Bishop Dr. Josephat Gwajima
SOMO: TUMEFICHWA NA KRISTO (HATUONEKANI)
Ijumaa, 04.12.2020
Wakolosai
3:1-3 ‘….kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo
katika Mungu..’. Kuna mambo mawili
ambayo inabidi kujifunza ambayo ni ‘kwa maana mlikufa’ na ‘uhai
wenu umefichwa’.
Silaha
kubwa ya kivita ni kumuona adui hata kama unasilaha kubwa kuliko mwingine.Ukisoma
Wagalatia 2:20 ‘Nimesulubiwa pamoja na Kristo;
lakini ni hai; wala si mimi tena, bali
Kristo yu hai ndani yangu….’
Maana yake sisi tulikufa tayari na hatumo/hatuonekani maana tumefichwa na
Kristo.
Wachawi
wanapoenda nyumbani mwa mtu lazima wakuone na hawaishii kukuona tu ulivyo
mwilini bali hatima yako yaani utakuwa nani, utaoa au kuolewa na nani, nani
atakaezaliwa kupitia tumbo lako? kwahiyo mashetani ndio husema tu mchukue huyu
mtu. Lakini tofauti ya mtu aliyeokoka na asiyeokoka nikuwa mashetani hawawezi
kukuona kama umeokoka kwa maana umefichwa pamoja na Kristo. Unapookoka na
kumpokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako tayari unakuwa umefichwa
na Kristo.
· Always
remember “So as to succeed in any sphere of life you need to import
spiritual facts from the bible in your life and live accordingly”; you can also refer in the Book of Galatians
2:20.
Ezra
10:14 ‘Inuka; maanca shughuli hii
inakuhusu wewe; na sisi tu pamoja
nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitenda.’ Usiache kuomba na ujue siku zote
shetani hawezi kukuuwa bali anauwezo wa kukujaza hofu ambayo itakusababishia
mauti. Mungu ni neno kwaiyo kumshambulia Shetani tumia andiko lolote kwa maana
ndio silaha yetu ya vita. Vaa ujasiri wa kumkabili shetani kwa maana ushindi
tunao tayari.
Nena
kwa lugha muda wa kutosha na usome maandiko kwa maana ndio njia ya kupambana na
adui shetani kwa yoyote aliyeokoka. Na ndo maana ukilala ukiwa umeachia andiko
‘Mimi ni mwali ya moto’ au ‘Mimi ni chumvi ya ulimwengu’ pia ‘Mimi ni rungu na
silaha za Bwana za vita’ ndivyo adui akuonavyo na ndio maana tunasema HATUONEKANI
kwa maana tumefichwa na juu yake
tumepewa mamlaka ya kutamka na ikawa.
Shetani
hufanya wakristo wengi waliokoka kujiona wakawaida ili aweze kuzuia kusudi la
Mungu lakini wewe ambao tayari Mungu amekufunulia haya kazana kunena kwa lugha.
Kuna mambo ambayo ukiwa unaomba Mungu anatengeneza connection kwenye ulimwengu
wa roho.
Lakini wakati wote inabidi kuchunga mambo
matatu (3);
1. Chunga cha kuangalia
-Shetani hutumia kile ulichokitazama kuharibu nafsi yako.
2. Kataa kusikiliza
baadhi ya vitu
-Vitu unavyosikia husababisha uwepo wa Bwana kutoweka.
3. Kataa kwenda mahali
ambapo roho wa Bwana hakuruhusu
-Kama mbegu isivyoweza
kumea kwa baadhi ya eneo ndivyo na roho zetu zilivyo.
0 Comments