiganaye kwa
kusitasita huwezi kupata au kumiliki chochote. Usiogope kufa kwa maana tayari
tulishakufa na kufufuka pamoja na Kristo. Siku zote unatakiwa kujua kuwa
wanaokutakia mafanikio ni wachache na waliokinyume na wewe ni wengi.Hakuna
kumiliki pasipo kupigana vita.
Kila
mwanadamu ni matokeo ya mjumuiko wa formula mbili ambayo ya kwanza ni
Muunganiko wa mbegu ya mama na baba kutengeneza mwili au nyumba yako ya nje
alafu cha pili ni muunganiko wa roho yaani mtu halisi na nyumba yake ambayo ni
mwili wenye sili ya udongo. Baada yakutungwa mimba miezi tisa ndipo unazaliwa
lakini tu unapoingia duniani wachawi huona kila shehena na hazina au kusudi
lako; sasa hazina hiyo ndiyo nyota ndio maana vita yako huaanza kuanzia ukiwa
mtoto.
Malaki 4:5 – Hapa biblia inaeleza kuwa kizazi cha watoto kupingana
na baba yao ama wazazi kugeuka watoto wao kilihitaji roho ya Eliya lakini pia
inaendelea kusema baadae atakuja mtu ambaye atakuwa na roho ya Eliya ambaye badae
alikuwa ni Yohana Mbatizaji. Hapa biblia inaonyesha kuwa kwa kila jambo yupo
mtu aliendaliwa kwa kwa kusudi maalum hata kama sehemu hiyo kwa akili za
kawaida inaonyesha haiwezekani lakini ndivyo itakwavyo kuwa. Zacharia
alishindwa kuamini yale malaika aliyosema maana tayari walishasoma habari ya
Eliya na ndo maana kusitasita kwake kulipelekea kupata ububu.Haipaswi kusita
pale Mungu anapoinua kusudi juu ya maisha yako, Mungu hapendezwi na watu
wasitao.
Lakini pia
kupitia kuzaliwa kwa Eliya kupitia mwili wa Yohana mbatizaji kunaeleza wazi
kuwa upo uwezekano wakuzaliwa na jambo fulani ndani yako bila wewe kujua au
majirani,ndugu,na marafiki kujua wewe ni nani au kusudi lako ni lipi. Ndio
maana hata Yohana hakujua yeye ni nani maana alimuuliza Yesu ‘…. Je! wewe ni
Eliya au Musa…?’ hii dhahiri ilimfanya Yesu ajue kuwa kwa kawaida si rahisi mtu
kujua asili yake au roho yake ama kusudi lake ndipo alimjibu sawa sawa na
uelewa wake kuwa ‘…vipofu wanaona,viziwi wanasikia,viwete wanatembea, na wafu
wanafufuka!’.
·
1
Wathesalonike 4:16 ‘…. Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka juu pamoja na
mwaliko wa parapanda……’
-Upo uwezekano wa mtu wa
ndani yaani roho kulazwa huku mwili ukiwa unaonekana u mzima kabisa. Na ndio
maana unakuta upo pale pale kila siku bila kujua sababu ni ipi hiyo ina maana
kuwa aliyechukua control ya maisha yako ni roho nyingine si yako tena.
-Kwa kawaida kushindwa
kwingi ndio kufanikiwa kwingi,vikwazo vingi ndio kupenya sana. Usikate tamaa
hata kama pakiwa ni pagumu kupita.Biblia imedhibitisha wazi kuwa wenye kusudi
kubwa ndio waliopigwa vita au kuwekewa kizuizi lakini waliopambana ndio
waliopenya.
-Hivyo inapaswa kumuamsha
mtu wako wa ndani, maana ndio mbeba maono yako,mwili wako upo kwaajili
yakutimiza au kudhihirisha kweye ulimwengu unaoonekana (yaani ulimwengu wa
mwili), amuru kila aliyepandwa ndani yako kuzuia usipige hatua kwenda kwenye
hatima yako. Futa kila mashitak yaliyowekwa mbele yako ili usiwe mwenye haki wa
kumiliki hazina zako.
Ukiwa na
kitu ndani yako huwezi kujua kuwa unakitu mpaka utakapochukua hatua.
BONYEZA HAPA👇👇 KUANGALIA IBAADA NZIMA YA LEO JUMAPILI
0 Comments