UFUFUO NA UZIMA UBUNGO
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 30 JULAI
2023
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: BARAKA YA MUNGU
Baraka ya Mungu ni nini? Tunaposema mtu
kabarikiwa mara nyingi tunaangalia ana magari kiasi gani, nyumba kiasi gani,
nguo n.k. Mungu akikupenda hakupi pesa wala mali bali baraka ambayo itakupa pesa
na mali. Ayubu alikuwa na mali zote lakini shetani alianza kushughulika vyote
alivyokuwa navyo kwa ruhusa ya Mungu.
“Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu
walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA
akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema,
Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha
BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa
hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha
Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo
Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na
nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo
mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo
yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. BWANA akamwambia Shetani,
Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu
yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.” Ayubu 1:6-12.
Ayubu alianza kupoteza mwilini kumbe makubaliano
yalishafanyika rohoni kati ya Mungu na shetani. Matukio yote yaliyompata Ayubu
yalianzia rohoni kwa mamlaka ya rohoni. Lakini pamoja na kupoteza vyote Ayubu alijua
kwamba baraka sio vitu alivyokuwa navyo bali baraka ili leta vitu.
Ilifika mahali mpaka marafiki zake ambao ni
wacha Mungu wakaanza kumhukumu kuwa Ayubu kamuacha Mungu.
Duniani wapo rafiki wa aina tatu;
- Comrade – Urafiki wenu ni kwa sababu mnapigana na adui mmoja. Aina hii ya urafiki utavunjika huyo adui akiondoka. (You share a common enemy)
- Constituents – Rafiki anayetafuta kile unachotafuta. Mfano ni mfanyabiashara na wewe mfanyabiashara wote mnatafuta hela inapelekea mnakuwa marafiki. (He/She is for what you’re for)
- Confidant – Rafiki ambaye ukifika kwake unamwambia siri zako zote na asimwambie mtu. Rafiki anayeweza kukukemea, kukupa pole na asimwambie mtu. Huyu ndiye rafiki wa kweli ambaye atakuwa na wewe wakati wa kilio chako na wakati wa kicheko chako
Yesu ni confidant wa watu wote aliowafia
msalabani na kuwaokoa.
“Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama
nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa
uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda
niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake;
lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu
nimewaarifu. Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi;
nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba
lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. Haya nawaamuru ninyi, mpate
kupendana.” Yohana 15:12-17.
Baada ya yote Mungu alimrudishiwa Ayubu vyote alivyopoteza. Kilichorudisha vyote ni baraka.
“Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo
alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo
aliyokuwa nayo kwanza.” Ayubu 42:10.
Kanuni ya neno limetajwa wapi ndio linaonyesha umuhimu
yake. Baraka kwenye Biblia inaanza kuonekana kwenye kitabu cha mwanzo.
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu,
kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama,
na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu
akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze
nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila
kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Mwanzo 1:26-28.
Kanuni ya kwanza, kubariki ni kusema. Baraka ni kusemewa/
kuambiwa maneno sawa na upoambiwa maneno kinyume ndio laana. Lile neno linaanza
kusababisha matukio kwenye ulimwengu wa roho bila wewe kujua. Magari, nyumba,
afya, familia bora n.k sio baraka ila ni matokeo ya baraka.
Elisha alitamka maneno ya laana, na maneno yale yakazaa dubu wakawala watoto. Baraka na laana yote hutokea baada ya maneno.
“Akakwea kutoka huko mpaka
Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji,
wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa! Akatazama
nyuma akawaona, akawalaani kwa jina la BWANA. Wakatoka dubu wawili wa kike
mwituni, wakawararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao.” 2 Wafalme
2:23-24.
Kanuni ya pili, mdogo hubarikiwa na mkubwa, mdogo
hawezi kumbariki mkubwa.
“Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo
hubarikiwa na mkubwa.” Waebrania 7:7.
Maneno unayotamkiwa na mkubwa ndio yanayoamua
mwisho wako. Israeli yaani Yakobo aliwabariki Efraimu na Manase hata kama
hakuwa baba yao, lakini maneno ya baraka aliyotamka Israeli yaliwabeba pia.
“Israeli akawaona wana wa Yusufu, akasema, Ni
nani hawa? Yusufu akamwambia babaye, Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa.
Akasema, Tafadhali uwalete kwangu nami nitawabariki. Na macho ya Israeli
yalikuwa mazito kwa uzee, wala hakuweza kuona. Akawaleta kwake, naye akawabusu,
na kuwakumbatia.” Mwanzo 48:8-10.
“Akawabariki siku ile akasema, Katika ninyi
Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na Manase.
Akamweka Efraimu mbele ya Manase” Mwanzo 48:20.
Yakobo aliyaumba maneno ya baraka kwa wanae. (Mwanzo
49:1-28)
0 Comments