UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 23 JULAI 2023
ASKOFU DKT. JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KABLA YA KUZALIWA ULIKUWEPO
Wewe Mungu amekuchagua tangu asili yaani kabla mbingu na nchi hazijaumbwa. Mwili ni mavumbi na utarudi mavumbini, ila wewe ni roho na itamrudia Mungu. Yesu anasema kabla Ibrahimu hajakuwepo, alikuwepo, akionyesha kuwa wana wa Mungu wapo tangu asili.
“Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.” Yohana 8:53-59.
Yesu alikuwa duniani kavaa mwili kama sisi tulivyokuwa ndani ya mwili. Kama Yesu alivyoshuka duniani sisi pia tumeshushwa duniani japo sehemu mbalimbali lakini Baba yetu ni mmoja, ni viumbe wa mbinguni na tuna kazi ya kufanya duniani. Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa Mungu Baba, na sisi ni wazaliwa wa pili kwa Mungu Baba na tumejazwa uwezo wa kuanza na kumaliza. Mungu ana watoto wake wa kiroho, Mungu ni roho na watoto wake ni roho. Mwili unachoka na kubeba mwili ni kazi. Wapo wanaoweza kumdhuru wa nje lakini wa ndani ana asili ya mbinguni.
“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Warumi 8:29.
Vita inapiganwa kwenye uliwengu wa roho na ushindi unaonekana mwilini. Ukuta unaotenganisha kushindwa na kufanikiwa ni baraka. Huwezi kumlaani aliyebarikiwa. Baraka inadesturi ya kusababisha matukio fulani ya kukupigisha hatua sehemu unayotakiwa kufika na usiyoijua. Ukibarikiwa kuna baadhi ya milango inafunguka bila wewe kujua, ni kama bahati nasibu. Yakobo alitembea kwenye baraka ya uzaliwa wa kwanza.
“Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.” Mwanzo 28:12-15.
Kama vile baraka ifanyavyo kazi vivyohivyo maneno
ya laana yanakaa mahali mpaka yatimie.
“Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine. Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.” Mwanzo 35:17-18.
"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"
0 Comments