UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL.
IBADA YA JUMAPILI 4TH JUNE
2023
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE.
SOMO: KUGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.
Vile ulivyo unaweza ukawa mtu mwingine,
Mungu anapokuwa na shughuli na mtu anamkuta mtu akiwa na maisha anaona ndio
yakwake kama vile amefika ila Mungu ana jambo kubwa vile ujawahi kuwaza, Mungu ana
mawazo makubwa sana na anapotaka kuyatimiza hayo mawazo kupitia wewe ana desturi
yakumgeuza huyu mtu na kuwa mtu yule amtakaye.
“Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani
pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake
Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha
hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi
wake. Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na
kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda
hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri
habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya
mwanangu? Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa
Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko
Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate
mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; nao watakusalimu na
kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. Baada ya hayo
utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa,
utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa
juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa
wakitabiri; na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja
nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine. Basi, hapo ishara hizi
zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.
Nawe utatelemka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko,
ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba
utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya. Ikawa,
alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu akambadilisha moyo; nazo ishara zile zote
zikatukia siku ile ile. Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii
wakakutana naye; kisha roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu, naye akatabiri kati
yao. Ikawa, wote waliomjua zamani walipoliona jambo hilo, kwamba,
tazama, huyo anatabiri pamoja na manabii, ndipo watu wakasemezana, Ni nini hilo
lililompata mwana wa Kishi? Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii”.1Samweli10:1-11
Hii ni Habari ambayo unaifahamu, habari
ya kijana mmoja wa familia ya Benjamini alikuwa anachunga na kufuga mifugo na
baba yake mzee Kishi, anakaa sehemu ambayo ni ukoo wa watu wa maskini wakawaida
kabila dogo la Benjamini. Kwa hiyo huyu kijana wa kabila dogo kuna mambo hufanya
watu wakaheshimika na kudhaniwa wanaweza kufanya mambo makubwa kwasababu ya
kabila ambalo ametoka, hata hapa kwetu ukisema kabila lako watu wanaweza
kubashiri unaweza kufanya mambo gani. Ukisema kabila lako wataweza kusema
unafaa kucheza ngoma au mchawi au unaweza kufanya biashara ukisema tu kabila.
Kijana huyu alipoteza punda na kuanza kuwatafuta
punda wa mzee Kishi sehemu mbalimbali wakafika mahali wakaamua waache kutafuta
punda warudi nyumbani lakini mtumishi wa mzee Kishi aliyekuwa na Sauli
akamwambia mji huu kuna mtumishi wa Mungu ambaye akisema neno huwa linatokea
tumuende yeye. Wakaenda wakafika kwa Samweli, Samweli alipomuona Sauli,
maandiko yanasema Mungu akamwambia huyu ndiye niliyekuambia mpake mafuta, maana
siku moja kabla Mungu aliishamfunulia Samweli kuwa atamletea mtu ampaka mafuta
ili awe mfalme wa Israel, Sauli alizania anaenda kutafuta mambo ya kimwili
lakini amekutana na mtu wa Mungu ana jambo la mbinguni nakuanzia pale akabadilika
akaacha kuwa mchunga punda na kuanza kutumikia kusudi la maisha yake.
Umekuja mahali hapa ili uaambiwe maneno
ambayo kabila lako hawafanyagi maana utageuzwa nakuwa mtu mwingine, unaweza
kusema nilikuja hapa nimelogwa, nimepoteza hata Sauli anadhania ni punda kumbe
hata Mungu anaweza kubadilisha ili upate cha thamani zaidi, Mungu anaweza
kufanya upoteze ndoa, masomo ili ukutane na mtu wa hatima yako.
Mungu huwa anapeleka watu kwa mtu,
akitaka akubadilishe hakutokei wewe maana hutamuelewa, maisha ya watu yanabadilika
wanapokutana na watu wengine wenye maelekezo ya Mungu kwa habari ya hatima yako
nasio kila mtu.
Hata wewe umeletwa na Bwana, maana
anataka akugeuze uwe mtu mwingine kabisa. Samweli akaambiwa ampake mafuta sauli
na Roho wa Mungu akamjilia yeye kwa nguvu, kazi ya Samweli ilikuwa ni kumbaini
ni nani tu na kumpaka mafuta, mengine Mungu atamaliza.
