UFUFUO
NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL
IBADA
YA JUMAPILI - 9 JULAI 2023
ASKOFU
BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: KUTAKA KWA MAOMBI
Mungu anataka kujua kutoka
kwako unataka akufanyie nini. Mungu anafahamu kuna mtu anaweza kumsaidia,
lakini hawezi kumsaidia kabla ya yule mtu kutaka kusaidiwa. Kupitia maombi ndio
Mungu anajua kuwa mtu anataka kitu gani.
"“Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.” Danieli 9:1-3.
Danieli yuko nchi ya ugeni
lakini alisoma kitabu na kujua wakati wa kutoka utumwani, lakini pamoja na
kwamba muda wa kutoka utumwani ulifika ilibidi Danieli atake kwa kuomba.
Maneno haya aliyoyasoma
Danieli kuhusu kutoka utumwani baada ya miaka sabini yaliandikwa na nabii
Yeremia.
“Basi BWANA wa majeshi
asema hivi, Kwa kuwa hamkuyasikiliza maneno yangu, angalieni, nitapeleka watu
na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe
kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi
hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyopo pande
zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha
kuzomewa, na ukiwa wa daima. Tena, nitawaondolea sauti ya kicheko, na sauti ya
furaha, sauti ya bwana arusi, na sauti ya bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia,
na nuru ya mishumaa. Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha
kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.”
Yeremia 25:8-11.
“Maana BWANA asema hivi,
Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno
langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa.” Yeremia 29:10.
Mambo huwa hayatokei kwa
kuwa ni mapenzi ya Mungu au muda umefika bali kwa kutaka kwa maombi. Mungu
hafanyi mambo kwa mapenzi ya mwanadamu, anakanuni zake za namna ya kumpa
mwanadamu kile alicho muahidi.
Wakati ukifika, ili
litokee lazima ufunge na kuomba. Danieli anatuonyesha kuna mambo Mungu aliahidi
yatatokea lakini ili uyapate lazima utake kwa kuomba.
“Vita vyatoka wapi, na
mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo
vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala
hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!”
Yakobo 4:1-2.
Namna ya kujua unayotakiwa uyapate kutoka kwa Mungu?
- Yale yalioandikwa kuhusu wewe anayotaka uyapate.
- Shauku ya ndani, ya moyoni kutaka jambo.
“Kwa maana ndiye Mungu
atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi
lake jema.” Wafilipi 2:13.
Agano jipya Mungu anakaa
ndani yetu, kila mtu aliyeokoka Mungu anaishi ndani yake kwa njia ya roho
mtakatifu. Sasa huyu Mungu aliyendani yako kuna mambo anataka uyapate. Kwa
sababu yupo ndani yako, anakupatia kutaka ili atomize jambo duniani kupitia
wewe. Usipuuzie ile sauti ya kutaka mambo ya Mungu ndani yako.
Kwanini ni muhimu kuomba ukishataka.
- Ili upate akili na ufahamu wa ki Mungu wa kuyafanya yale ambayo umeyataka. Kila jambo la Mungu linahitaji akili za ki Mungu za namna unatakiwa kufanya iwe biashara, siasa, kazi nk.
“Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za BWANA, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu; naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu. Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya. Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.” Danieli 9:20-24.
Shule inakupa akili ya mtu
wa nje lakini maombi yanakupa akili ya mtu wa ndani yaani roho. Mtu yeyote wa
Mungu kwenye siasa, biashara nk, unahitaji akili za ki Mungu.
- Maombi yanakupatia kibali kwa watu ambao wanamchango mkubwa kuyafanya yale unayotaka yatokee.
Namna rahisi ya watu
kukusaidia ni Mungu awaguse mioyo yao. Mungu akikupa kibali kuna watu watataka
tu kuwa karibu na wewe au kukusaidia. Nehemia aliomba ili apate kibali mbele ya
mfalme.
“Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nalikuwa mnyweshaji wa mfalme).” Nehemia 1:11.
Baada ya Nehemia kuomba alipata
kibali kutoka kwa mfalme kujenga ukuta. Baada ya kuomba ndipo aliposema na
mfalme maana alishapata kibali mbele ya mfalme.
“Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wo wote. Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana. Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto? Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. Mfalme akaniuliza, (malkia naye ameketi karibu naye), Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Nawe utarudi lini? Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka; nami nikampa muda. Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio ng’ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda; nipewe na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza mwitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanyizia boriti kwa malango ya ngome ya nyumba, na kwa ukuta wa mji; na kwa nyumba ile nitakayoingia mimi. Naye mfalme akanipa, kama mkono mwema wa Mungu wangu ulivyokuwa juu yangu.” Nehemia 2:1-8.
- Ili kushinda upinzani wa rohoni.
“Akaniambia, Ee Danieli,
mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana
kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka. Ndipo
akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo
wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa;
nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi
alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu
wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za
mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado.” Danieli 10:11-14.
"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"
“
0 Comments