Bishop
Dr. Josephat Gwajima
Somo: NAMNA
YA KUFIKIA HATIMA YAKO
Alhamisi, 03.12.2020
Katika ulimwengu huu kuna viumbe vya aina mbili,
visivyoonekana na vinavyoonekana. Kwahiyo sio kwasababu kitu hukioni basi
hakipo, ni kama upepo unapovuma na miti kuyumba haoni upepo ila ni matokeo ya
upepo. Hivyo ndivyo viumbe vya rohoni vilivyo yaani majini, mapepo, mawakala
wote wa shetani walivyo, hawaonekani ila matokeo yao ndio huonekana na ndo
maana unakuta mtu anapagawa mapepo au anakuwa mgonjwa. Kwahiyo ule uwezo wa wao
kuona utakuwa nani baadae ndio sababu huinua vita dhidi yako bila wewe kujua
kwasababu huwaoni. Tayari kwenye ulimwengu wa roho viashiria vya hatima yako
huonekana na mbinguni Mungu na malaika anatengeneza njia ya wewe kufika na
wakati huohuo shetani na kamati yake wanapambana usifike.
· Warumi 8:30- ‘Na wale aliowachagua tangu asili..’ maana yake tayari tunaasili zetu tokea mbinguni kwa maana Mungu anasema ‘Maana mawazo ninayo wawazia ninyi si mabaya..’ kwahiyo anakua ameandaa mengi mazuri lakini unapokuja duniani shetani anaingia hapo kati kukuzuia
Luka 21:22 ‘Kwakuwa siku hizo ndizo za mapatilizo,ili yatimizwe yote yaliondikwa’ pia Luka 18:31’….na mambo yote yatatimizwa,Mwana wa
adamu aliyoandikiwa na manabii’ maana yake lipo jambo ambalo kila mmoja
ameandikiwa litimie.
Lakini haimaanishi kwamba
umeandikiwa hayo basi unakaa na kusubiri yatimie au nabii akatabiri ukaamini bila
kuweke jitihada zozote ukisoma Luka 18:31.
Nabii anapokuwa anatoa unabii anazungumza ambayo Mungu amemfungulia rohoni
kuhusu wewe kwahiyo anapokuambia ni jukumuu lako kuyachukua na kutendea kazi.
Ukisoma kitabu cha Isaya 11:1 na Isaya 7:1 hapo Nabii
Isaya alikuwa akionyeshwa kuwa miaka ijayo Yesu atazaliwa, sasa vilevile na
wachawi wanaona kuwa miaka ijayo yupo mtu atazaliwa ambaye ataharibu kazi zao.
Na ndio maana unakuta waombaji wengi walipokuwa wadogo walikumbana na
changamoto hatari sana au hata akiwa anakua alipitia misukosuko mingi mno Mfano, anazaliwa kabla ya wakati, anakuwa
mgonjwa kwa muda mrefu au hata kukataliwa na wazazi wake.
· Isaya
9:6- Isaya anaeleza unabii kwa kutumia wakati timilifu akisema, ‘Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanaume;na
uweza wa kifalme utakuwa begani mwake…’
maana yake kwenye ulimwengu wa roho tayari yaliyoandikwa kuhusu Yesu yalikuwa yameshatimia bado tu kudhihirika
ndivyo hivyo na hatima zetu zilivyo kwa bidii ya kuomba ni wakati tu kuyaona. Lakini
wazuiaji wapo kama vile wana wa Israeli walivyokuwa wamepata Musa wakuwatoa
Misri ila akainuka Farao na kuufanya muujiza wao kuwa mgumu kutimia ila kwa
mkono wa Mungu wakashinda. Kumbe basi siri ya kudhihirika kwa hatima zetu ni
kuomba kwa bidii bila kukoma.
BONYEZA HAPA👇👇 KUANGALIA IBAADA NZIMA YA LEO ALHAMISI
0 Comments