Kuna mambo watu wanayatamani ila wewe
umewekewa biashaara ambayo watu wanaitamani, umewekewa ndoa ambayo watu
wanaitamni umewekewa kazi ambayo watu wanaitamani. Unaweza sema mimi kabila langu
mbona halina mambo hayo, hata kama ni kabila dogo maana kabila lako halina
chakufanya na hatima yako maana yupo Mungu ameanda mambo ambayo watu wanatamani
amekuwekea wewe. Samweli akachukua kichupa cha mafuta akamwagia kijana huyu ambaye
hajawahi kuwa na ndoto yakuwa mfalme na hata yeye alienda kwa Samweli sio ana mfahamu
hapana anayemfahamu Samweli ni mtumishi wa Sauli, Sauli alikuwa mbishi na
kuweka vikwazo ni kama kwamba hayaki kwenda lakini ndiye aliyewekewa. Samweli alimpaka
mafuta na kumwambia Bwana amekufanya kuwa mkuu juu ya Israel. Mungu kama bado
hajakufanya mkuu unatakiwa usubiri na ukajikuza kuwa mkuu Mungu atakupiga maana
Mungu huwapiga wajikuzao subiri wakati wa Bwana wakukufanya kuwa mkuu na kuna
eneo kabisa la wewe kuwa mkuu. Kila eneo lina watu wakuu na Bwana ndio ana wafanya
kuwa wakuu, akasema atawamiliki watu wa Bwana na utawaokoa na adui zako na sasa
nakupatia ishara ili ujue kuwa hayo mambo yatatokea, ishara ya kwanza ukitoka
hapa kwangu utafika karibia na kaburi la Raheli pale Selsa utakutana na watu
wawili hao watu watakuambia punda wakwenu wamepatikana na mzee ameanza kuhofia habari
yako hao achana nao utaendelea mbele mpaka kwenye Mwaloni wa Tabori, utafika
kwenye Mwaloni wa Gaboni utakutana na wanaume 3, wa kwanza ana wanambuzi watatu
wapili ana mikate mitatu na watatu ana kiriba cha divai, bila kuwaomba watakupa
tu, mafuta hufanya kupewa vile ambavyo hujaomba, mafuta huleta mvuto watu
watakuona una kibali kwao, mafuta ya Bwana yakufanye uwavutie watu kwenye
biashara, kazi uwe na kibali kwa watu. Usichanganye na mafuta mengine
yakukanyaga naongelea mafuta ya bwana.
Mafuta mtu akipakwa Roho wa Bwana
anamjilia kwa nguvu, neno la Bwana linatosha Yesu alipokuja kuna mambo yalikoma
maana alitupatia mamlaka akatuachia neno na neno la Bwana lina nguvu zaidi ya
mafuta, vitambaa hata Yesu hakuwa na mafuta alikuwa na neno la Bwana, Yesu
alimwambi Petro kuna baadhi ya watu wameniacha na nyie mtaniacha? Petro
akamjibu tuende kwa nani mwenye neno.
Neno la Bwana ni kali linachoma ni
jepesi kutambua mawazo ya mwanadamu fuata neno nenda neno lilipo sio mafuta wa
chumvi hapo mwanzo palikuwa na neno sio vitamba wala chumvi palikuwa na neno na
neno alikuwa kwa Mungu na neno alikuwa Mungu na vyote vilifanyika kwa huyo na
pasipo yeye hakuna ambacho kilifanyika ndani yake umo uzima na uzima ni nuru
nayo nuru ya ng`aa gizani wala giza haliwezi kulishinda.Wafalme watatu, Mfalme wa
Israel, mfalme wa Yuda na mfalme wa Moabu wamefika mahali wamekwama hakuna
maji wakaanza kuulizana jamani hivi mji
huu kweli hakuna mtu wa Mungu tumuulize, mmoja akasema kuna kijana alikuwa
anamwaga maji kwenye mikono ya Eliya, akasema huyu ana neno la Bwana, kuna kosa
kubwa linafanyika kukuza vitu ambavyo sio sahihi, kukuza vitambaa, mtu hana
neno la Bwana ila ana stoo ya maji, na neno la Bwana likae kwa wingi, Ukristo
unakuwa dhaifu kwasababu watu wanataka kunywa mafuta au kumwagiwa ila hapendi kukaa
chini kusikia neno. Yesu alikuwa mwalimu hakugawa maji wala mafuta alifundisha
neno na wakati mwingine pepo walitoka kwa kusikia neno tu. Hata kama una sura
mbaya ila una upako basi unavutia. Hata kama anakula asali ya mwitu, anavaa
nguo za singa ila anaupako basi anavutia, kijana ambaye hujaoa ila anaupako
nakuambia utaoa yeyote maana watu wataacha kazi zao wakufuate wenye pesa na wasio
nazo, wakubwa kwa wadogo watakufuata muone Yesu alikuwa na upako na watu
wakamfuata na habari zake zikaenea kotekote na wasomi wanawake wenye mali
wakamfuata nakumtumikia na mali zao. Maana anasema Roho wa Bwana yu juu yangu Bwana
amenipaka mafuta, Bwana akikupaka mafuta utavutia watu wakila aina. Yohana
walimfuata mpaka porini kwa sababu ya mafuta aliyopakwa.
