Bishop
Dr. Josephat Gwajima
Somo:
TUPO VITANI
Jumatano,
02.12.2020
Hatima za watu hazipimwi na binadamu bali Mungu
mwenyewe tayari ameshapanga na kukufahamu. Lakini shetani pia anaouwezo wakufahamu
umebeba nini au utakuwa nani ndio maana kuna vita ya rohoni. Tayari Mungu
amepanga kuwa utakuwa nani na utafanya nini, sasa kuna watu ambao wamesheheni au
wamebeba vitu vingi hivyo hata vita yao inakuwa kuwa kubwa zaidi.
Mfano, Daudi alikuwa amesheheni vitu vingi ndo
maana vita yake ilikuwa kubwa. Kwanza hakuwa mtoto anaethaminiwa na familia
yake,ila pia baada ya kumpiga Goliathi bado aliibua vita na Sauli.
Uwezo wa kushinda vita yako au kuvipita vikwazo
vyako ndio uwezo wako wakumiliki. Maombi ndio njia kubwa yakufungua shehena
zako kwahiyo juhudi yako katika maombi
· Luka 3:21 -Huu mstari unaonyesha
tofauti ya Yesu Kristo na watu wengine waliobatizwa. Baada tu ya Yesu kubatizwa
alianza kuomba na mbingu ikafunguka lakini wengine wote walibatizwa lakini
mbingu hazijafunguka kwasababu hawakuomba.
Upo uwezekano wa mtu kufa kabla ya yale ambayo
ameyabeba hayajatimia kama hutotia bidii. Kuna watu wanahatima kubwa ila
wanaweka hofu ambayo huzuia kutimia kwa kusudi lao.
· Yohana 21:17-Hapo Petro anaaambiwa
atakuwa mzee lakini baadae Petro akaja kukamatwa kabla hajawa Mzee.Ukisoma
Matendo12:1…unaeleza namna Petro alivyotaka kuuwawa kabla hata hajaandika
kitabu cha Petro.Hapo tunajifunza wapo watu wanaweza kufanya hatima yako
isitimie;lakini baada tu ya wale wanafunzi kuamua kuomba kwa bidii malaika
akamtokea Petro gerezani na kumtoa nje.
Ni vyema kujifunza kuomba kwa bidii bila kukoma
ukiwa umepata au umekosa kwa maana maombi hukaa akiba, maombi ambayo unaomba
leo yanaweza kubadilisha maisha yako baada ya miaka mitano ukiwa hukumbuki kabisa
ama huna nguvu za kuomba. ‘Kuomba kwake
mwenye haki kwa faa akiomba kwa bidii..’ kazana kuomba kwa bidii sana.
Kufanikiwa katika maisha sio kuwa na utajiri bali
kutimiza wito wako ulioitiwa duniani. Lile jambo linalokusukuma kila mara
ufanye au linakukereketa kulitimiza ndio kusudi lako.
· Matendo 9:19 – Hapa Paulo
anaonyeshwa baada ya kuokoka alitafutwa kuuwawa ila huku aliahidiwa kuhubiri
kwa mataifa mbele za wafalme lakini pia wakati huo hakuwa ameandika kitabu hata
kimoja kwenye
· 2Wakorintho 11:31-33 anaeleza jinsi watu
walivyoandamana kumuua hata ikabidi kushuka kwa kikapu.Ila kusimama na Mungu
ndio kilichomwinua Paulo mpaka hatima yake au kusudi lake la kuhubiri,kuandika
vitabu sawa sawa na neno la Bwana.
Kuna watu wanatumwa kukuharibia anaweza kuwa rafiki,
mume/mke,jirani au hata wazazi ama ndugu.
Matendo
14:19 –Hapo mstari unaelezea jinsi Paulo alivyopigwa na
watu ambao walipanga kumuua hata kabla neno la Mungu halijatimia au kusudi lake
halijadhihirika. Unapoamua kufunga na kuomba unaharibu kila mipango ya adui
zako na kukusaidia kufungua njia yako na kupita katikati yao.
0 Comments