UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL.
IBADA YA JUMAPILI 11TH JUNE 2023.
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE.
SOMO: KUBATILISHA MASHAURI YA GIZA.
“Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku. Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye Hodari”. Ayubu 5:12-15
“Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande. Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi”. Isaya 8:9-10
Mwanamke hata kama mayai yameisha hawezi kuzaa ila wa rohoni akisema utazaa unazaa kweli. Sara alikuwa amekoma kwa desturi ya wanawake ila wa rohoni alisema akazaa, unaweza mambo yote katika yeye akutiaye nguvu. Kwa neno la Bwana yote yanawezekana. Bwana akisema ukaamini itakuwa hivyo hivyo imani yako itafanya yasiyowezekana yakawezekana. Mungu akisema jambo halina mantiki ila ukiamini yanawezekana. Mungu anamwambia Yoshua zungukeni ukuta mara saba hahitaji kugusa ukuta zungukeni pembeni na ikafika siku ya saba hakuna ufa wala nini ila walimuamini Mungu, alisema utaanguka na ukaanguka. Japokuwa sayansi inasema ukuta ili ubomoke unahitaji kulipuliwa, neno la Bwana likamjia Elisha akawaambia chimbeni mahandaki hakuna mvua wala wingu wala dalili yoyote ila mahandaki yakajaa maji, ukiamini neno la Mungu utafanikiwa hata kama hujasoma sana, mpenzi nakuombea ufanikiwe na kuwa na afya njema kama roho yako ifanikiwavyo baada ya hapo biashara ndoa zitafanikiwa sisi ni watu ambao hatutembei na kanuni za sayansi. Yeye aliyetoka juu yupo juu ya yote hata kama hali ni mbaya uchumi ni mbaya hata kama dunia ikiharibika wewe ni wajuu na aliye juu yu juu ya yote amekuweka hujajiweka.
Ukiendelea kuamini sayansi huwezi kufanikiwa kwa sababu sayansi inasema wa aina yako hawezi kufanikiwa ila ukiamini kwake yeye aminiye yote yanawezekana. Hakuna dalili hatutembei kwa dalili kama amesema itanyeshe itanyesha kweli. Miaka mitatu kulikuwa na njaa akamtuma Eliya nenda kajionyeshe maana nitaleta mvua hata kama hakuna dalili neno la Bwana limenena itatokea. Mungu anaweza akaongea na ikawa hakuna dalili na ikatokea, ukiamini utapokea sawasawa na imani yako, Mtumishi wa Eliya alimwambia kuna dalili ya wingu kama kiganja , akasema hiyo hiyo ni mvua kubwa na ikanyesha, Paulo akamkuta kiwete ajatembea toka yupo tumboni mwa mama yake lakini Paulo akaona ana imani ya kutembea akasema simama uende, saa ile ile akasimama akaenda, hata wewe hata kama kuna dalili za kuachia au kufilisika au kufa kama una imani hautakufa, hautafilisika, hautachika.Wenyeji wetu ni wa mbinguni na wanatumia imani huyanena yasiyo kuwako kama kwamba yameishatokea ongea mambo ya mafanikio ya biashara, ya ndoa ambayo hayako kuwa yako hiyo ndio imani. Biblia inasema nayaweza mambo yoye katika yeye anitiaye nguvu nitatenda mambo makuu maana msaada wangu ukatika Bwana. Yeye halali ananilinda mchana na usiku chini ya mbawa zake nitapata kimbilio, ulimwengu usioonekana unaupata access kwa imani unaugusa kwa imani vile unasema kwa jina la Yesu nawafuata.
Usiwaze kinyume kuwa ukisema haitatokea usiseme kinyume, usiseme ndugu zangu hawatanisaidia wakijua ninamuamni Mungu, msaada wako upo kwa Mungu, ukisema neno litatimia, mtu yeyote anaweza kuamini, kuna mambo hayaeleweki yanahitaji imani. Hakuna formula iliyosema pakavu paonekane zaidi ile ile formula ya imani. Tutaingia ulimwengu wa roho tutaomba tutavunja sema kwa msaada wa Bwana naruka ukuta na hapo unaongea hakuna dalili na imani inanoga pale panapokuwa hakuna imani. Jisemee mwenyewe majira kama haya mwakani nitakuwa mke wa mtu na unaanza mafunzo ya kupika chapati mnyumbuliko kwa ajili ya mumeo hapo unakuta hauna mchumba ila unakuwa na imani unafanya mipango kwenye ulimwengu usioonekana. Mungu akiwa na vita anakutumia wewe maana wewe ni rungu la Bwana la vita.
Ayubu 5 inasema yeye huyatambua mashauri ya wadanganyifu mikono yao isipate kutimiza maovu yao, kwa mkono wa Paulo na Musa na Haruni Bwana akatenda, wewe pia una mkono na shetani ana mikono wale watu wanaotumiwa na shetani kukuumiza leo ni mkono wa shetani huo. Maana wana mipango ukiolewa usizae lakini leo tunaenda vitani maana Bwana huyatangua mashauri yao yasipate nafasi, ukiomba usimuangali mtu mchawi yeye kama yeye muone wa nyuma yake , maandiko yanasema shetani aliporuhusiwa kunyoosha mkono kwa Ayubu ili amtende mabaya, alitumia mikono ya Waamaleki, Waseba , kuna matukio kwenye ulimwengu wa mwilini ni matokeo ya ulimwengu wa roho, unaweza mchukia mtu kumbe yeye ni silaha tu anatumika sio yeye, unakuta mbibi anakupiga vita usiolewe na yeye hapo ana hadi vitukuu , sio yeye huyo bali anatumiwa kama silaha ya shetani, leo ni vita tu hapa nikupigana tu hata maombi ya kubariki chakula ni maombi ya vita. Omba kwa kusema tunageuza chakula kiwe chakula hasa naondoa mauti kwa jina la Yesu, maana imeandikwa wana wa manabii wakamwambia Elisha imo mauti ndani ya sufuriani. Ulimwengu usioonekana unaandaa matukio kwa ulimwengu wa mwili.