Ishara ya tatu, Gibea ya Mungu palipo
na ngome ya wafilisti utakutana na manabii wanatabiri, Roho wa Bwana atakujilia
kwa nguvu nawe utakuwa mtu mwingine, kuna watu walikuwa hawafai wanaoga ila
wamefika hapa wamekuwa majasiri wananena kama sisi. Maandiko yanasema akaanza
kutabiri akashangaa watu, wakasema nini hiki kimempata mwana wa Kishi. maana Sauli
hayumo kwa manabii wala hajasoma kozi ya kunena ila ni Roho wa Mungu amemjilia
kwa nguvu. Mtu ni roho ukitaka badiliko lolote lazima lianzie rohoni na
badiliko lazima liletwe na roho ukishughulika na mtu wanje unapoteza muda maana
mtu ni roho, shughulika na roho, badiliko la mtu wanje sio la kudumu ni lamuda kitambo
tu badiliko lianzie ndani. Sulemani anasema hata ukimpiga mpumbavu ukamtwanga
kwenye kinu, bado hata badilika. Unamuona mgerasi anaishi makaburini watu
wakamshika wakamfunga wanataka kumsaidia wakamfunga wakamvisha nguo walipotoka
akavunja minyororo ili awakomeshe akaenda kukaa sehemu watu hawafiki kwenye
makaburi ila siku mmoja Yesu wa Nazareti akaenda akamkemea maandiko yanasema
baada yahapo alikuwa amekaa na Yesu na amevaa nguo na ana akili zake. Kuna mambo
mtu akiyafanya sio ya akili yake, mwanadamu ana mambo ambayo sio ya akili yake
na ambao niya akili yake ukiona mwanadamua anatembea uchi ujue sio akili yake
kama binti anatembea maziwa yako nje kama anauza maziwa ina maana hana akili zake
kuna maeneo ya mwili yako hakuna mtu anatakiwa kuyaona zaidi ya mume wako na
mkiwa wawili tu.
Kubadilika ni mtu kuanzia ndani. Alipokutana
na Yesu akamkemea akavaa nguo bila kuambiwa, kuna jambo Mungu anataka kufanya
kupitia wewe ila haitawezekana mpaka akubadilishe, Sauli alitamkiwa maneno
akabadilishwa neno la Mungu linaweza kubadilisha mtu maana neno la Mungu ni Roho
tena ni uzima. Kusikia neno la Mungu tena na tena unabadilika wengine kuhubiri,
biashara, nafasi fulani kazi sasa hivi ulivyo huna sifa ila utageuzwa kuwa mtu
mwingine, maandiko yanasema kuna mambo jicho halijawahi kuona sikio halijawahi
kusikia ameandalia wamchao. Utanzaa kufanya mambo yasiyoya asili yako watu
watashangaa. Ukipuuzia mambo ya Rohoni unapuuzia hatima yako, watu wanamuda na
shule, watu wengine hata mvua inyeshe vipi lazima uende shule au kazini ila
kanisani wingu tu ukiona hauendi kanisani.
“Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Angalia, nimemwita kwa
jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; nami
nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi
ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa
fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti,
na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.Tena, tazama, nimemchagua, awe
pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia
hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote
nilivyokuagiza; yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti
cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema; na meza, na
vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu
ya kufukizia uvumba; na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo
vyake vyote, na birika na tako lake; na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri,
na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika
kazi ya ukuhani;”Kutoka 31:1-10
Mungu anataka mtu awe fundi ila mtu
huyo sio fundi wakati huo, mtu huyo yupo jangwani wanatoka Misri kwenda Kanaani
ila Mungu anataka mtu awe fundi na hakuna veta, anatakiwa atengeneze vitu
ambavyo Musa ameona katika ulimwengu wa Roho bila kusimuliwa, Mungu anataka awe
fundi, Mungu anakuwazia jambo ila haongei nawewe, Mungu anaongea na Musa
akaongee na Bezaleli, Mungu aliongea na Samweli sio Sauli anaongea na mtu mwenye
mamlaka juu yako aje aongee na wewe. Mungu anajua kutengeneza vitu zamani
walikuwa wanachora kwenye magome ya mti, Roho wa Mungu atamgeuza. Kuendelea kusudi
la Bwana lazima ugeuzwe huwezi kwenda na akili yako hiyo Roho atawajilia kwa
nguvu, Samson hakuwa mtu wa kawaida akamwambia Delila mkininyoa nywele nitakuwa
mtu wa kawaida ina maaana hakuwa wakawaida, Samson Roho wa Mungu alimjia
kwanguvu akaenda akanyanyua geti na kupanda nalo mlimani. Kuna kazi Mungu
anataka uifanye. Kuna jambo hapa anataka ulifahamu.
“Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema;
kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe. Nawe utatelemka mbele yangu mpaka
Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa,
na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na
kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya”. 1Samweli 10:7-8
Roho atakapokujilia kwa nguvu chochote
utakachoona vema fanya hapa ndipo hatima za watu zimelala, wewe ndio unaona
vema sio jumuiya yako, mtu Mungu amemvuvia aanze biashara na anatoka kwenda
kumuuliza mtu anakuvunja moyo, ila ulivuviwa wewe pekee yako. Ishara hizi
zikitokea fanya na usipo fanya utakuwa yule yule wazamani, ukiishaona fanya
usianze vikao vya kuzungumzia fanya. Mungu anamwambia Kornelio tuma watu waende
kumuitia Petro maana zamani ilikuwa hairuhusiwi kwenda kwa Wayahudi ila Bwana amesema
tuma watu huko huko kwa hao wasiochangamana na watu. Hatima imefichwa kwenye
mambo usipofanya utabaki kuwa yule yule.
Chukua hatua kuna maelekezo ya Mungu
huonekana hayaeleweki, mpaka uchukue hatua ndio utaelewa. Ibrahim kwa Imani alipoitwa
akaitika kwa Imani akatoka asijue aendako. Eliya aliambiwa toka hapa nenda nimekuandalia
mwanamke mjane akulishe, akaenda akafika akamkuta mwanamke akamwambia naomna
maji pia njoo mkate, mwanamke akamwambia nimebakiza konzi moja ya unga na
mafuta nipike nile na mwanangu ale tukafe akamwambia nitengenezee mimi kwanza na
mwanamke akafanya hivyo akampikia Eliya kwanza na unga na mafuta hayakuisha mpaka
siku Bwana alipoleta mvua.
Maisha ni mapigano tegemea upinzani
tokea mwanzo, jiandae kutokukata tamaa mpaka ukuta uanguke. Fanya biashara
fanya ufundi mafanikio yamefichwa kwenye mambo unafanya hatua kwa hatua, kidogo
kwa kidogo hata kama hujui vingi utajua vingine mbele ya safari. Mungu
atakuandalia mtu akufundishe biashara akufundishe kwa ustahili zaidi lakini
lazima uanze anasema ameweka watu kwa ajili yako watu wa mataifa mbalimbali. Hii
dunia usipofanya kitu utakufa ujafanya chochote maana kuna watu lazima
watakupiga vita hata usipofanya.
Unaweza kusikia jambo umeanza ndio kama
unaharibu usiogope anza kufanya hapo hapo hata kama watakucheka maana hao hao
kuna siku watakushangilia ukiona vema Roho akakujia fanya uonavyo maana Bwana
yuko na wewe. Watu walinicheka sijui kuhubiri naongea ongea tu mbona hawaki, na
sikuacha nasiachi maana kuna mahubiri ya anayewaka na asiyewaka. Kuna mambo
unatakiwa ufanye na utapigwa vita ila usiache hata wakikutisha. Mungu
anamwambia Yeremia nimekuita ila watashindana na wewe ila hawatakushinda.
Mungu akujilie lile eneo ambalo
umeitiwa muombe akuongoze kwa Roho wake wa nguvu mwite naye atakuonyesha mambo.
Yesu akabatizwa akaanza kuomba kwa nguvu, Roho akamuongoza kwenda nyikani peke
yake akarudi katika nguvu za Roho mtakatifu akaanza kuhubiri neno la Mungu.
Watu wakamshangaa wakasema huyu si alikuwa seremala imekuwa je? ukijazwa na Roho
wa Mungu unakuwa watofauti kabisa utawashangaza wote maskini na matajiri unayaweza
mambo yote katika yeye atutiaye nguvu huyu Roho atakusaidia kuona mambo na
kutenda kama Mungu anavyoona. AMEN.
0 Comments