google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTU NA WAKATI WAKE WA VITA


Bishop Dr. Josephat Gwajima
Somo: Mtu na wakati wake wa vita
Jumapili, 20.12.2020


Watu tunajifunza neno la Mungu kwasababu kiroho tunafanana na simu kwamba lazima simu ichajiwe ili ifanye kazi vizuri  vivyo hivyo na sisi neno hutujaza kiroho ili kuwa sawa zaidi.
-Vita ya mtu hufanana na hatima yake yaani ‘HATIMA KUBWA HULETA VITA KUBWA NA HATIMA NDOGO HULETA VITA YA KAWAIDA’

Ayubu 7:1
Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi?
Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa?

-Siku zote Taifa la Israeli liliandamwa na vita siku zote kwanzia kwa Farao Misri kwasababu tayari ilipaswa azaliwe Kristo kwaajili ya kutuokoa.
-Angalia kwenye familia zetu au hata kwenye historia kawaida mtoto mwenye matatizo mengi ndiye mwenye kubeba maono au hatima kubwa. Unakuta mtoto ni mgonjwa,mkorofi,alikataliwa,alizaliwa kwa tabu,hana akili darasani,amedharauliwa na familia baadae huibuka kuinua familia zao  Mfano; Mfalme Daudi ,Paulo,Rahabu (Bibi yake Yesu),Ruth, Musa n.k

-Mungu huruhusu ukae jangwani kwaajili ya kukutengeneza ili ijapoinuka vita njiani uikabili. Matatizo yapo kukunoa na kanuni ya kunolewa lazima vipande vitoke kwahiyo usiumie sana pale unapoona baadhi ya mambo hayako sawa ni kunolewa kwenyewe huko.
-Ulipozaliwa kwanzia wazazi ,eneo, na sifa ya kabila ina changia kwa sehemu kubwa wewe kuwa nani baadae (HATIMA). Usingepitia yale uliopitia usingefika hapo ulipo mshukuru Mungu. Mfano hai ni Raisi wa Kwanza wa South Africa, Nelson Mandela alizaliwa akiwa mtoto mtundu sana kwenye familia yao baadae akaingia jela lakini yote hayo ni kumuandaa kuwa Raisi wa kwanza mweusi ambae aliwafukuza makabulu na kuweka historia kubwa duniani kote.

Ndio maana watu weusi wanapigwa vita na wazungu kwasababu ya Hatima yetu, ukifuatilia historia Raisi wa kwanza duniani alikuwa ni mtu mweusi anaitwa Nimrod. Sasa hofu yakutawaliwa tena na watu weusi ndio huwafanya kutupiga vita kwa njia yoyote ile ili isitokee.

Yeremia 13 : 23
Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoa-doa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya.
-Sasa shetani anajaribu kukufanya sifa ulizowekewa ili ufike kwenye hatima yako ziharibike. Mfano, Msichana anakuwa ni mwenye dharau kiburi,hasira kiasi ambacho hata mchumba aliyepangiwa anamkataa, au unakuwa shule unafeli kila kidato matokeo yako ni mabaya kiasi ambacho kazi hupati itakayo kuvusha kuanza biashara yako uliopanga.

Kazana katika maombi ili kuweza kufanya kusudi la Bwana kwenye maisha yako litimie. Nena kwa lugha muda wa kutosha, hudhuria ibada ili kuji-charge kwaajili ya kazi iliyopo mbele yako. Hakika yake hatima yako haitapindishwa na mtu yoyote mpaka itimie.



BONYEZA HAPA👇👇 KUANGALIA IBAADA NZIMA YA LEO JUMAPILI



Post a Comment

1 Comments