Mashauri yanapangwa ukiyaendelea kimasihara utaumia, vita inatengenezwa wakati wa amani wasemapo kuna amani ndipo vita hutoke, usisubiri vita ianze anza kuomba mapema kuizuia, wafuatae kwenye uwanja wao wafuate kule kule walipo kwenye mashimo yao kwa msaada wa Bwana tunalifatia jeshi, wakati ndoa ina amani, mnapendana, namvaa sare, mnapeana maneno mazuri mazuri ,kuwa leo bila yeye huwezi kuisha, unafunguliwa mlango wa gari, ndio mipango ya kuachana inapangwa. Wasemapo kuwa ni amani kwenye ulimwengu wa roho shetani anapanga mipango baada ya muda unaitwa mbwa. Mipango yao na mashauri yao tuyaendee kabla ya mikono yao kupata nguvu.
Yesu anauona mji analia wakati kule kuna amani furaha luka 19 wakati watu wanamshangilia yeye anaulilia mji, kwakuwa walikuwa na furaha kwakuwa macho yao yamefungwa hawaoni ila Yesu aliona mika 40 ijayo juu ya huo mjini. Baada ya Yesu kusema hayo maneno ilipita miaka 40, kipindi cha 70AD warumi wakaingia wakawachinja watu. Hata watu wa Mungu hujisahau sana wakati wa amani kuwa ndipo vita inapangwa. Wakati kuna farasi wa kijivu wanamsahau, ulimwengu wa roho ukipanga matukio wanaweka ni wapi yatokee na muda haijalishi ni muda gani, ndio anasema farasi wa kijivu na amepandwa na mtu anaitwa mauti anakuja kuharibu biashara, kazi, ndoa, kabla hujaolewa ulikuwa muombaji mzuri ila ulivyoolewa ukaanza kutokuhudhuria kanisani ghafla uharibu unatokea, ukiona mtu ana haribikiwa uujue mishauri yao yametoka kwenye upangaji yanaingia kwenye utekelezaji.
“Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana. Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai. Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari. Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao. Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi. Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema. Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile Esta 3:5-11,14
Huyu ni mtu ana ugomvi na mtu mmoja tu, huyo Hamani ana ugomvi na Mordekai tu lakini anatangaza vita ya kufuta watu wote, watu wengi hudhani hivi kwa kuwa hana ugomvi na watu wengi basi hatakuwa na vita. Puri ni ni mambo ya uganga inayopigwa kuangalia ili kutekeleza majukumu kwakuteuliwa tarehe nzuri yakutekeleza jambo Fulani.
Mfalme akamuelewa na kumpa na fedha ili akatekeleze mambo aliyosema, kikawaida ipo kabla mtu hajahukumiwa anahaki ya kusikilizwa na hakuna mtu anaweza kuwa mwamuzi kwenye kesi yake mwenyewe, Hamani anafahamu hayo yote ila alichofanya ili kupindisha alianzia rohoni kupika puri hoja yake ikatendewa kazi maana kuna mashetani yalimvuvia mfalme, hata wewe inaweza kutokea ofisini kwako ghafla tu ukashangaa unafukuzwa kazi kwa kosa dogo hii ni mambo ya ulimwengu wa roho iliishapangwa, watu walioachika ukiwauliza ilivyoanza mpaka kufika kuachika nisababu isiyo na maana kabisa. Hoja ambayo haina mashiko mfalme amekubali na pesa ametoa kumbe kuna mpango wa rohoni umepangwa. Kuna wakati wanandoa wanakuja kwangu wakiwa na matatizo ya ndoa ukimsikiliza unakuta ni mambo ya kawaida kabisa, ni ukweli huwezi kukwepa majibizano kwenye ndoa basi usioe kaa tulia mtumikie Mungu kama hutaki majibizano, kugombana kununiana. Unaweza kusema unataka kuoa binti mdogo atakayekuheshimu ila ukweli ni kwamba hata yeye atakuchanganya sana maana mambo hayo ni kawaida kwenye mahusiano haijalishi kuwa wewe ni mchungaji.
Esta akawambia wayahudi wafunge kwa sababu aliyesaini ni mume wake na hakuna maneno ya kimapenzi yangeweza kusaidia, akawambia waombe maana mpango uliaanzia rohoni. Huwezi kushinda mpango wa rohoni kwa harakati za mwilini. Tutaomba mipango yao iwarudie wao wenyewe ,ndoa yako kuvunjika ilianzia rohoni na sisi tuanzie rohoni, maana kila silaha itakayoinuka juu yako haitafanikiwa , niwewe unatakiwa ubatilishe kila mipango iliyopangwa juu yako na mpango ulipangwa mwei wanne na unatakiwa utokee mwezi wa 12, kuna ndoa kuna biashara zinaonekana ziko salama ni kwakuwa wapo kwenye mipango, omba kila mipango yao iharibike wafunge mikono ya isipate maana huwafunga wafalme wao mikono yao, mkono wa shetani usiucheze maana siku moja aliyekuwa na kondoo,mbuzi ,ngamia na watoto walipotea wote, unayaweza mambo yote katika yeye akutiaye nguvu. Umepewa mamlaka na hekima unayo ya kuwashinda adui zako. AMEN
0 Comments