UFUFUO NA UZIMA UBUNGO CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 27 AGOSTI 2023
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MATUKIO KATIKA DAMU YA UKOO.
Tumetoka kwenye koo na historia tofauti (we come from different background) kwa namna ya mwili. Yapo matukio yanayotembea kwenye damu ya kila ukoo, ni kama vile unavyoambiwa unafanana na Baba, Mjomba nk.
Kuna koo na familia
zinapitia matukio au matatizo yanayofanana, na matukio hayo ndio matukio katika damu ya ukoo. Kwenye Biblia tunaona ukoo unaongelewa kwenye
kitabu cha Mathayo cha ukoo wa Yesu.
“Kitabu cha ukoo wa Yesu
Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.” Mathayo 1:1.
“Yakobo akamzaa Yusufu
mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.” Mathayo 1:16.
Kama vile kuna kitabu cha
ukoo wa Yesu vivyo hivyo kuna kitabu kinachomuhusu kila mtu kwenye ukoo aliotokea kwenye ulimwengu wa roho. Yesu
kwenye mwili anatoka kwenye ukoo fulani ambao una matukio yalioufata huo ukoo
yawe mazuri au mabaya.
Ukoo unaotokea una uhusiano mkubwa na hatima yako. Matukio yanayokupata yamesukwa ndani ya damu ya ukoo unaotokea.
Kuna matukio yanayofuata kila ukoo yawe mazuri au mabaya, na ili kurekebisha
kitabu cha matukio ya damu ya ukoo wako ni lazima utumie damu ya Yesu.
Kuna mambo yanayoufuata
mwili uliozaliwa kwenye uko fulani, hivyo basi ni ngumu roho kufikia hatima iliyoandikwa
kuhusu wewe. Lile ganda la nje yaani mwili ndio linalokupa shida maana limezaliwa
ndani ya ukoo fulani wenye maagano na matukio fulani.
“yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,” Warumi 1:3.
"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"
Somo la leo linapatikana kwenye Kitabu cha "MATUKIO KATIKA DAMU YA UKOO". Wasiliana nasi kupata nakala yako kupitia maelekezo yafuatayo.
0 Comments